Sajenti
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 3,651
- 414
Nina mtoto wa kike wa miaka 9 na sasa anasoma darasa la 4. Kwa ujumla katika masomo yake amekuwa akijitahidi sana hata mimi anani-impress. Tangu yuko darasa la 1 habanduki katika wale wanafunzi watano wa kwanza.
Tatizo lillilojitokeza ni tangu mwaka huu uanze. Kwa mapenzi tu kama mzazi niliamua kuwafungia Dstv pale nyumbani angalau nao wapate kuburudika. Lakini sasa naelekea kujilaumu kwani binti amekuwa anatumia muda wake mwingi kuangalia TV na hasa ile channel ya Catoon (Catoon Network).
Nilipoona anakuwa busy sana na Tv nilimueleza kwa upole tu apunguze hiyo kitu na akakubali, lakini hata binti wa kazi amenieleza kuwa anaporudi shule tu yeye yuko kwenye Tv.
Nikaamua kuwa naficha remote ninapotoka nyumbani huenda itamfanya apunguze hiyo kitu. Kiasi nafikiria hata kuachana na matumizi ya Tv kabisa maana hapo nyuma nilikuwa namnunulia DVD za catoon kama Tom & Jerry na nyingine sasa amekuwa mpaka anaenda kuazima kwa rafiki zake.
Nakosa amani kabisa.