Msaada: Nimetupiwa kipande nateseka mwaka wa 3 sasa, nahitaji msaada

Hapa wengi hawawezi kukuelewa vita katika maisha hasa ya biashara ni kubwa sana.. Pole sana naamini utapata msaada!.
Sasa nakupa huduma ya kwanza kama unahisi unaweza fanya ukiona haikufai chukua majivu loweka kwenye ndoo oga then chukua malumba lumba wengine wanaita kivumbasi na yawe majani weka kwenye sufulia chemsha jifukize hayo majani yawe mengi baada ya kujikiza acha yapoe na uyaoge huku ukijisugua na hayo majani kwa manuizi ya matatizo yako
 
Kama utani lakini unaumia hivo.
Kufanikiwa kuna hitaji ukomavu na roho ngumu haswaa.
Hapo ndo umeingia ulingoni sasa kadiri utakavokuwa unarudia hali yako ya zamani mdo kadiri utapingwa.
 
Kwanza samehe wale wote waliokukosea na ambao umewakosea uwasamehe kabisa. halafu nenda kanisani au msikitini na utoe sadaka ya urejesho wa nafsi Yako,maana inawezekana wachawi wameichukua nafsi Yako nzuri wakakuvalisha kivuli kinachokuzuia na kuwaogopa watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Biashara ni fursa iliyo machoni, kama hiyo fursa ikiisha muda wake basi hakuna biashara tena. Unless uwe marketing genius. Hakuna bahati wala uchawi, bali ni kusoma uhalisia na mazingira.

Kama hiyo biashara imebuma, badala ya kulialia. Kaa chini tafuta solution ufanye biashara nyingine. Ndio maana nasema kabla hujafanya biashara, soma kuhusu biashara. Sababu hiyo ni profession kama professions nyingine.

Kile kitendo tu cha wewe kuamini umelogwa, tayari ni tatizo, na linapoanzia hapo. Sababu akili yako haitofanya chochote kutokana na hiyo excuse ya kijinga.

Uchawi na imani nyingine zitakupoteza na kukutia kwenye shimo utaloshindwa kutoka milele. Fanya kitu kingine.
Me nadhani kama wewe unahisi labda pengine wengine hawana akili ya kupambanua mambo ni vema uka skip post huwez pungukiwa kitu mkuu. 🙏🏻
 
Wewe Utapona Kanisani, inabidi urudi Kanisani...!

Ongeza sana Imani yako, isiwe na shaka ndani yake....!

Nakupa Siri ya kupona kwenye maombi...!

Kabla ya maombi, ya Mchungaji yoyote, Amini kuwa umeshapona, Amini kuwa tatizo lako lilikwisha, na sasa ni mtu huru, mwambie Mungu asante .... Hii iwe kabla ya maombi.

Usiende tena kwa Mganga yoyote, Usiende Jumapili Kanisani jumatatu kwa Mganga...!

Katika Jina la Yesu utakua mzima kama zamani, narudia tena...!

Wachawi na Majini huwa wanaogopa sana mtu akiamua ku deal nao kwa njia ya maombi.... Huwa wanaogopa, kwa sababu nnguvu ya Mungu kupitia Mchungaji inapoachiliwa ili ifanye kazi huwa ni over 100%... Thats wy wannaogopa...!

Ila ukienda kwa Mganga tu, Majini na Wachawi hawaogopi tena, sabbabu ni Vita wanavyoweza kupigana, Ni vita ambapo uwezo wa Nguvu unazidiana.

Mwammbie Mungu akusamehe, na umuhaidi hutoenda tena kwa Mganga maisha yako yalobaki, then jenga imani upya, na utashinda.

NAKAZIA
 
Ametupiwa kipande 🤔🤔🤔

Uzi wa kupata mume / mke mwenye akili nilisema wa Tanzania tunaamini sana ushirikina. Hivyo ni ngumu kupata mwenza asieamini ushirikina Tanzania.

Maneno ya jamaa kutupiwa kipande ni ushahidi wa wazi
 
Habari wana jamvi, kama kichwa cha habari kinavyo jieleza ntaomba kuelezea kwa uchache changamoto ninazopitia kwa miaka 3 sasa. Ikibidi nitaandaa treads ya kusimulia mkasa mzima toka ulivyo anza mpaka hali niliyonayo kwa sasa.

Nipende tu kuwaomba wale wenye itikadi za kidini kukaa pembeni kwanza kwani kama hujapitia shida kubwa ktk maisha huwezi kujua kuwa kuna ya walimwengu pia.

Niende kwenye mada, mimi ni kijana wa kiume ambae kazi yangu kubwa ni media producer & fundi wa vifaa vya umeme. Nilihamia wilaya hii iliyoko mkoa x kutoka wilaya nyingine ya mkoa huu huu ili kufata fursa za kibiashara. Mwanzo mambo yalienda vizuri sana na kutokana na kazi yangu iliniwezesha kusafiri mara kwa mara nje na ndani ya mkoa.

Nitafupisha stori, mwanzoni mwa mwaka juzi ndipo nilianza kuona mabadiliko ktk biashara zangu ikawa hata mteja ukimpa bei akaomba punguzo na ukamkubalia ila haitachukua dakika kadhaa kukupigia kuwa ameahirisha kazi hiyo lakini nikifatilia nakuta amefanya kazi sehemu nyingine na haina ubora kama ninavyofanya mimi.

Kifupi niliona ni masuala tu ya kibiashara kufanya au kutokufanya kazi na mteja, lkn hali ikazidi kuwa mbaya kwangu binafsi hata nikienda kazini kwangu ni kulala na hakuna wateja, akienda mwingine kuna nafuu japo hela ya matumizi inapatika. Kiukweli naumia kuona nimewekeza almost vifaa + ofisi zaidi ya 10ml lkn unapata hela ya kula tu hata kodi naelekea kushindwa kilipa.

Kwa muda wote huo mabadiliko yalianza kwangu kuhisi naogopa watu, kujitenga hata sikuwa na ujasili tena ambao nilikuwa nao wa kwenda kwenda kukusanya habari kwenye mikutano, makongamano, sherehe nk kwani watu wamekuwa wakiona kama kitu flani cha ajabu hivi wengine kupelekea kukucheka 😭😭 jambo ambalo limeniathiri sana kisaikolojia, nikiwa na maana kuwa watu wanao cheka ni ambao tunafahamiana nao miaka kadhaa toka nihamie hapa ikiwa kipindi sina tatizo lolote. (Jaribu kuwaza ikiwa wewe ikatokea siku staff wenzo, watu wako wa karibu pengine na familia wanakucheka, kukusengenya na kukudhihaki huku unawaona ni jambo gani utafanya?).

Mpaka sasa nimebaki pekeangu hakuna rafiki wala watu wa dini kuwa karibu tena na mimi, nimebaki na familia yangu hasa mke na watoto ndo wafariji wangu. Na kinachoniumiza zaidi ni mama yangu ambaye kwa sasa anasumbuliwa na pressure iliyotokana na kuniona nikiwa ktk hali hii na jinsi jamii inavyo ni treate kwani mimi ndiye msaada mkubwa kwake.

Kwa muda wote huo nimekuwa nikitafuta suluhiso la tatizo hili, ni nilianzia kwenye maombi miezi kadhaa bila mabadiliko ndipo nikashauriwa kuangalia tiba asili napo nimepita maeneo mengi ya ndani na nje ya mkoa. Kikubwa ambacho nimeambiwa na wengi ni kwamba NIMETUPIWA KIPANDE. Kifupi nimepotea fedha nyingi mpaka sasa na uchumi wangu umeyumba bado sijapata nafuu ya tatizo sababu siwezi kusema kuwa labda wale wataalam wa tiba asili kuwa walikuwa matapeli, hapana sababu kila mtu anao uwezo wake ktk kutatua matatizo ya watu, ndio maana nikaja huku kuomba msaada wa kupata matibabu kwani hali ni mbaya ndugu zangu na familia wananitegemea na sioni nuru mbeleni sababu nimekuwa nikiota ndoto za ajabu ajabu na za kutisha mara nyingi, mara uote unazikwa mara unabeba jeneza nk. 😭.

Japo wengine hufikiria kujiua ili kuondokana na hizi shida za dunia lakini mimi NASEMA KAMA MUNGU ALIRUHUSU MATATIZO HAYA KUNIPATA BASI ASIPORUHUSU KUPATA MSAADA WA KUPONA KABISA BASI NITAISHI HIVIHIVI, SIWEZI KUJIUA.

Naomba nifupishe stori na kuwasilisha kwenu. Kama kuna mtu anaweza nisaidia tiba, namna ya kupona nitashukuru sana.

Mungu awabariki kwa muda wenu.
🙏🏻🙏🏻

Mshana Jr
Hizb Tahrir Tanzania
Hizbu Sharifu
Pole sana, labda ujaribu kutafuta tafsiri ya hizo ndoto unazoziota mfano unaota unazikwa au kubeba jeneza. Kingine hiyo nyota yako wamekuibia. Jaribu kwenda Pemba nasikia kuna traditional healers wazuri sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom