Taa ya ABS na VDC au SLIP LIGHT

matinel

Member
Dec 31, 2022
12
18
Habari wana jamii,

Ninagari aina ya nissan xtrail newmodel ya 2009 nimeinunua mwezi uliopita nilipoenda nayo rough road nikakuta chin inagonga balaa nilivyopeleka kwa fundi akasema stabilizing joint zimechoka na wish bone joint akabadili gari ikatulia lakin baada ya ile service pale walizalisha tatizo nikakuta kwenye dash board ile taa ya vdc na alama yake ile ya kuslip inaonekana kila nikianza kutembesha gari na kuna wakati naona kama matairi ya mbele yaanakwaruza kwaruza inafanya hivyo kwa sekunde chache then taa ya ABS inatokea baada ya hapo zinawaka constant mpaka ntakapofika ninakokwenda na brake zinakuwa zinashika kama kawaida tu niikizima nikiwasha tena tatizo linanza kujitokeza kama awali.

Hii hali inanikera nifanyaje ili niondoe hii shida.

Na siku hiyo wanabadilisha hizo stabilizing joints walibadili na brake pad pia maana zilikuwa zimeisha toka huko japan ilikokuwa inatumika.

20221227_091817.jpg
 
Kwenye gari yangu hili bati halipo mkuu, afu siyo kwamba linakwaruza mda wote yani natembesha kidogo tu ndo naanza kusikia kama brake zinakamata na kuachia afu baada ya sekunde chache taa ya abs inajitokeza baada ya hapo gari inakuwa fresh tu unaenda umbali mrefu sana tu
 
Mtoa mada sijajua upo mkoa gani Ila kama upo DAR nenda pale shaurimoyo Kariakoo kuna mafundi wazuri wa nissan, Subaru na mitsubishi Hilo tatizo lako litaisha kabisa.

Haya magari tofauti na Toyota hayataki mafundi makanjanja kwasababu Hilo tatizo ni dogo Sana lkn ukienda Kwa mafundi wetu ndo hivyo unaenda kuzalisha tatizo
 
Hizo taa zinazimwa na mashine. Upate fundi mwenye mashine nzuri anazima bila shida.

Ni kawaida Kwa Nissan X-Trail new model, ukifungua miguu zinawaka.
 
Kwenye gari yangu hili bati halipo mkuu, afu siyo kwamba linakwaruza mda wote yani natembesha kidogo tu ndo naanza kusikia kama brake zinakamata na kuachia afu baada ya sekunde chache taa ya abs inajitokeza baada ya hapo gari inakuwa fresh tu unaenda umbali mrefu sana tu
Tairi za mbele lazima liwepo..nyuma ndo hakunaga
 
Mtoa mada sijajua upo mkoa gani Ila kama upo DAR nenda pale shaurimoyo Kariakoo kuna mafundi wazuri wa nissan, Subaru na mitsubishi Hilo tatizo lako litaisha kabisa.

Haya magari tofauti na Toyota hayataki mafundi makanjanja kwasababu Hilo tatizo ni dogo Sana lkn ukienda Kwa mafundi wetu ndo hivyo unaenda kuzalisha tatizo
Mawasiliano ya hao wataalam Kiongozi. Kuna Pajero inasumbua hapa Moro.
 
Tatizo la breki kushika na kung'ang'nia limenisumbua sana kwenye Kluger!! Ukipeleka kwa fundi wanarekebisha inakuwa safi. Lakini baada ya kutembelea kidogo ukifunga breki zinashika jumla zile za mbele hadi moshi unafuka! Naomba ushauri!!
 
Tatizo lilianzaje mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom