Msaada: Nimepewa siku 30 niondoke nyumbani kwa Baba mkubwa

Mkuu ukikaa Kwa watu , Kwa bro , au Kwa sista ,au Kwa ndug yyte hata rafk tuu, jitahd uwe mpole kabisa , yaan wew uwe Mzee wa Yes , jali mambo yako tuu....!!

Yaan hata kuleta marafk hapo home acha, kutongoza mfanyakaz usijarbu kabisa , na usiwe na mazoea saaana nao ..... Na uwe na furaha always , usinung'unike chakula sjui nn , wakikupa kazi fanya Kwa furaha...issue zako zikikaa Sawa unaamsha sasa
 
Mwaka fulani, nilipoteza kazi nikiwa sina chochote! Nyumbani kwetu kuna nyumba kubwa sana, na kwavile watoto wote ni wakubwa (the youngest is now 26), karibu, except huyu dogo, wana "kwako"! Hata huyu dogo bado yupo home kwavile, as a big brother, nilimwambia asitoke lakini uwezo wa kupanga anao! Ninachotaka kusema ni kwamba, ingawaje nyumba ni kubwa sana lakini ilikuwa inaishi baba, mama, mfanyakazi wa ndani, na huyu dogo huku chumba kimoja na sebule (uani) kukiwa hakuna mtu, na chumba kimoja wakaamua kuweka kuku kwavile na chenyewe kilikuwa hakina kitu! Aidha, kulikuwa na banda lingine kubwa la uani (upande mwingine wa nyumba) ambako walikuwa wanaishi wapangaji ambao ni MMOJA TU ndie alikuwa analipa kodi kwa wakati! Wengine wote walikuwa na sifa ya kutimuliwa!!!

Unaona jinsi ambavyo nilikuwa na "utajiri" wa makazi?! Lakini pamoja na yote hayo, nikagoma katakata kurudi home kwenye nyumba ya bure! Nilichofanya ni kuuza pikipiki yangu na kwenda kupanda sehemu iliyokuwa nafuu zaidi! Usidhani ilikuwa rahisi! Niliishi kwa shida SANA! Mlo mmoja ilikuwa kawaida! Nikipika chai, majani nilikuwa simwagi! Amini usiamini, sufuria ya chai ilibadilika rangi kutokana na kutoisafisha kwa hofu ya kumwaga majani! Mboga yangu ilikuwa maharage, na wala sikuwa na uhakika wa kuyapata! Niliachana na jiko la gesi na kuanza kutumia mafuta ya taa sababu ilikuwa ni rahisi kupata buku 2 ya mafuta ya taa kuliko 15K hadi 18K ya gesi! Si mara moja wala mara mbili kukaa na njaa lakini nikakomaa ingawaje wazazi wapo hai Dar, Sister wangu (hana mume) yupo hai Dar na ana nyumba yake, uncle wangu, yupo hai Dar na ana nyumba yake, Bro wangu akanipatia banda la uani pale kwake Charambe! Lakini kote huko NILIGOMA kwenda!

Leo sina cha kujivunia lakini naweza kulipa kodi ya mwaka mzima! Najua unajua huwezi kulipa kodi mwaka mzima wakati hauna uhakika wa kula!!!

Ninachotaka kusema ni kwamba, ONDOKA hapo unapotimuliwa! kapambane mtaani uingie akili! Huwezi kuwa kula kulala bure halafu ukapata akili ya ku-fight!!
Huu ni mfano bora wa mtafutaji, lakini yaweza kuwa ni kitisho kwake.
 
Tatizo lako ulikaa kwa Baba mkubwa kisha ukabweteka,ulikaa miezi 4 bila kutafuta solution ya tatizo lako?

Halafu inaonekana Baba yako mkubwa haoni ukifanya juhudi zozote za wewe kuja kujitegemea na kuondoka,huenda anakuona una shinda ndani tu,

Najua ni ngumu ila Baba yako mkubwa anataka ushughulishe kichwa,sidhani kama anakufukuza coz hakupendi au kuna kosa umefanya,anataka ukomae,anataka ushughulishe kichwa,

Nakuombea kwa Mungu akuonyeshe njia ila usije kumsahau huyo Baba yako mkubwa,naamini kabisa hana nia mbaya na wewe,utakuja kugundua hilo siku za mbeleni,

Good Luck.
 
Wana JF wenzangu, nilikuwa nimepanga maeneo ya Kimara miaka kadhaa iliyopita. Kutokana na changamoto ya maisha, kazi nilikuwa sina nikaenda kuishi kwa bamkubwa ili nijipange upya.

Kwa sasa nimekaa miezi minne kwake leo asubuhi kaniambia “nimekupa siku 30 uondoke kwangu”.

Wakuu naombeni msaada wapi pakuanzia? Nifanye nini? Nianzie wapi?

Hakuna ushauri hapo, hama chap chap kama ulivyoagizwa! Yule ana familia yake, sasa wewe kuhifadhiwa pale umegeuza kuwa ni nyumbani kwenu!

Ni afadhali ukabane kwenu ulikozaliwa hata kama ni kijijini kuliko kukaa kwa mtu na huna unachochangia hapo zaidi ya kula na kujizurulia tu maana inaonesha huna kazi yoyote ya kufanya!

Mimi swali langu la pili ni kuwa: hivi kwa nini vijana wengi mnapenda kujazana Dar na kuanza kulalamika kuwa maisha magumu? Halafu shida zenu mnazirusha humu ili sisi tuwacheke au tuwafanyie nini maana mnajianika uninga wenu na hakuna anayeweza kutatua shida zako zaidi yako mwenyewe!

Nendeni mikoani nje ya Dar mkatafute kazi hata ya kusukuma mkokoteni, pesa ni pesa haina harufu ya kazi uliyokuwa unafanya hadi kuipata! Sasa wewe mlalamikaji au mleta uzi huu, mimi nakushauri ONDOKA HARAKA SANA HAPO HATA KABLA YA SIKU 30 KUFIKA!
 
Wana JF wenzangu, nilikuwa nimepanga maeneo ya Kimara miaka kadhaa iliyopita. Kutokana na changamoto ya maisha, kazi nilikuwa sina nikaenda kuishi kwa bamkubwa ili nijipange upya.

Kwa sasa nimekaa miezi minne kwake leo asubuhi kaniambia “nimekupa siku 30 uondoke kwangu”.

Wakuu naombeni msaada wapi pakuanzia? Nifanye nini? Nianzie wapi?
Jiandae kuondoka tu kakupa muda wa kutosha tuu
 
Unataka msaada gani sasa ndugu yetu, si uhame kama ulivyoelekezwa.

Father ako amegundua wewe kichwa hakinacharge so anakuboost kiaina maana kama ungekua umekosea sehemu angekupa masaa nane tu uwe umeshaondoka

Lakini kakupa mwezi mzima jua ana nia njema sana na wewe utakuja kumshukuru.

Kuna mchungaji mmoja alikua anafundisha kua "kuna upendo wa wakupendao usio na faida kwako ila kuna chuki ya wakuchukiao yenye faida kwako" nafikiri ni somebody Kimaro.
 
Mkuu ukikaa Kwa watu , Kwa bro , au Kwa sista ,au Kwa ndug yyte hata rafk tuu, jitahd uwe mpole kabisa , yaan wew uwe Mzee wa Yes , jali mambo yako tuu....!!

Yaan hata kuleta marafk hapo home acha, kutongoza mfanyakaz usijarbu kabisa , na usiwe na mazoea saaana nao ..... Na uwe na furaha always , usinung'unike chakula sjui nn , wakikupa kazi fanya Kwa furaha...issue zako zikikaa Sawa unaamsha sasa
Niliwahi kuishi kwa dadangu damu 1 alikua ameolewa...hahaa...jaman maisha haya ..walikua wakipika wenyewe wanaenda kulia chumban na mumewe...nilikua nachota maji najaza pipa 2 ..lakini hom kwetu ni kila kona wafanyakazi..nilikonda kwakweli.inahitaji wito mno!sipend hayo maisha tena
 
Kuishi Kwa ndugu ni kipaji , unakuwa kama kabati 😋 Leo linageuzwa hv , Kesho vile zaidi ya hapo lazima mtibuane...Mimi hata mtu akiniambia nikamtembelee alaf yupo Kwa ndug , siendi mana wote tunakuwa under guidance...may be tukutane hotelin au kwake
 
Wana JF wenzangu, nilikuwa nimepanga maeneo ya Kimara miaka kadhaa iliyopita. Kutokana na changamoto ya maisha, kazi nilikuwa sina nikaenda kuishi kwa bamkubwa ili nijipange upya.

Kwa sasa nimekaa miezi minne kwake leo asubuhi kaniambia “nimekupa siku 30 uondoke kwangu”.

Wakuu naombeni msaada wapi pakuanzia? Nifanye nini? Nianzie wapi?
Unakaaje kwa bamkwe km co kujiaibsha,,
Kuwa maskin jeur kapambane kwenye nyumba za watu bak huko
 
Back
Top Bottom