Msaada: Nyumba kuwa na matumizi makubwa ya umeme!!!

donlucchese

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
17,047
21,523
Salam wakuu,
Mwaka Jana rasmi niliunganishwa na Tanesco umeme nikaanza kupata huduma. Waliniweka kwenye Ile tariff ambayo ukiweka umeme wa elfu kumi unapata units 28. Sasa ndugu zangu changamoto iliyokua inanikabili ni kwamba hizo 28 mwezi sitoboi lazima ninunue tena umeme. Nikaenda tanesco nikaongea na mhasibu mwezi December akasema nije February wanihamishe tarrif. Cha ajabu juzi nimeenda ananiambia mbona nina matumizi makubwa sana (January takribani units 131 nimetumia). Sasa nikashangaa kwa maana ndani nina friji dogo tu (hisense) TV, subwoofer na Xbox (ambayo siitumii ipo tu). Lakini matumizi yanakua makubwa, mhasibu akaniambia kunaweza kukawa na tatizo somewhere kwenye wiring. Tatizo fundi aliyenifanyia wiring kwa sasa hayupo. Hivyo kwa wataalam WA umeme naomba mnishauri nikimtafuta fundi nimwambie aangalie vitu gani ambavyo vinapelekea umeme kutumika mkubwa kiasi hiko. Jama saa SITA mchana nilirekodi units zilizokua zimebaki ambazo NI 6.65, kuja kuangalia mchana WA Leo nimekuta zimebaki units 2.79b(takribani units 3.86) zimetumika ndani ya masaa 24. Je, shida iko wapi wakuu? Shukrani.
IMG-20230221-WA0000.jpg
 
Kaka hapo hua kuna issue kubwa mbili, kwanza ni ile earth rod hua inachoka au hakuiweka vzr, hii ilinilia sana unit kabla haijabadilishwa
Pili ni size ya waya za wiring, ita fundi aangalie vitu hivyo viwili na vingine atakavyoshauri yeye
Shukran!!
 
Kaka hapo hua kuna issue kubwa mbili, kwanza ni ile earth rod hua inachoka au hakuiweka vzr, hii ilinilia sana unit kabla haijabadilishwa
Pili ni size ya waya za wiring, ita fundi aangalie vitu hivyo viwili na vingine atakavyoshauri yeye
Shukran!!
Shukrani kaka
 
Salam wakuu,
Mwaka Jana rasmi niliunganishwa na Tanesco umeme nikaanza kupata huduma. Waliniweka kwenye Ile tariff ambayo ukiweka umeme wa elfu kumi unapata units 28. Sasa ndugu zangu changamoto iliyokua inanikabili ni kwamba hizo 28 mwezi sitoboi lazima ninunue tena umeme. Nikaenda tanesco nikaongea na mhasibu mwezi December akasema nije February wanihamishe tarrif. Cha ajabu juzi nimeenda ananiambia mbona nina matumizi makubwa sana (January takribani units 131 nimetumia). Sasa nikashangaa kwa maana ndani nina friji dogo tu (hisense) TV, subwoofer na Xbox (ambayo siitumii ipo tu). Lakini matumizi yanakua makubwa, mhasibu akaniambia kunaweza kukawa na tatizo somewhere kwenye wiring. Tatizo fundi aliyenifanyia wiring kwa sasa hayupo. Hivyo kwa wataalam WA umeme naomba mnishauri nikimtafuta fundi nimwambie aangalie vitu gani ambavyo vinapelekea umeme kutumika mkubwa kiasi hiko. Jama saa SITA mchana nilirekodi units zilizokua zimebaki ambazo NI 6.65, kuja kuangalia mchana WA Leo nimekuta zimebaki units 2.79b(takribani units 3.86) zimetumika ndani ya masaa 24. Je, shida iko wapi wakuu? Shukrani. View attachment 2526613
Duh mm umeme wa elf 10 napata unit 74nspikia, nanyooshs, nna fridgekubwa urefu nalingana nayo nna cm175,
 
Back
Top Bottom