Msaada-paypal | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada-paypal

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by donlucchese, Apr 9, 2011.

 1. donlucchese

  donlucchese JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 9,308
  Likes Received: 3,450
  Trophy Points: 280
  Nimefanikiwa kulink credt card yang na paypal. Sasa swali linakuja,pale kwenye shipping adress ivi unaweka adress yako ya posta au? Maana kwa wenzetu hususan marekani hua kuna street adress kabisa sasa mimi nakaa Goba kwa Ndambi ntafanyaje? Asanten wakuu
   
 2. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Mie mwenzio nahitaji msaada kama wewe
   
 3. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2011
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Shipping Address unatakiwa uweke address ambayo mzigo au barua inaweza kukufikia kwa kuletewa na hizi courier services kama DHL, TNT au EMS. Kama unafanya kazi ni vizuri kutumia anuani ya kazini kwako, na pia kuna sehemu unaweka namba yako ya simu, hivyo mzigo ukija tu wanakupigia simu ili wakupate. Maana huduma ya Paypal, unalipia hadi gharama ya kuletewa mzigo ulipo.
   
 4. Ikumbilo

  Ikumbilo JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 455
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naomba unijuze ulitumia CR ya bank gani?
   
 5. Ikumbilo

  Ikumbilo JF-Expert Member

  #5
  Apr 9, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 455
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naomba unijuze ulitumia CR ya bank gani?
   
 6. donlucchese

  donlucchese JF-Expert Member

  #6
  Apr 9, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 9,308
  Likes Received: 3,450
  Trophy Points: 280
  nilitumia tembo visacard mkuu
   
 7. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #7
  Apr 9, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Kuna bank, kama sikosei ni Stanbink au Exim ambazo unaweza ukawa na credit card, ila minimum balance kwenye account iwe million 3. Nijuavyo mimi bank karibu zote Tanzania zina debit card na sio credit card. Labda wataalamu watujuvye.
   
 8. Michael Paul

  Michael Paul Verified User

  #8
  Apr 10, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 60
  Mkuu hongera kwa kufanikiwa kulink kadi yako. Ninaomba utufahamishe zaidi kuhusu huduma za paypal na vigezo vya kujiunga. Shukrani.
   
 9. donlucchese

  donlucchese JF-Expert Member

  #9
  Apr 10, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 9,308
  Likes Received: 3,450
  Trophy Points: 280
  Mkuu paypal ni huduma inayokuwezesha kulipa,kupokea malipo na kununua bidhaa mtandaoni(online shopping) ni huduma ambayo ni rahis na ya uhakika na si rahisi kutapeliwa. Kikubwa unachotakiwa kuwa nacho ni kadi ya benki yenye visa au mastercard( i used tembocard visa),unaenda kwenye benk yako nakuomba kujiunga na internet banking nao wanakupa form unajaza. Baada ya hapo unaenda paypal.com na unafata procedures rahis naam ndan ya siku 2-3 utaweza kulink card yako na kununua bidhaa new york city ikaletwa mpaka mlangon kwako tandale kwa mtogore.
   
 10. s

  sniper619 Member

  #10
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Habari zenu wakuu....ningependa kuweka ujuzi wangu hapa.....na pia nina maswali.....
  Credit card ya Exim (ambayo mie ninayo)...kuna Silver (min. Balance ni 1m na unaweza kutumia hadi laki 8)...na Gold (min. Balance ni 3m)....

  Hiyo Tembo Visa Card ni kutoka benki gani?...min. Balance kiasi ngapi?....

  Halafu je mabenki wanaku-charge kuitumia hiyo credit card?...yaani kuna bank charges au bank commission yeyote?....
   
 11. Ikumbilo

  Ikumbilo JF-Expert Member

  #11
  Jun 27, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 455
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Asante Ozzie77 nitalifanyia kazi , bado ningependa kujua je ni lazima account yako iwe na dollar au Tshs?
   
 12. Osaba

  Osaba JF-Expert Member

  #12
  Jun 27, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Vyovyote sh au dola coz sh huwa wanaibadili na kuwa kwenye dola
   
 13. Osaba

  Osaba JF-Expert Member

  #13
  Jun 27, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  No paypal sio kazi yao kukupigia simu mfano kama unanunua kitu kutoka ebay au kivuko paypal kazi yao ni kuwalipa hao ebay kupitia credit card yao sasa hao ebay kazi yao ni kuufatikia mzigo wako ulipofikia na kukujulisha kupitia email,nimeitumia sana hii ebay kununulia vitu mtandaoni na software za apple kupitia paypal hao paypal huwa kuna kaasilimia kadogo sana wanakata kutokana na huduma yao,so kama uko crdb na unataka kununua vitu vya dola 500 akaunti yako isiwe chini ya laki 8 za kitanzania usiweke pesa nyingi sana kwa akaunti ya mtandao coz wajanja siku hizi ni wengi na wazungu wwenyewe nao ni wajanja sana.
   
 14. LOOOK

  LOOOK JF-Expert Member

  #14
  Jun 27, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,392
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Take care na online purchase itakuja kuku ingiza mkenge usio tarajia na usimuone wakumdai au kumshtaki unatakiwa kujua u fake haupo kwenye bidhaa tu hadi kwenye mitandao .kuna mtu sisi huku niliko alipata ichizi baada ya jamaa kukwapua 78mil na kumuachia 5elfu tu. So unatakiwa kuwa na uelewa wa kutosha sana kujua secure webs an unsecured webs sasa hiyo lazima uwasiliane na crdb au bank yeyote yenye hiyo service before kwani kuna form ambazo kwa mfano crdb wanakupa uijaze ili ili wakuingize huko kwenye hiyo huduma. Ila naungana na mdau omary salumu kwamba usiweke pesa nyingi katika a/c ambayo unatumia katika huduma ya online purchase watuwana hack hiyo card yako na unakombewa mkwanja woooooooote unaachiwa 5000/- kitunza a/c tu anbacho huwa hakitoki. Take care na huduma hii.
   
 15. Ikumbilo

  Ikumbilo JF-Expert Member

  #15
  Jun 27, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 455
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Asante kwa ushauri wako mkuu.
   
 16. Ikumbilo

  Ikumbilo JF-Expert Member

  #16
  Jun 27, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 455
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sasa kujua ipi ni nzuri ni mtihani, duh poa kwa ushauri makini.
   
 17. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #17
  Jun 27, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Paypal ni kitu kingine kabisa. Kuhusu kutapeliwa ni kwa kutumia njia zingine kulipa for online purchase na siyo paypal. Njia hizo ziko nyingi including Western Money Union, Moneygram nk. Tofauti wengine Paypal wana mikataba na hao unaonunua kwao. Kwa mfano ebay au amazon etc. In the event umenunua kitu say toka ebay na hakijakufikia after agreed time, paypal wanaku-refund pesa yote uliolipia.Kwa kifupi ni kwamba ukinunua kupitia PayPal hakuna swala la kupoteza fedha yako. Changamoto ni kujitaidi kununua vitu online ktk maduka yanayotumia huduma ya PayPal kwa malipo.
   
 18. Millah

  Millah JF-Expert Member

  #18
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwanza mkuu Paypal hawakati hata senti moja kwa mnunuzi bali wanachukua kamisheni kwa muuzaji. Pili unapolipia bidhaa kwa Paypal yaiwezekani kuibiwa, kinachofanyka ni hichi:-

  Unapojisajili kwenye Paypal wao wanaweka taarifa za akaunti yako, unaponunua bidhaa kutoka kwa muuzaji yeye hawezi kuzipata taarifa za akaunti yako ila wewe unawapelekea taarifa Paypal kisha Paypal wanamlipa fedha muuzaji aliyekuuzia wewe bila ya kumpa taarifa za akaunti yako ya benki. Hivyo basi njia hii ni salama kwenye ununuzi.

  Vile vile eBay sio wanaokutafuta wewe na kukutumia bidhaa unayonunua, eBay hawana bidhaa hata moja bali wauzaji mbali mbali huuza bidhaa zao kupitia mnada wa eBay. Kwa hiyo unaponunua bidhaa kwenye eBay uwe makini na kuhakikisha kwamba muuzaji yuko tayari kupost mzigo kuja Tanzania. Wengi huorodhesha nchi ambazo wako tayari kupost, ikiwa hakuorodhesha unaweza kumuandikia email na kumuuliza muuzaji kabla ya kununua, kama yuko tayari kupost Tanzania na atakuchaji shilingi au dola ngapi.

  Mwisho kabisa ukilipia bidhaa kwenye eBay na kulipa kwa Paypal, iwapo mzigo haukukufikia Paypal wanakurudishia fedha zako zote bila ya kukata hata senti moja. Lakini huchukua muda kama wa mwezi mmoja kufanya uchunguzi ni kwa nini mzigo haukukufikia na kuhakikisha kwamba wewe sio tapeli uliyepokea mzigo kisha unajifanya hukuupata. Mimi binafsi nilishawahi kununua simu miaka michache iliyopita, nakumbua ilikuwa ni HTC Advantage kwa £300.00, kumbe jamaa alikuwa ni tapeli akaingia mitini kwa hiyo nililipwa pesa yangu ingawa ilichukua takriban siku 40 hivi.
   
 19. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #19
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  tembo card ni ya crdb
   
 20. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #20
  Jun 28, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,024
  Likes Received: 8,508
  Trophy Points: 280
  Huduma ya paypal inamilikiwa na eBay so ukilipia via paypal kununua ebay kuna uhakika zaidi kuliko kununua amazon ama alibaba
   
Loading...