Msaada: Nimepewa siku 30 niondoke nyumbani kwa Baba mkubwa

Huwezi nielewa..siwakimbii.ila kuishi nao na mm nna maisha yangu mnajikuta kuna mikwaruzano
NAKUELEWA KUWA SIKU HIZI UNAONA TAABU KUWEZA KUISHI NA WAZAZI WAKO KWA VILE NI WAZEE; LAKINI KAMA WEWE ULIVYOWAHITAJI ULIPOKUWA MTOTO NAO WANAHITAJI MSAADA WAKO WAKATI HUU NI WAZEE!! JITAHIDI KUISHI NA WAZEE WAKO UTAPATA BARAKA NA EPUSHA MIKWARUZANO.
 
Mwaka fulani, nilipoteza kazi nikiwa sina chochote! Nyumbani kwetu kuna nyumba kubwa sana, na kwavile watoto wote ni wakubwa karibu, except huyu dogo, wana "kwao"! Hata huyu dogo bado yupo home kwavile, as a big brother, nilimwambia asitoke lakini uwezo wa kupanga anao! Ninachotaka kusema ni kwamba, ingawaje nyumba ni kubwa sana lakini ilikuwa inaishi baba, mama, mfanyakazi wa ndani, na huyu dogo huku chumba kimoja na sebule (uani) kukiwa hakuna mtu, na chumba kimoja wakaamua kuweka kuku kwavile na chenyewe kilikuwa hakina kitu! Aidha, kulikuwa na banda lingine kubwa la uani (upande mwingine wa nyumba) ambako walikuwa wanaishi wapangaji ambao ni MMOJA TU ndie alikuwa analipa kodi kwa wakati! Wengine wote walikuwa na sifa ya kutimuliwa!!!

Unaona jinsi ambavyo nilikuwa na "utajiri" wa makazi?! Lakini pamoja na yote hayo, nikagoma katakata kurudi home kwenye nyumba ya bure! Nilichofanya ni kuuza pikipiki yangu na kwenda kupanda sehemu iliyokuwa nafuu zaidi! Usidhani ilikuwa rahisi! Niliishi kwa shida SANA! Mlo mmoja ilikuwa kawaida! Nikipika chai, majani nilikuwa simwagi! Amini usiamini, sufuria ya chai ilibadilika rangi kutokana na kutoisafisha kwa hofu ya kumwaga majani! Mboga yangu ilikuwa maharage, na wala sikuwa na uhakika wa kuyapata! Niliachana na jiko la gesi na kuanza kutumia mafuta ya taa sababu ilikuwa ni rahisi kupata buku 2 ya mafuta ya taa kuliko 15K hadi 18K ya gesi! Si mara moja wala mara mbili kukaa na njaa lakini nikakomaa ingawaje wazazi wapo hai Dar, Sister wangu (hana mume) yupo hai Dar na ana nyumba yake, uncle wangu, yupo hai Dar na ana nyumba yake, Bro wangu akanipatia banda la uani pale kwake Charambe! Lakini kote huko NILIGOMA kwenda!

Leo sina cha kujivunia lakini naweza kulipa kodi ya mwaka mzima! Najua unajua huwezi kulipa kodi mwaka mzima wakati hauna uhakika wa kula!!!

Ninachotaka kusema ni kwamba, ONDOKA hapo unapotimuliwa! kapambane mtaani uingie akili! Huwezi kuwa kula kulala bure halafu ukapata akili ya ku-fight!!
Hii living proof Yako nimeipenda....

Ishu kubwa hapa ni jamaa kupewa connection.... Either Kazi au whetever.....

Kuna state mtu anafikia maishani bila kua agressive mwenyew au kupata mtu wa kuku shika mkono unakua loser...

NB: ANGALIZO KUNA WATU NI MAGUNIA YA MISUMARI HAWABEBEKI
 
Back
Top Bottom