Msaada: Nahisi mtoto wangu ameathirika na Runinga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada: Nahisi mtoto wangu ameathirika na Runinga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sajenti, May 3, 2010.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nina mtoto wa kike wa miaka 9 na sasa anasoma darasa la 4. Kwa ujumla katika masomo yake amekuwa akijitahidi sana hata mimi anani-impress. Tangu yuko darasa la 1 habanduki katika wale wanafunzi watano wa kwanza.

  Tatizo lillilojitokeza ni tangu mwaka huu uanze. Kwa mapenzi tu kama mzazi niliamua kuwafungia Dstv pale nyumbani angalau nao wapate kuburudika. Lakini sasa naelekea kujilaumu kwani binti amekuwa anatumia muda wake mwingi kuangalia TV na hasa ile channel ya Catoon (Catoon Network).

  Nilipoona anakuwa busy sana na Tv nilimueleza kwa upole tu apunguze hiyo kitu na akakubali, lakini hata binti wa kazi amenieleza kuwa anaporudi shule tu yeye yuko kwenye Tv.

  Nikaamua kuwa naficha remote ninapotoka nyumbani huenda itamfanya apunguze hiyo kitu. Kiasi nafikiria hata kuachana na matumizi ya Tv kabisa maana hapo nyuma nilikuwa namnunulia DVD za catoon kama Tom & Jerry na nyingine sasa amekuwa mpaka anaenda kuazima kwa rafiki zake.

  Nakosa amani kabisa.
   
 2. K

  Kwayu JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2010
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  The other side of utandawazi.hata ufiche remote watenda kucheki kwa jirani.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Huyuo ni wa kuongea nae kwenye round-table tu mkuu, na kushauriana nae.
  Huwezi kumdhibiti kwasasa, maana hiyo hobby iko damuni...
   
 4. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Sajenti

  ni ajabu kuwa mtoto mdogo ndo anayekuongoza hapo home. mimi watoto wangu nawapenda sana, nikirudi home wananirukia, lakini nikisema kitu fulani sitaki, hakuna anayefanya. kwasababu huwa nawarudi pia kama wakikosea.Wewe huho mtoto wako wa miaka tisa inaelekea ni yai, unaogopa kulidondosha, sasa unatengeneza bom.

  Unatakiwa kumakamata, mtandike fimbo za kutosha, mwambie hakuna kuangalia luninga kwa mida uliyokataza. akirudia tena, njoo niambie. msiwalee watoto wenu kama watoto wa ulaya ambao wanawajibu hata wazazi wao, ambao mzazi umelala kitandani unashitukia mtoto tayari ameshaingia chumbani kwenu wewe na mkeo bila hata hodi anaomba kalamu, waleeni watoto wenu kwa adabu, ili wakija kuwa watu wazima wawashukuru, ukiwalea vibaya watakuja kukulaumu wakijakupata akili na watakutelekeza uzee wako utaula kwa shida.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  May 3, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Kwa hapo mkuu, bakora zitasaidia kimtindo!
   
 6. E

  Erica Furaha Member

  #6
  May 3, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo unatakiwa kumpangia ratiba ,kama ni jumamosi na jumapili
   
 7. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mwana wa Mungu

  Nimekupata mkuu...Si kwamba sijui kucharaza, ni mzuri sana katika kutembeza bakora isipokuwa sipendelei sana ukizingatia kwenye mambo mengi ninayomkataza anatii. Haya nitajaribu kutembeza mjeledi...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Katavi ushauri wako mbaya wewe ..viboko vitamfanya awe sugu
  swala hapo ni kuongea nae kwa upole na kumpangia ratiba ya kusoma pia ya kuangalia Tom & jerry umri huo bado ni wa kujifunza
   
 9. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #9
  May 3, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Thanks. Hata mimi napendelea sana dialogue nae.
   
 10. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  watoto wanahaki ya kupumzika, kaka mimi wala sioni sabu ya wewe kujutia uamuzi wako wa kuwafungia DStv watoto wako ilikuwa ni haki yao na umefanya hivyo kama mzazi the thing which I congratulate you. Maoni yangu ni kuwa nafikiri ushauri huu hapo juu ni mzuri mpangie ratiba tu, kuwa akitoka shule anaweza tizama Tv kwa muda fulani tu, baada ya hapo aji engage katika homework, ila nafikiri ni vizuri nawe kama huna majukumu mengi yanayokubana uwe nyumbani mapema kumsaidia kwa homework zake na kuhakikisha ratiba uliyompangai anaifuata, hapa viboko sio dawa kabisa!
   
 11. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ..Nimekugongea senksi kule FL1. Huwezi kuamini huyu binti huwa nazungumza nae kama mtu mzima mwenzangu kiasi kwamba mengi ninayomueleza hutekeleza mpaka nashangaa, I wish siku moja ungekaa uzungumze nae FL1!
   
 12. FrankOwner

  FrankOwner Member

  #12
  May 3, 2010
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ....ndugu yangu ...mrushe mtoto angaza .....wale wanatoa ushauri na 'saa' ...ukifika acha ushauri chukua saa ..chagua nzuri mpe mtoto ataipenda ata chukia tv...
   
 13. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #13
  May 3, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mbona mimi nimekushauri exactly kama FL1, (tena nilitangulia)wala hujanigongea senksi.,..Tutafika kweli wakunyumba?
   
 14. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #14
  May 3, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sajenti Hivi hapo kwako hakuna miti ukate viboko? Mboja unapoteza muda wakti vibo vipo hata maneno ya Mungu yanashauri kuwachapa. Ila usijeruhi sana!
   
 15. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #15
  May 3, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Afu sajenti mimi usinibanie thanks!
   
 16. vkeisy2006

  vkeisy2006 JF-Expert Member

  #16
  May 3, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 230
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  NIMESOMA KWA PUPA MADA NIKIJUA AMEATHIRIKA NA UKIMWI ........daaaah mbona unnawapa watu prsha aaaah..........mi dstv inaharibu hata kazi nyumbani saa nyingine hazifanyiki kutwa moviemagic......nakuonea huruma huyo mtoto na katuni hahaha
   
 17. j

  jingoist Member

  #17
  May 3, 2010
  Joined: Mar 24, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  this comedian is talking about beating kids on youtube

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. M

  Mwijungula Member

  #18
  May 3, 2010
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ohh Pole rafiki na hali hiyo. But unaweza ku mcontrol mapema, ni bado mdogo anaweza kubadilika. Samaki mkunje angali mbichi
   
 19. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #19
  May 3, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ....Sawa wa kunyumba nimegonga pale. Kotoka kuhyoma mlongo wangu chabwina lepa!!!...
   
 20. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mkuu, miti ni kwa ajili ya matunda na kivuli si kuchapia watoto!!! Taratibu mazee!
   
Loading...