Sababu ya Nyumba kuungua kwa tatizo la Umeme na Utatuzi wake

Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
15,857
20,710
NB:Nimeileta kama ilivyo,haijahaririwa!

Napenda kuwakaribisha katika majadiliano ya tatizo hili ambalo limekuwa likisababisha majanga makubwa sana hapa kwetu Tanzania kutokana na hasa kuongezeka kwa matumizi ya umeme.

Uchambuzi nitakao utoa hapa ni kwa majibu wa elimu yangu ya umeme pamoja ufahamu wangu juu sheria ya umeme ya kimataifa IEE regulation.

Pia uchambuzi huu utazingatia British Standard of the IEE Wiring Regulations. Kwani mfumo yetu mingi ya umeme ya Kiafrika hata ule wa Tanzania ume-copy kutoka katika regulation hizi kubwa mbili duniani.

Na sababu ya kutumia IEE wiring regulation ambayo ni ya British standard 7671 ni kwa sababu inazungumzia sheria na kanuni za umeme wa kiwango cha 230V kwa single phase. Ambao ndiyo shirika la umeme Tanzania Tanesco linausambaza kwenye makazi ya watu.

1. MAKOSA YANAYO SABABISHWA NA MAFUNDI KWENYE KUFANYA WIRING.

(a). Overload of power supply wire: Hii husababishwa na line moja ya power supply kutoka katika main switch kutumika kusambaza umeme katika yumba vingi.

Mfano nyumba nyingi mafundi hutumia 2.5 mm2 wire kama supply ya kwenye vyumba, supply hii hutumika kama junction supply ya vyumba vingine.

Wire ya 2.5 mm2 kitaalamu mwisho wake wa kupitisha current kiusalama ni 20Ampere ikitokea current zaidi ya ishirini ikalazimishwa kupita katika waya ya namna hii husababisha waya kupata moto, kama hali hii itakua kubwa sana waya uungua. Na huenda ukasababisha moto.

(b). Current ya Miniature Circuit Breaker(MCB): kuwa kubwa kuliko current ya wire. Mfano wire wa 2.5 mm2 tumeona una uwezo wa kupitisha 20 Ampere kiusalama, hivyo MCB yake inatakiwa iwe ya 20Ampere.

Lakini mafundi wengine kwa kujua au kuto kujua
hujikuta wanafunga MCB zenye current kubwa zaidi ya wire husika, hali hii huweza kusababisha wire husika kuungua kwani MCB itashindwa kujizima hata pale wire itakapo kuwa imefikia kiwango chake cha mwisho cha kupitisha current. Matokeo yake wire husika unaweza kuungua na kusababisha moto.

Viwango sahihi vya MCB na size ya waya zake zinazo shauriwa kimataifa ni hizi hapa: 1.5 mm2 cable - 15 amp miniture circuit breaker.2.5 mm2 cable - 20 amp miniture circuit breaker.4 mm2 cable - 25 amp miniture circuit breaker.

6 mm2 cable - 32 amp miniture circuit breaker.10 mm2 cable - 40 amp miniture circuit breaker.

(c). Loose Connection: katika maungio ya waya na kwenye vifaa vinavyo funga waya kwa screw. Kama fundi hato kaza waya vizuri wakati wa kuziunga pamoja katika viungo vya screw au waya kwa waya ni chanzo kikubwa cha kutokea kwa cheche ambazo
hatimaye huweza kuanzisha moto.

(d). Tabia ya mafundi umeme kukubali kuunga mfumo wa wiring wa nyumba nyingine dhidi ya nyumba nyingine. Kwa kawaida Tanesco huingiza umeme katika nyumba kutokana na plan pamoja na mahitaji ya kiwango cha umeme cha nyumba husika(Kilowatt Hour).

Hili hujumuisha ukubwa wa size ya waya wa kuingiza
umeme katika nyumba yako n.k Pia waya unao ingiza umeme kutoka katika meter kwenda ndani ya nyumba (tail wire) mara nyingi size yake hutegemea mahitaji ya nyumba husika.

Hivyo nyumba inapo pewa umeme hua imejitosheleza kwa mahitaji yake binafsi kitaalamu. Inapotokea nyumba nyingine ikaungwa katika mfumo huo wakati plan yake haikuhusishwa wakati wa kufunga umeme katika nyumba ya awali hali hii hupelekea OVERLOAD katika tail wire hali ambayo inaweza kupelekea wire hiyo kuungua na kusababisha moto.

2. MAKOSA YA SHIRIKA LA USAMBAZAJI UMEME

(a). Kuto funga Vilinda circuit wakati wa kufunga meter za umeme. Shirika la usambazaji umeme ni lazima lihakikishe
linaweka vifaa vya kulinda nyumba husika dhidi ya matatizo ya umeme.

Shirika la umeme ni lazima liweke vifaa kama vile CUT-OUT au CRCUIT BREAKER kabla ya umeme haujaingia katika METER ya umeme au ndani ya nyumba Ufungaji wa vifaa hivi ulikua unazingatiwa sana zamani (sababu licha ya kuwa kama fuse CUT-OUT zilitumika kukata umeme katika nyumba pale mteja akishindwa kulipa bill ya umeme).

Sasa baada ya kuingia kwa meter za LUKU imeonekana kama CUT-OUT hazina maana tena hivyo suala lake la kutumika kama kifaa cha kulinda mfumo wa umeme kama fuse limepuuziwa. Kuna baadhi ya nyumba zimefungwa CUT-OUT hadi sasa licha ya kuwa zinatumia LUKU, pia kuna wenye bahati ambao mita zao zina Circuit breaker.

Ufungaji wa umeme usio zingatia vifaa hivi,unaongeza uwezekano mkubwa wa kutokea short ya umeme yenye madhara. Kama umeingiziwa umeme katika nyumba yako halafu vifaa nilivyo vitaja hapo juu hujafungiwa hata kimoja (yaani umeme umetoka katika bracket na kuingia katika meter moja kwa moja bila kupitia katika CUT-OUT au CIRCUIT BREAKER ) mfumo wako wa umeme si salama ni haki yako kufungiwa vitu hivyo una haki ya kudaibkwa usalama wa nyumba yako.

(b). Miundo mbinu mibovu ya shirika la ugavi wanumeme. Hali hii hupelekea kukatika katika hovyo kwa umeme, hali hii huweza kuzalisha Electrical Surges ambazo huweza kuleta madhara kwa watumiaji wa umeme.

3. KUCHAKAA KWA WIRING ,VIFAA BANDIA NA VIFAA VIBOVU.

(a) Circuit breaker mbovu au feki. Kuna circuit breaker nyingine mbovu au bandia ambazo zinashindwa kujizima pale short ikitokea, hakikisha unaijaribu circuit breaker yako mara kwa mara kwa kubonyeza “trip test” kuona kama inafanya kazi au la.

(b) Switch za umeme na extension cables ambazo ni mbovu au hazijakidhi vigezo(bandia)ni chanzo kikubwa cha moto katika makazi yetu. Vifaa kama vile switch ambazo zimesha haribika vibadilishwe ili kuepuka kutokea kwa moto. Pia epuka kutumia Extension cables ambazo ni bandia.

(c) Wiring iliyo chakaa huweza kusababisha kutokea kwa moto kutokana na kulegea kwa viungo vyake ambavyo husababisha chehe, pia wire zake huwa zimeshambuliwa sana na wanyama na wadudu hivyo zinaweza zikagusana na kusababisha short yenye kupelekea moto kutokea.

4. KUFANYA MATENGENEZO YA VIFAA VYA UMEME NA KUVITUMIA BILA KUWA NA UTAALAMU:

Watu wengi wamekuwa wakifanya matengenezo ya vifaa vya umeme angali hawana utaalamu wa umeme. Vifaa vyote vya umeme ni lazima vikatengenezwa na mtu ambaye amesomea kazi hiyo.

Mfano watu wengi hubadilisha fuse katika mifumo mbalimbali ya vifaa vya umeme pale zinapoungua. Ubadilishaji wa fuse hizi mara nyingi hufanyika
kiholela bila kuzingatia kiwango cha current cha fuse husika. Hali hii husababisha fuse husika kuto kukatika wakati short ikitokea, hivyo huweza kupelekea waya kuuungua napengine kusababisha short ya umeme.

5. KUJAZA VIFAA VINAVYO TUMIA UMEME KATIKA EXTENSION CABLE KUZIDI UWEZO WAKE:

Extension cable zimetengenezwa kwa uwezo tofauti tofauti. Hakikisha hauzidishi vifaa vya umeme vinavyo chukua umeme kupitia extension cable yako ili kuepuka uwezekano wa extension cable hiyo kuungua.

SOLUTION 1. 1. Makosa haya makubwa matano yanaweza yakaepukika kwa kila mmoja kufata utaratibu na kanuni za ndani ya nchi na za kimataifa zinazo simamia matumizi bora ya umeme.

2. 2. Walaji wa umeme wawe na utaratibu wa kukagua mifumo yao ya umeme mara kwa mara kupitia
wataalamu wa umeme, ili kuthibitisha usalama wa
mfumo wake wa umeme katika nyumba yake.

Utaratibu huu wa ukaguzi ni muhimu ambapo mtaalamu
atakagua kama wiring system yako imekidhi vigezo; ambapo mtaalamu wa umeme hutakiwa kuchukua
vipimo maalumu na kuangalia kama mfumo wako wa umeme umekidhi kanuni na taratibu zinazo simamia mifumo ya umeme.

Baada ya vipimo mtaalamu huyo hutakiwa kuandaa ripoti yenye taarifa ya ukaguzi na kutoa matokeo ya ukaguzi huo wa mfumo wa umeme katika nyumba
yako. Mkaguzi atatoa majibu makuu matatu kulingana na
sheria na kanuni za mifumo ya umeme majumbani kuwa mfumo wako wa umeme ni Salama,Salama
kidogo, unahitaji marekebisho au si salama. Report hiyo ataisaini na kukukabidhi.

3. Ufungaji wa vifaa vinavyo tambua ishara ya kutokea kwa moto(fire sensor)

1. 4. Kuepuka kufanya matendo ambayo yatapelekea kutokea kwa tatizo la umeme ambalo linaweza kusababisha moto.

5.Kuwa na vifaa vya kuzimia moto katika majumba yetu. An electrical fault will not give you a chance to correct your mistake,so BE CAREFUL!

Kwa mawasiliano na na shunghuli zote zinazo husu umeme wasiliana nami kwa 0674656694 / whatsapp

Source:Umeme Services Compant Ltd.
 
Maelezo mengi. Nikajua ntaona fidia inakua ya namna gani na nini kifanyike mteja anapounguliwa nyumba maana hapo juu umeanza na neno sheria alafu maelezo umeelezea usalama.
 
Maelezo mengi. Nikajua ntaona fidia inakua ya namna gani na nini kifanyike mteja anapounguliwa nyumba maana hapo juu umeanza na neno sheria alafu maelezo umeelezea usalama.
Mimi nimesaidia tu kwa ufahamu wangu nilio nao,ili watu wachukue tahadhari hasa kwa sababu ya tatizo la umeme lililopo sasa.Mada hii nimeileta on request.Niliona kwa vile mtu mmoja ame-request,niilete kama bandiko linalojitegemea,ili watu wajue what actually causes a fire as related to electrical faults,kwa pande zote mbili,wateja wa TANESCO na TANESCO yenyewe, maana TANESCO mara nyingi inaruka kimanga.Naamini hii ni muhimu.Sasa kama wewe huoni hivyoo,pita tu.
 
Mimi nimesaidia tu kwa ufahamu wangu nilio nao,ili watu wachukue tahadhari hasa kwa sababu ya tatizo la umeme lililopo sasa.Mada hii nimeileta on request.Niliona kwa vile mtu mmoja ame-request,niilete kama bandiko linalojitegemea,ili watu wajue what actually causes a fire as related to electrical faults,kwa pande zote mbili,wateja wa TANESCO na TANESCO yenyewe, maana TANESCO mara nyingi inaruka kimanga.Naamini hii ni muhimu.Sasa kama wewe huoni hivyoo,pita tu.
Mhhhh,.
Sawa.
 
Mhhhh,.
Sawa.
Unajua mkuu hata kufuatia compensation baada ya nyumba yako kuungua,ni lazima kwanza ujue kuna uwezekano wa kupata,sasa hili bandiko linakupa picha kwamba TANESCO wanaweza kuunguza nyumba za watu kwa yale yanayoendelea sasa,so they can be sent to court for endangering human life and property!
 
Circuit breaker watoe tanesco ili kuepuka zisizo na kiwango na wawajibike zitakapoleta tatizo,fundi majukumu yake yaanzie kwenye main switch.
 
Unajua mkuu hata kufuatia compensation baada ya nyumba yako kuungua,ni lazima kwanza ujue kuna uwezekano wa kupata,sasa hili bandiko linakupa picha kwamba TANESCO wanaweza kuunguza nyumba za watu kwa yale yanayoendelea sasa,so they can be sent to court for endangering human life and property!
Nimeelewa mzee mwenzangu
 
circuit breaker watoe tanesco ili kuepuka zisizo na kiwango na wawajibike zitakapoleta tatizo,fundi majukumu yake yaanzie kwenye main switch.
Tatizo ni kwamba wiring ndani anafanya mkandarasi,sio TANESCO.Anyway ni wazo zuri.Ila wakandarasi wengi wanajua haya mambo,kwa hivyo hata mkandarasi akikushauri ukanunua mwenyewe is fine.
 
Back
Top Bottom