Msaada: Nahisi mtoto wangu ameathirika na Runinga

....ndugu yangu ...mrushe mtoto angaza .....wale wanatoa ushauri na 'saa' ...ukifika acha ushauri chukua saa ..chagua nzuri mpe mtoto ataipenda ata chukia tv...
..Mh! Hii mbona mbado kujua rafiki??
 
Duh thread name yako inashitua - "ameathirika" mwanzo unajua miwaya kumbe DSTV lol
Mwache acheki si umemuwekea wewe mwenyewe, wala si tatizo mbona wewe upo JF kila siku tangu asubuhi hadi jioni na wewe pia "umeathirika"
kama ana akili anazo tu usiwe na wasiwasi mkuu - tena TV inaongeza uwezo wake wa kufikiria tatizo ya wazazi wengi wanataka watoto wao kila muda wasome tu, imagine mtoto anarudi toka shule tu - utasikia mzazi haya kunywa soda au chakula HOME WORK.... oohh TUISION wapi na wapi parents?
 
Afadhali wa kwako ni catoon tu, lakini wa kwangu yuko form I na anafanya vizuri tangu primary, lakini kila wakati yuko na tamthilia hasa zile za capital, tufanyeje?
 
ni ajabu kuwa mtoto mdogo ndo anayekuongoza hapo home. mimi watoto wangu nawapenda sana, nikirudi home wananirukia, lakini nikisema kitu fulani sitaki, hakuna anayefanya. kwasababu huwa nawarudi pia kama wakikosea. wewe huho mtoto wako wa miaka tisa inaelekea ni yai, unaogopa kulidondosha, sasa unatengeneza bom. unatakiwa kumakamata, mtandike fimbo za kutosha, mwambie hakuna kuangalia luninga kwa mida uliyokataza. akirudia tena, njoo niambie. msiwalee watoto wenu kama watoto wa ulaya ambao wanawajibu hata wazazi wao, ambao mzazi umelala kitandani unashitukia mtoto tayari ameshaingia chumbani kwenu wewe na mkeo bila hata hodi anaomba kalamu, waleeni watoto wenu kwa adabu, ili wakija kuwa watu wazima wawashukuru, ukiwalea vibaya watakuja kukulaumu wakijakupata akili na watakutelekeza uzee wako utaula kwa shida.

si suruhisho nafikiria hapo utakuwa unajenga ukuta na siajabu wakakupa na jina ukifika tu hm wanatawanyika sebureni wanasema "mzee wa busara kafika" tek tek tek
 
Afadhali wa kwako ni catoon tu, lakini wa kwangu yuko form I na anafanya vizuri tangu primary, lakini kila wakati yuko na tamthilia hasa zile za capital, tufanyeje?
mtoto kama kichwa ni kichwa tu hata kama hatakwenda shule wiki akifika anafumua paper - hongera kaitaba we mwache acheki tu ndo utandawazi huu tutaficha ficha hadi lini wakati watoto wanaazimana mi DVD mashuleni - ukimzuia TV anaweka DVD kwenye computer anacheki live....picha tena kwa kificho.
 
Kuongea naye ni suala njema zaidi; na ningelishauri umuelekeza kuwa na ratiba yake kwa siku mathalani muda wa kuangalia "Tom & Jerry"; muda wa kujisomea, muda wa kumsadia dada (house girl kazi) -kumbuka anatakiwa kujifunza kazi za mikono pia; muda wa kucheza na wadogo zake au watoto wengine anaosoma nao/watoto wa majirani. Kisha utoe ushirikiano wa kumsaidia kuiishi ratiba yake. Katika maongezi, ni vema umkampa muda mwingi zaidi wa yeye kuwa mpangaji, nao ukae kiti cha nyuma cha mashua kwa ajili ya kuendesha chombo/mtumbwi.
Nikutakie kila lal kheri ktk hili
 
Afadhali wa kwako ni catoon tu, lakini wa kwangu yuko form I na anafanya vizuri tangu primary, lakini kila wakati yuko na tamthilia hasa zile za capital, tufanyeje?

...Ah! Hata humo kwenye hayo matamthilia mbona ndimo alimoanzia. Kuna siku nimekuta binti kanijia na kamzigo ka DVDs za Prison break. ananiambia daddy season zote za prison break nimepata. Umepata wapi? Nimeazima kwa rafiki yangu tunasoma nae. Nilitulia ingawa na mimi mwenyewe nilijikuta naangalia pia.
 
Umeshauri vema kama mzazi mkuu....
Ndugu, kuwa na msimamo tu na watoto wako lazima uhakikishe wanaufuata hii ni kuwatakia mema na wajue ukisema kitu unamaanisha hivyo.
Samaki mkunje angali mbichi.

ni ajabu kuwa mtoto mdogo ndo anayekuongoza hapo home. mimi watoto wangu nawapenda sana, nikirudi home wananirukia, lakini nikisema kitu fulani sitaki, hakuna anayefanya. kwasababu huwa nawarudi pia kama wakikosea. wewe huho mtoto wako wa miaka tisa inaelekea ni yai, unaogopa kulidondosha, sasa unatengeneza bom. unatakiwa kumakamata, mtandike fimbo za kutosha, mwambie hakuna kuangalia luninga kwa mida uliyokataza. akirudia tena, njoo niambie. msiwalee watoto wenu kama watoto wa ulaya ambao wanawajibu hata wazazi wao, ambao mzazi umelala kitandani unashitukia mtoto tayari ameshaingia chumbani kwenu wewe na mkeo bila hata hodi anaomba kalamu, waleeni watoto wenu kwa adabu, ili wakija kuwa watu wazima wawashukuru, ukiwalea vibaya watakuja kukulaumu wakijakupata akili na watakutelekeza uzee wako utaula kwa shida.
 
ni ajabu kuwa mtoto mdogo ndo anayekuongoza hapo home. mimi watoto wangu nawapenda sana, nikirudi home wananirukia, lakini nikisema kitu fulani sitaki, hakuna anayefanya. kwasababu huwa nawarudi pia kama wakikosea. wewe huho mtoto wako wa miaka tisa inaelekea ni yai, unaogopa kulidondosha, sasa unatengeneza bom. unatakiwa kumakamata, mtandike fimbo za kutosha, mwambie hakuna kuangalia luninga kwa mida uliyokataza. akirudia tena, njoo niambie. msiwalee watoto wenu kama watoto wa ulaya ambao wanawajibu hata wazazi wao, ambao mzazi umelala kitandani unashitukia mtoto tayari ameshaingia chumbani kwenu wewe na mkeo bila hata hodi anaomba kalamu, waleeni watoto wenu kwa adabu, ili wakija kuwa watu wazima wawashukuru, ukiwalea vibaya watakuja kukulaumu wakijakupata akili na watakutelekeza uzee wako utaula kwa shida.
Mwana wa Mungu nani kakwambia wa Ulaya hawachapi? Mie natandika kimtindo nahakikishia jamaa wa social hawasikii ila kibano huwa kinatokea tu. Tena mie tatizo ilikuwa TV na laptop sasa hv ni weekend tu. Hakuna ujinga. Chapa viwili vya fasta mnaendelea na maisha.
 
Sajenti, hili ni tatizo kwa familia nyingi japo wapo wengine hawalioni kama ni tatizo. Watoto wengi sana wapo addicted to Catoons, na ni lazima kama mzazi umpangie ratiba kama wengine walivyoshauri, ila kama addiction nyingine ni vigumu sana kwao kufuata ile ratiba hasa kama haupo. Kina dada wanakoma na watoto wetu hawa maana mwishoe mtoto anamwambia kwani TV yako? Inafika mahali wanawaacha isije kuwa taabu! Kuna rafiki yangu alificha remote watoto wakagundua njia zao nyingine na mbaya zaidi wakam-PG yeye (parental guide) sasa yeye ndie akawa hawezi kuangalia vile anataka na akifika wanajikausha kama hawajui nini kimetokea.

Usione familia nyingine DSTV ipo connected chumbani kwa wazazi tu, japo hili si suluhisho maana hata hizo film za ndugu zetu nazo zinawachukulia muda mwingi sana. Ni tatizo ambalo ni vyema kuongea na watoto na kukubaliana. Keep talking
 
Mbona mimi nimekushauri exactly kama FL1, (tena nilitangulia)wala hujanigongea senksi.,..Tutafika kweli wakunyumba?

Mzee PiJei Nimekugongea senksi... Kuwa mpole. Ila hata maneno ya Mungu yanasema, Fimbo inamnyoosha mtoto ila haiui.
 
Sajenti, hili ni tatizo kwa familia nyingi japo wapo wengine hawalioni kama ni tatizo. Watoto wengi sana wapo addicted to Catoons, na ni lazima kama mzazi umpangie ratiba kama wengine walivyoshauri, ila kama addiction nyingine ni vigumu sana kwao kufuata ile ratiba hasa kama haupo. Kina dada wanakoma na watoto wetu hawa maana mwishoe mtoto anamwambia kwani TV yako? Inafika mahali wanawaacha isije kuwa taabu! Kuna rafiki yangu alificha remote watoto wakagundua njia zao nyingine na mbaya zaidi wakam-PG yeye (parental guide) sasa yeye ndie akawa hawezi kuangalia vile anataka na akifika wanajikausha kama hawajui nini kimetokea.

Usione familia nyingine DSTV ipo connected chumbani kwa wazazi tu, japo hili si suluhisho maana hata hizo film za ndugu zetu nazo zinawachukulia muda mwingi sana. Ni tatizo ambalo ni vyema kuongea na watoto na kukubaliana. Keep talking
Hili nalo Neno Liz Senior!!
 
kupiga wala si kulea utamharibu tu mtoto wako

sema nae Sajenti, kama anarudia rudia mpe adhabu za kawaida (mnyime kitu anachopenda)
usichoke kukanya friendly na ataacha.

mdogo wangu wa kiume alipokuwa na umri wa miaka 5 alimwibia mjomba elfu tano akaenda nayo kanisani (yeye na mtoto wa mamdogo) wakajichana mavitu sunday school. jioni mjomba akacheki njenje buku 5 zimepungua, dogo akaruka kiunzi hajachukua, yule wa kike akasema 'mmh leo tumekula mavitu kibao kanisani....Tino amenunua....(ni wazi yeye ndiye alichukua)

when mom came home we told her, hakusema kitu, tukala chakula jioni then akamwita dogo, in a loving way alimwambia hw sad she was, does he want to loose his mom maana anampa pressure?

dogo alililia kwa uchungu mpaka na mimi nikamsaidia. Believe you me toka siku hiyo hata akiokota ishirini huko nje atamletea mama!!!
 
tumia remote control kufunga channel usizotaka na ziwe accessible kwa password tu. halafu hujamtendea haki mwanao kwa kusema ameathirika kwani kwa sasa katika jamii neno hilo linamaanisha ameambukizswa HIV. kafanye maombi ya kuvunja hiyo laana uliyoipandikiza juu yake vinginevyo kweli atakuja kujikwaa siku moja.
DSTV mara nyingi wanaonyesha jinsi ya kufunga channel ziusizofaa kwa mtumiaji. menu, parental control, channel option na vitu kama hivyo.
 
Watu wengine bwana naona bado ushauri wakuuliza nipate watoto wangapi jmn. Muulize maswali yenye akili. Pamoja na kuangalia tv kiwango kineshuka?? Kuangalia tv kwa muda mrefu sio nzuri. Pili we bb ukiyenunua tv huna maamuzi nuymbani kwako? Bb mfuatiliaji ana muda maalum wa kuwa home n kuhahkikisha maagizo yanayoyatoa yanatekelezwa. Fimbo isitumike pse. Ziko adhabu nyingi sio physicla. Anyimwe baadhi ya vitu, asitoke nje nk na itekelezwe. Ttz tunasema na kuacha hewani watt wanatusoma wanajya we are mit serious.
 
Nina mtoto wa kike wa miaka 9 na sasa anasoma darasa la 4. Kwa ujumla katika masomo yake amekuwa akijitahidi sana hata mimi anani-impress. Tangu yuko darasa la 1 habanduki katika wale wanafunzi watano wa kwanza. Tatizo lillilojitokeza ni tangu mwaka huu uanze. Kwa mapenzi tu kama mzazi niliamua kuwafungia Dstv pale nyumbani angalau nao wapate kuburudika. Lakini sasa naelekea kujilaumu kwani binti amekuwa anatumia muda wake mwingi kuangalia TV na hasa ile channel ya Catoon (Catoon Network). Nilipoona anakuwa busy sana na Tv nilimueleza kwa upole tu apunguze hiyo kitu na akakubali, lakini hata binti wa kazi amenieleza kuwa anaporudi shule tu yeye yuko kwenye Tv. Nikaamua kuwa naficha remote ninapotoka nyumbani huenda itamfanya apunguze hiyo kitu. Kiasi nafikiria hata kuachana na matumizi ya Tv kabisa maana hapo nyuma nilikuwa namnunulia DVD za catoon kama Tom & Jerry na nyingine sasa amekuwa mpaka anaenda kuazima kwa rafiki zake.

Nakosa amani kabisa.

Kwenye decorder kuna card. Itoe bila yeye kujua. Uweke pia bila ya yeye kujua. Pia ongea nae kwamba utamshitaki kwa mwalim wake. Wakati mwingine watoto wanaogopa walimu kuliko sisi wazazi nyumbani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom