Msaada namna ya kuhuisha (re-new) leseni ya udereva

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,696
22,729
Habari wanabodi.

Kwa wale madereva wenzangu wa magari naomba muongozo wenu namna ya kupata leseni mpya au ku-renew baada ya niliyonayo kupita muda wake wa matumizi.

Hii niliyonayo ilitolewa tarehe 15/10/2012 na itaisha muda wake wa matumizi tarehe 14/10/2015.

Kwa hiyo anayefahamu utaratibu wa kupata leseni mpya naomba anijuze.

Natanguliza shukrani.
 
Nenda TRA pia kumbuka Tin Number yako, na shs 40,000/= wataingiz hiyo Ti Number yako kisha watakuelekeza kwenda Trafic kwenye ofisi zao. Trafic watairuhuu kama haina shida.

Then utakwenda tena TRA na kuprint karatasi ya kulipia bank hizo fedha. Kumbuka kuwa kwa sasa haina haja ya kujaza zile karatasi kamazamani, ila kwa sasa Daraja E wanainyofoa kama huna cheti cha NIT,auVETA. japo kwa ufupi ni hayo na sijajua uko wapi kwa sasa.
 
Nenda TRA(Kama upo Dar nenda Myfair au Samora-karibu na Clock Tower) ukiwa na lesen yako (hakuna chochote utakachoulizwa zaidi ya leseni yako) wataingiza kwenye system watafanya michakato yao(haichukui zaidi ya dk 5} then watakuprintia karatasi za kwenda kulipia bank 40,000/= tu, baada ya siku moja utarudi ya hiyo karatasi uliyolipia na utapewa leseni yako (hii ni kwa Dar nakueleza nilivyofanya mimi, sijui kama hizi taratibu ni uniform hadi mikoani au laa...maaake huko mikoani sometimes utafikiri upo serikali nyingine)

Kama leseni yako ni ya magumashi usiende, maana palepale polisi wapo
 
mimi bado ninayo ya kitabu class E kipindi wanabadilisha mfumo nilikuwa nje ya nchi,je naweza saidiwa pia kupata ii mpya
 
Hii sio kwa mara ya kwanza kweli????

Kurenew kwa mimi nilienda na leseni yangu tu...wakaniprintia kiasi cha kulipia baada ya malipo nikapewa tarehe ya kuchukua

Nenda TRA pia kumbuka Tin Number yako, na shs 40,000/= wataingiz hiyo Ti Number yako kisha watakuelekeza kwenda Trafic kwenye ofisi zao. Trafic watairuhuu kama haina shida. Then utakwenda tena TRA na kuprint karatasi ya kulipia bank hizo fedha. Kumbuka kuwa kwa sasa haina haja ya kujaza zile karatasi kamazamani, ila kwa sasa Daraja E wanainyofoa kama huna cheti cha NIT,auVETA. japo kwa ufupi ni hayo na sijajua uko wapi kwa sasa.
 
hiyo 40,000 ni hela ya serikali ila kuna watu wanajiita madalali kunajamaa juzi amepigwa hadi laki mbili na kumi,ili kuepuka usumbufu sijui uende kwa trafic we nenda na laki moja vinginevyo utasumbuliwa tu na huo usumbufu hauna maana nyingine zaidi ya rushwa tu.
 
daraja B,D mkuu!

Mkuu nenda moja kwa moja ofisi za TRA kitengo kinachoshughulika na utoaji Leseni za kuendesha vyombo vya moto na 1.Leseni halisi iliyokwisha muda wake. 2.Cheti chako cha kuhitimu mafunzo ya kuendesha gari (Cheti halisi) 3.Namba yako ya mlipa kodi,kama huna nenda ofisi ya TRA inatolewa bure. 4.Shilling 40,000/= za malipo ambazo utapewa maelekezo na afisa wa TRA utalipia wapi.

Hapo hakuna Rushwa wala dalali nenda mwenyewe usimtume mtu wala asikuguse dalali wa aina yoyote, onana na afisa wa serikali.
 
mimi bado ninayo ya kitabu class E kipindi wanabadilisha mfumo nilikuwa nje ya nchi,je naweza saidiwa pia kupata ii mpya

kwa mfumo wa sasa nakushauri nenda ofisi za trafiki polisi ukapewe utaratibu wa jinsi ya kupata Leseni mpya
 
Mkuu nenda moja kwa moja ofisi za TRA kitengo kinachoshughulika na utoaji Leseni za kuendesha vyombo vya moto na 1.Leseni halisi iliyokwisha muda wake. 2.Cheti chako cha kuhitimu mafunzo ya kuendesha gari (Cheti halisi) 3.Namba yako ya mlipa kodi,kama huna nenda ofisi ya TRA inatolewa bure. 4.Shilling 40,000/= za malipo ambazo utapewa maelekezo na afisa wa TRA utalipia wapi.

Hapo hakuna Rushwa wala dalali nenda mwenyewe usimtume mtu wala asikuguse dalali wa aina yoyote, onana na afisa wa serikali.

Maelezo ya mdau yanajitosheleza kabisa, hizo ndio hatua za kufuata ili uweze kupata leseni mpya.

Pia usisahau kwenda na leseni ya zamani siku utakapoahidiwa kwenda kuchukua hiyo mpya, kuna mzee mmoja mwembamba ana elements za kikoloni mbaya, usipokuja nayo hata kama umeisahau mkoani, hautakabidhiwa leseni yako mpya, unless uwe na police loss report ikiwa umepoteza ya zamani.
 
Back
Top Bottom