Msaada: Nahisi mtoto wangu ameathirika na Runinga

Msaada: Nahisi mtoto wangu ameathirika na Runinga

Mkuu tatizo la waafrika hatujui kuishi ki manufaa na utandawazi kama nchi zilizoendelea.ndo maana watoto wetu wanashidwa kutumia vipawa/vipaji vyao ipasavyo. Cha msingi jitahid umuwekee ratiba ya mda mchache TV na mda mwingi masomo.huyo bado unaweza kumbadili kabla hajapotea kabisa.
 
watoto wanahaki ya kupumzika, kaka mimi wala sioni sabu ya wewe kujutia uamuzi wako wa kuwafungia DStv watoto wako ilikuwa ni haki yao na umefanya hivyo kama mzazi the thing which I congratulate you. Maoni yangu ni kuwa nafikiri ushauri huu hapo juu ni mzuri mpangie ratiba tu, kuwa akitoka shule anaweza tizama Tv kwa muda fulani tu, baada ya hapo aji engage katika homework, ila nafikiri ni vizuri nawe kama huna majukumu mengi yanayokubana uwe nyumbani mapema kumsaidia kwa homework zake na kuhakikisha ratiba uliyompangai anaifuata, hapa viboko sio dawa kabisa!

Mkuu Kilembwe,
umeshauri vizuri sana hata mie nina binti 8 years ratiba anafuata vizuri na tunaenjoy
 
Dialogue ni nzuri lakini ikishindikana ili kumrudisha kwe.nye mstari tumia njia mbadala.! Ujue na yeye anaweza kuwa anakupima kwamba njia zote ulizo mzoesha kutumia kumkanya zikishindwa utafanyaje.?

Hii ni dunia nyengine wanasoma mengi nje.!
Mtokee ki vyengine chapa vizuri na itasaidia hata aogope kufanya na upuuzi mwingine .!
 
Malezi ya kipumbavu hayo! wewe mtu mzima unategemea mtoto aache kutazama Tv muda wote wakati hajui madhara yake!!
Mtoto unamuelimisha taratibu na kumuonya kuhusu madhara ya kutazama television, asipokusikia ni fimbo tu.
 
Mpe ratiba
Nawe baba la baba chukua nafasi yako na mwajulishe ai mwambie kwa siku awe na ratiba ya saa moja au mawili ya kuangalia tv na isidhidi hapo
 
Mwana wa Mungu

Nimekupata mkuu...Si kwamba sijui kucharaza, ni mzuri sana katika kutembeza bakora isipokuwa sipendelei sana ukizingatia kwenye mambo mengi ninayomkataza anatii. Haya nitajaribu kutembeza mjeledi...

Kama anatii hayo mengine, kwa nini hilo moja awe mkaidi? Ni lazima mtoto amtii mzazi wake, vinginevyo hata maendeleo yake katika masomo yatakuwa bure. Si sahihi mzazi uanze kuhangaika na kuficha remote ya TV,au kung'oa kabisa TV kwa sababu mtoto under 10 years hataki kusikia unachosema.

"Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu" (Ufunuo Wa Yohana 1:19)
 
watoto wanahaki ya kupumzika, kaka mimi wala sioni sabu ya wewe kujutia uamuzi wako wa kuwafungia DStv watoto wako ilikuwa ni haki yao na umefanya hivyo kama mzazi the thing which I congratulate you. Maoni yangu ni kuwa nafikiri ushauri huu hapo juu ni mzuri mpangie ratiba tu, kuwa akitoka shule anaweza tizama Tv kwa muda fulani tu, baada ya hapo aji engage katika homework, ila nafikiri ni vizuri nawe kama huna majukumu mengi yanayokubana uwe nyumbani mapema kumsaidia kwa homework zake na kuhakikisha ratiba uliyompangai anaifuata, hapa viboko sio dawa kabisa!
 
Japo thread ya zamani but kama una mtoto ambaye amekuwa addicted na TV ni kuongea nae na kumbadilishia ratiba.. Hamna haja ya kuficha remote.. Mweleze kwamba utaangalia katuni jumamosi na jumapili tena kwa muda maalumu.. Watoto wanastahili mwongozo na anatakiwa aheshimu hilo.. Hapa tuna 2 kids wanajua kuwa they are only allowed to watch TV on weekends tena kwa muda maalumu asubuhi na jioni basi.. Na wamezoea hivyo japo wana access ya cartoon full time but wanajua no watching TV... During the week wakitoka shule ni kufanya homework na kucheza michezo mengine.. Tuliwaeleza kuwa watching TV all the time itawafanys kuwa wajinga walielwa tangu wakiwa hawajafikisha hata 5 years.. As a parent you have a control over your child.... Use that control to make him or her a better and responsible person in the future.... Ongea nae aelewe DO and DON'T....
 
Kama anatii hayo mengine, kwa nini hilo moja awe mkaidi? Ni lazima mtoto amtii mzazi wake, vinginevyo hata maendeleo yake katika masomo yatakuwa bure. Si sahihi mzazi uanze kuhangaika na kuficha remote ya TV,au kung'oa kabisa TV kwa sababu mtoto under 10 years hataki kusikia unachosema.

"Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu" (Ufunuo Wa Yohana 1:19)

So true... Mtoto mdogo kias hiki anatakiwa aheshimu unapomwambia kitu... Hakuna sababu ya kuficha remote wala nn... Eka hapo mwambie no watching TV mpaka weekend... Tunatakiwa tupumguze muda watoto watu wanaotazama TV... Know when and what your child is watching.. Have a time schedule..
 
Malezi ya kipumbavu hayo! wewe mtu mzima unategemea mtoto aache kutazama Tv muda wote wakati hajui madhara yake!!
Mtoto unamuelimisha taratibu na kumuonya kuhusu madhara ya kutazama television, asipokusikia ni fimbo tu.

Mkuu punguza presha maana mtt kwa sasa ana karibu miaka 19, so huyuko tena darasa la 4
 
Nina mtoto wa kike wa miaka 9 na sasa anasoma darasa la 4. Kwa ujumla katika masomo yake amekuwa akijitahidi sana hata mimi anani-impress. Tangu yuko darasa la 1 habanduki katika wale wanafunzi watano wa kwanza.

Tatizo lillilojitokeza ni tangu mwaka huu uanze. Kwa mapenzi tu kama mzazi niliamua kuwafungia Dstv pale nyumbani angalau nao wapate kuburudika. Lakini sasa naelekea kujilaumu kwani binti amekuwa anatumia muda wake mwingi kuangalia TV na hasa ile channel ya Catoon (Catoon Network).

Nilipoona anakuwa busy sana na Tv nilimueleza kwa upole tu apunguze hiyo kitu na akakubali, lakini hata binti wa kazi amenieleza kuwa anaporudi shule tu yeye yuko kwenye Tv.

Nikaamua kuwa naficha remote ninapotoka nyumbani huenda itamfanya apunguze hiyo kitu. Kiasi nafikiria hata kuachana na matumizi ya Tv kabisa maana hapo nyuma nilikuwa namnunulia DVD za catoon kama Tom & Jerry na nyingine sasa amekuwa mpaka anaenda kuazima kwa rafiki zake.

Nakosa amani kabisa.
ukilikoroga lazima ulinywe. Kazi kwako
 
darasa la4 ni mapema sana kujua muelekeo wa mtoto hivyo usiridhike.
mnunulie vitabu na uwe unamuachia homework mbali na anazopewa shuleni.
lock channels zote zisizomuhusu muachie katuni ili afurahie,ni haki yake.
mkataze kabisa kuazima dvd kwa watu,ni kitu kidogo lakini kina maana sana,mkataze aache.
mfunze mtoto kuridhika na vilivyopo nyumbani(mweleze ungekuwa na uwezo ungemnunulia kila kitu anachotaka) ila usimnunulie kila anachotaka.
mpangie mda wa kulala, akijisomea nusu saa au saa 1 kwa siku inatosha mda uliobaki akiwa kwenye tv sio mbaya,katuni sio tatizo.
 
Hapo unatakiwa kumpangia ratiba ,kama ni jumamosi na jumapili

Kabisa mkuu. Amuwekee ratiba nzuri tu na kuhakikisha anaifatilia pia kuwa mkali sometimes. Pia ongea na house girl ahakikishe mtt wake anafata kila alichopangiwa kwa wakati.
 
Back
Top Bottom