Msaada: Nimepewa siku 30 niondoke nyumbani kwa Baba mkubwa

Niliwahi kuishi kwa dadangu damu 1 alikua ameolewa...hahaa...jaman maisha haya ..walikua wakipika wenyewe wanaenda kulia chumban na mumewe...nilikua nachota maji najaza pipa 2 ..lakini hom kwetu ni kila kona wafanyakazi..nilikonda kwakweli.inahitaji wito mno!sipend hayo maisha tena
Huyo Dada yako alikua anajidharaulisha kwa mumewe bila kujijua,kitendo cha yeye kukwepa kukupa chakula wewe ndugu yake wa damu ni roho mbaya sana ambayo itafanya hata huyo mumewe asimuamini tena.
 
Nafikiri ni vizuri ukienda kuishi kwa watu ili kujipanga utoe na deadline we mwenyewe, like "bamkubwa naomba kukaa kwa miezi miwili, tarehe fulani nahisi ntakuwa nimejipanga nitaondoka" hii inakupa hata wew nguvu ya kufight, sasa wewe unakaa tu kizembezembe. Kitimoto huwalishi walq kufagia banda lao, nani anataka hivyo.l!!?
 
Huyo Dada yako alikua anajidharaulisha kwa mumewe bila kujijua,kitendo cha yeye kukwepa kukupa chakula wewe ndugu yake wa damu ni roho mbaya sana ambayo itafanya hata huyo mumewe asimuamini tena.
Walininyanyasa kinoma...alikua ana mimba ikawa inamsumbua ..so hom wakaniambia nitoke chuo niwe narudi kwake daily hana bek3 unaamka saa10 unachota maji had 12 unapga deki unapika chai unasepa chuo..yaan walinifanya kama yatima mbweha wale
 
Mwaka fulani, nilipoteza kazi nikiwa sina chochote! Nyumbani kwetu kuna nyumba kubwa sana, na kwavile watoto wote ni wakubwa (the youngest is now 26), karibu, except huyu dogo, wana "kwako"! Hata huyu dogo bado yupo home kwavile, as a big brother, nilimwambia asitoke lakini uwezo wa kupanga anao! Ninachotaka kusema ni kwamba, ingawaje nyumba ni kubwa sana lakini ilikuwa inaishi baba, mama, mfanyakazi wa ndani, na huyu dogo huku chumba kimoja na sebule (uani) kukiwa hakuna mtu, na chumba kimoja wakaamua kuweka kuku kwavile na chenyewe kilikuwa hakina kitu! Aidha, kulikuwa na banda lingine kubwa la uani (upande mwingine wa nyumba) ambako walikuwa wanaishi wapangaji ambao ni MMOJA TU ndie alikuwa analipa kodi kwa wakati! Wengine wote walikuwa na sifa ya kutimuliwa!!!

Unaona jinsi ambavyo nilikuwa na "utajiri" wa makazi?! Lakini pamoja na yote hayo, nikagoma katakata kurudi home kwenye nyumba ya bure! Nilichofanya ni kuuza pikipiki yangu na kwenda kupanda sehemu iliyokuwa nafuu zaidi! Usidhani ilikuwa rahisi! Niliishi kwa shida SANA! Mlo mmoja ilikuwa kawaida! Nikipika chai, majani nilikuwa simwagi! Amini usiamini, sufuria ya chai ilibadilika rangi kutokana na kutoisafisha kwa hofu ya kumwaga majani! Mboga yangu ilikuwa maharage, na wala sikuwa na uhakika wa kuyapata! Niliachana na jiko la gesi na kuanza kutumia mafuta ya taa sababu ilikuwa ni rahisi kupata buku 2 ya mafuta ya taa kuliko 15K hadi 18K ya gesi! Si mara moja wala mara mbili kukaa na njaa lakini nikakomaa ingawaje wazazi wapo hai Dar, Sister wangu (hana mume) yupo hai Dar na ana nyumba yake, uncle wangu, yupo hai Dar na ana nyumba yake, Bro wangu akanipatia banda la uani pale kwake Charambe! Lakini kote huko NILIGOMA kwenda!

Leo sina cha kujivunia lakini naweza kulipa kodi ya mwaka mzima! Najua unajua huwezi kulipa kodi mwaka mzima wakati hauna uhakika wa kula!!!

Ninachotaka kusema ni kwamba, ONDOKA hapo unapotimuliwa! kapambane mtaani uingie akili! Huwezi kuwa kula kulala bure halafu ukapata akili ya ku-fight!!
Umempa ushuri wa kiungwana sana(ushauri wa kiume) kama asipokuelewa basi nina uhakika hata huyo Baba yake mkubwa hajamkosea ila kwa sababu aliomba hifadhi ya muda ila kadri muda unavyokwenda Baba mkubwa haoni mabadiliko yoyote ndio maana amempa huo muda ili ajiongeze
 
Wana JF wenzangu, nilikuwa nimepanga maeneo ya Kimara miaka kadhaa iliyopita. Kutokana na changamoto ya maisha, kazi nilikuwa sina nikaenda kuishi kwa bamkubwa ili nijipange upya.

Kwa sasa nimekaa miezi minne kwake leo asubuhi kaniambia “nimekupa siku 30 uondoke kwangu”.

Wakuu naombeni msaada wapi pakuanzia? Nifanye nini? Nianzie wapi?
Tumesikia upande mmoja upande wa pili hatujasikia!

Jamiiforums kuna watu wema sana!

Ndo ukubwa huo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wana JF wenzangu, nilikuwa nimepanga maeneo ya Kimara miaka kadhaa iliyopita. Kutokana na changamoto ya maisha, kazi nilikuwa sina nikaenda kuishi kwa bamkubwa ili nijipange upya.

Kwa sasa nimekaa miezi minne kwake leo asubuhi kaniambia “nimekupa siku 30 uondoke kwangu”.

Wakuu naombeni msaada wapi pakuanzia? Nifanye nini? Nianzie wapi?
kwa kuangalia ID yako yaonesha tosha age yako si chini ya 30 years. Mana uko humu tangu 2011. Kama unachokianadika hapa ni cha kweli basi umekosea kukaa kwa mtu(mzazi,rafiki au ndugu) kwa miaka hiyo yote. Labda inaeza kusababishwa na uwoga wa kujaribu na kupenda konewa huruma.
Bado hujachelewa unaeza anza sas, muhimu usiruhusu panic. Tafuta kazi yoyote halali kupitia marafikia hata kama ni ya kwa siku, kusanya ya kupata hata chumba kwa miezi mitatu na chukua bei rahisi. Usilazimishe uwe na kitanda mara sofa mara sabufa. Anza kutokana na uwezo wako. hapo sasa utaanza jifunza kuyajua maisha yanahitaji utunzaji wa hela na kuitafuta. Utapanda hadi ufikie unapo ona unastahili kufika japo si karibuni. Usilazimishe kuingia kwenye kukopa marafiki upate chumba au malazi, maana itakuweka kwenye stress zaidi ya kuyawaza maisha utabaki yawaza madeni.
 
Walininyanyasa kinoma...alikua ana mimba ikawa inamsumbua ..so hom wakaniambia nitoke chuo niwe narudi kwake daily hana bek3 unaamka saa10 unachota maji had 12 unapga deki unapika chai unasepa chuo..yaan walinifanya kama yatima mbweha wale
What not kill you makes you stronger,
hope ulipata experience fulani.
 
Pole sana hizo ndio changamoto za kuwa wa kiume, tafuta vibarua ukapange uswazi kama Tandale, Kigogo au nje ya mji kama Mbagala huko
 
Back
Top Bottom