Sintofahamu yako inakumbusha moja ya mikasa niliyowahi kukutana nayo na sijapata kuisahau maana kuna kitu kinanizuia kusahau
Ipo hivi.. mwaka fulani nilienda babati sehemu iitwayo Galapo katika halakati za ujana na kutafuta maisha nikapata marafiki wawili ambao tulishibana sana, rafiki yangu wa Gidamasi(jina bandia) alikuwa na mwanamke mmoja wa mchanganyiko wa m'mbulu na mang'ati aisee yule dada alikuwa mzuri sana kias kwamba kwa tamaa za ujana nikajikuta nimempora Gidamas yule msichana, ajabu ni kwamba Gidamas hakunichukia zaidi alinambia kumchukulia mwanamke isiwe mwisho wa ukaribu wetu, ndanj ya huohuo mwezi nikapatwa na hali mbaya sana ya kifedha kutokana na kufanya speculation mbovu ya juu ya ishu fulani so nikafanya investment ambayo ilikuja kunimaliza kabisa, yule mwanamke hakuwa mtu wa maisha ya shida so na mimi nikanyang'anywa na jamaa yetu alieitwa Gitemaa(jina bandia), hili tukio lilitokea ndani ya mwezi wa saba(binti alikuwa mtu wa tamaa na wote tulilijua hili), niliponyang'anywa yule bint haikunishtua maana kwa bankruptcy niliyokuwa nayo nilishajua kuwa ataondoka tuu, sasa mwezi wa tatu wa mwaka uliofaata akanipigia simu kuwa amejifungua na mtoto ni wangu, hapo ndipo maswali yasiyo na majibu yakaanza... ila mwsho wa picha nilipoenda mtoto nilikuwa ni copy yangu