Msaada: Nimetupiwa kipande nateseka mwaka wa 3 sasa, nahitaji msaada

Wewe Even MOre kuwa sawa ni simple sana.

Unachopaswa ni kufunguka zaidi kuhusu...
unapatikana mkoa gani?
Mazingira unayoishi yakoje?
Watu wako wa karibu ni akina nani?
Wewe ni dhehebu gani?

Ili usaidike mazima kwa nguvu ya MUNGU aliye juu zaidi.
 
Kwa namna ulivyoandika mtu hawezi kuelewa mkuu, ila kama ni mambo ya giza na hata mengine yoyote usihangaike kwa waganga, chukua muda piga magoti omba kwa Mungu atakusaidia hapo hauhitaji kupoteza hela yako maana ameahidi kutusaidia

ISA. :41:10
usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu

NB: Hayo matokeo siyo ya kumtendea mwenzako vibaya ikiwa ni hivyo Nenda upatane naye kwanza
 
kipande ndiyo nini?ila jaribu kufanya maombi hasa saa 6-8 usiku pia funga siku 7,mungu hamtupi mja wake nilikuwa kama wewe nilienda sana kwa waganga mwisho wanakwambia uwe kama wao kutokna na majini uliyo nayo mara nyingi hawakusaidii ila wanakupa unafuu wa kukuangamiza.

huna kipande,wala kitambulisho omba kwa imani yako...omba kupitia shida walizokuwa nazo mitume wao ndiyo kiigizo chetu mfano nabii Muhammad alirogwa ila mungu alimpa dua ya kusoma hivyo utasema kwa imani yako kuwa mungu mtume fulani alikuwa ni mwenye matatizo kadhaa wewe hukumuangusha ila ulimuinua kwa maadui na mimi naamini uwepo wako ndiyo umenipa hili jambo na wewe unaweza kuliondoa kupitia maombi haya na funga hizi..

waganga msiwape utajiri wa bure.
 
Nimebaki na familia yangu hasa mke na watoto ndo wafariji wangu. Na kinachoniumiza zaidi ni mama yangu ambaye kwa sasa anasumbuliwa na pressure iliyotokana na kuniona nikiwa ktk hali hii na jinsi jamii inavyo ni treate kwani mimi ndiye msaada mkubwa kwake.

Kwa muda wote huo nimekuwa nikitafuta suluhiso la tatizo hili, ni nilianzia kwenye maombi miezi kadhaa bila mabadiliko ndipo nikashauriwa kuangalia tiba asili napo nimepita maeneo mengi ya ndani na nje ya mkoa. Kikubwa ambacho nimeambiwa na wengi ni kwamba NIMETUPIWA KIPANDE.

Kifupi nimepotea fedha nyingi mpaka sasa na uchumi wangu umeyumba bado sijapata nafuu ya tatizo sababu siwezi kusema kuwa labda wale wataalam wa tiba asili kuwa walikuwa matapeli, hapana sababu kila mtu anao uwezo wake ktk kutatua matatizo ya watu, ndio maana nikaja huku kuomba msaada wa kupata matibabu kwani hali ni mbaya ndugu zangu na familia wananitegemea na sioni nuru mbeleni sababu nimekuwa nikiota ndoto za ajabu ajabu na za kutisha mara nyingi, mara uote unazikwa mara unabeba jeneza nk. 😭.

Japo wengine hufikiria kujiua ili kuondokana na hizi shida za dunia lakini mimi NASEMA KAMA MUNGU ALIRUHUSU MATATIZO HAYA KUNIPATA BASI ASIPORUHUSU KUPATA MSAADA WA KUPONA KABISA BASI NITAISHI HIVIHIVI, SIWEZI KUJIUA.

Naomba nifupishe stori na kuwasilisha kwenu. Kama kuna mtu anaweza nisaidia tiba, namna ya kupona nitashukuru sana.

Mungu awabariki kwa muda wenu.
🙏🏻🙏🏻

Mshana Jr
Hizbu Sharifu
Nenda Nachingwea
 
Nmerekebisha
Kwa namna ulivyoandika mtu hawezi kuelewa mkuu, ila kama ni mambo ya giza na hata mengine yoyote usihangaike kwa waganga, chukua muda piga magoti omba kwa Mungu atakusaidia hapo hauhitaji kupoteza hela yako maana ameahidi kutusaidia

ISA. :41:10
usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu

NB: Hayo matokeo siyo ya kumtendea mwenzako vibaya ikiwa ni hivyo Nenda upatane naye kwanza
Story ilikuwa nusu sasa iko kamili kasome tena
 
Kwa namna ulivyoandika mtu hawezi kuelewa mkuu, ila kama ni mambo ya giza na hata mengine yoyote usihangaike kwa waganga, chukua muda piga magoti omba kwa Mungu atakusaidia hapo hauhitaji kupoteza hela yako maana ameahidi kutusaidia

ISA. :41:10
usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu

NB: Hayo matokeo siyo ya kumtendea mwenzako vibaya ikiwa ni hivyo Nenda upatane naye kwanza
Ndg sijui ni nani wala watu gani wanaohusika ktk hili cz nimeambiwa ni kwenye masuala ya ki biashara
 
Habari wana jamvi, kama kichwa cha habari kinavyo jieleza ntaomba kuelezea kwa uchache changamoto ninazopitia kwa miaka 3 sasa. Ikibidi nitaandaa treads ya kusimulia mkasa mzima toka ulivyo anza mpaka hali niliyonayo kwa sasa.

Nipende tu kuwaomba wale wenye itikadi za kidini kukaa pembeni kwanza kwani kama hujapitia shida kubwa ktk maisha huwezi kujua kuwa kuna ya walimwengu pia.

Niende kwenye mada, mimi ni kijana wa kiume ambae kazi yangu kubwa ni media producer & fundi wa vifaa vya umeme. Nilihamia wilaya hii iliyoko mkoa x kutoka wilaya nyingine ya mkoa huu huu ili kufata fursa za kibiashara. Mwanzo mambo yalienda vizuri sana na kutokana na kazi yangu iliniwezesha kusafiri mara kwa mara nje na ndani ya mkoa.

Nitafupisha stori, mwanzoni mwa mwaka juzi ndipo nilianza kuona mabadiliko ktk biashara zangu ikawa hata mteja ukimpa bei akaomba punguzo na ukamkubalia ila haitachukua dakika kadhaa kukupigia kuwa ameahirisha kazi hiyo lakini nikifatilia nakuta amefanya kazi sehemu nyingine na haina ubora kama ninavyofanya mimi.

Kifupi niliona ni masuala tu ya kibiashara kufanya au kutokufanya kazi na mteja, lkn hali ikazidi kuwa mbaya kwangu binafsi hata nikienda kazini kwangu ni kulala na hakuna wateja, akienda mwingine kuna nafuu japo hela ya matumizi inapatika. Kiukweli naumia kuona nimewekeza almost vifaa + ofisi zaidi ya 10ml lkn unapata hela ya kula tu hata kodi naelekea kushindwa kilipa.

Kwa muda wote huo mabadiliko yalianza kwangu kuhisi naogopa watu, kujitenga hata sikuwa na ujasili tena ambao nilikuwa nao wa kwenda kwenda kukusanya habari kwenye mikutano, makongamano, sherehe nk kwani watu wamekuwa wakiona kama kitu flani cha ajabu hivi wengine kupelekea kukucheka 😭😭 jambo ambalo limeniathiri sana kisaikolojia, nikiwa na maana kuwa watu wanao cheka ni ambao tunafahamiana nao miaka kadhaa toka nihamie hapa ikiwa kipindi sina tatizo lolote. (Jaribu kuwaza ikiwa wewe ikatokea siku staff wenzo, watu wako wa karibu pengine na familia wanakucheka, kukusengenya na kukudhihaki huku unawaona ni jambo gani utafanya?).

Mpaka sasa nimebaki pekeangu hakuna rafiki wala watu wa dini kuwa karibu tena na mimi, nimebaki na familia yangu hasa mke na watoto ndo wafariji wangu. Na kinachoniumiza zaidi ni mama yangu ambaye kwa sasa anasumbuliwa na pressure iliyotokana na kuniona nikiwa ktk hali hii na jinsi jamii inavyo ni treate kwani mimi ndiye msaada mkubwa kwake.

Kwa muda wote huo nimekuwa nikitafuta suluhiso la tatizo hili, ni nilianzia kwenye maombi miezi kadhaa bila mabadiliko ndipo nikashauriwa kuangalia tiba asili napo nimepita maeneo mengi ya ndani na nje ya mkoa. Kikubwa ambacho nimeambiwa na wengi ni kwamba NIMETUPIWA KIPANDE. Kifupi nimepotea fedha nyingi mpaka sasa na uchumi wangu umeyumba bado sijapata nafuu ya tatizo sababu siwezi kusema kuwa labda wale wataalam wa tiba asili kuwa walikuwa matapeli, hapana sababu kila mtu anao uwezo wake ktk kutatua matatizo ya watu, ndio maana nikaja huku kuomba msaada wa kupata matibabu kwani hali ni mbaya ndugu zangu na familia wananitegemea na sioni nuru mbeleni sababu nimekuwa nikiota ndoto za ajabu ajabu na za kutisha mara nyingi, mara uote unazikwa mara unabeba jeneza nk. 😭.

Japo wengine hufikiria kujiua ili kuondokana na hizi shida za dunia lakini mimi NASEMA KAMA MUNGU ALIRUHUSU MATATIZO HAYA KUNIPATA BASI ASIPORUHUSU KUPATA MSAADA WA KUPONA KABISA BASI NITAISHI HIVIHIVI, SIWEZI KUJIUA.

Naomba nifupishe stori na kuwasilisha kwenu. Kama kuna mtu anaweza nisaidia tiba, namna ya kupona nitashukuru sana.

Mungu awabariki kwa muda wenu.
🙏🏻🙏🏻

Mshana Jr
Hizb Tahrir Tanzania
Hizbu Sharifu
You can't serve Devil forever.
 
Wewe Utapona Kanisani, inabidi urudi Kanisani...!

Ongeza sana Imani yako, isiwe na shaka ndani yake....!

Nakupa Siri ya kupona kwenye maombi...!

Kabla ya maombi, ya Mchungaji yoyote, Amini kuwa umeshapona, Amini kuwa tatizo lako lilikwisha, na sasa ni mtu huru, mwambie Mungu asante .... Hii iwe kabla ya maombi.

Usiende tena kwa Mganga yoyote, Usiende Jumapili Kanisani jumatatu kwa Mganga...!

Katika Jina la Yesu utakua mzima kama zamani, narudia tena...!

Wachawi na Majini huwa wanaogopa sana mtu akiamua ku deal nao kwa njia ya maombi.... Huwa wanaogopa, kwa sababu nnguvu ya Mungu kupitia Mchungaji inapoachiliwa ili ifanye kazi huwa ni over 100%... Thats wy wannaogopa...!

Ila ukienda kwa Mganga tu, Majini na Wachawi hawaogopi tena, sabbabu ni Vita wanavyoweza kupigana, Ni vita ambapo uwezo wa Nguvu unazidiana.

Mwammbie Mungu akusamehe, na umuhaidi hutoenda tena kwa Mganga maisha yako yalobaki, then jenga imani upya, na utashinda.
Soma hapa na uelewe nakutakia Kila la kheri katika Maisha yako mapya
 
Fanya kazi kwa bidii.
Soma media production na mambo mengine yanayohusiana nayo ili uwe more creative.
Jifunze biashara ya media.
utaona mabadiliko.
🙆🏻‍♂️ asee! Jaribu urudie kusoma vzr story nimeirekebisha nadhan utanielewa tu. Kifupi mimi ni experienced media producer VIDEO, GRAPHICS and Printing kwa ujumla wake na nina ofisi kabisa na haya matatizo yamenipata baada ya kufungua ofisi.
 
Nyie mnaobeza waganga na kutukuza wachungaji mnamaanisha nini?
Binafsi niliamshwa kwa dawa ya mganga,

Ndio nikazinduka toka Gizani, shimoni, vifungoni.

Nilipoanza kuendelea kujiweka sawa zaidi,
Kupitia njia za waganga, ikashindikana.

Nikaanza kufatilia kanuni za kuishi Kiuokovu,

Now namshukuru Mungu.
 
Icho kipande Ulicho Tupiwa Ni Jini Maiti. Ushaidi Ni izo Ndoto Mbili Ulizo Taja Kuota Unazikwa Au uko Msibani, Tabia Ya Jini Maiti Nikuzika Kuanzia Mawazo Yako Unayo Waza Kichwani, Inaonekana Ilo Jini Limekaa Kwenye Mlango Wako Wa Aja Apa Na Maanisha Matamanio Yako Yale Unayo Taka Aya Timiii. Ila Kumbuka Mtu Wa Mbali Awezi Kuloga Chunguza Ukoo Wako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom