Mwache akue, mwache aburudike na hizo katuni.. always home work ya mtoto kama huyo inatakiwa iwe kama nusu saa tu na si vinginevyo...!
nakumbuka mimi wakati niko darasa la pili, enzi hizo tv nilikuwa naisikia kwenye pipa tu, nilikuwa nasoma kwa muda wa saa moja tu chini ya uangalizi wa mama ambae alikuwa ni mwalimu, bado nikawa nafanya vizuri darasani..
sasa mtoto wa chekechea unataka umpe kazi ya masaa manne? amekuwa mwana chuo huyo kaka?
mwache mtoto afurahie maisha ya utoto... sana sana tu kama ni home work, awe awe anafanya immediately baada ya kupata chakula chake cha mchana!!! nusu saa tu inatosha usimchoshe mtoto!
Haya ni mambo ya nyakati. Kuyaondoa ni ngumu; labda kupunguza damage. Mimi wa kwangu kazi kubadilisha tu, mara cartoon kwenye tv; akichoka hapo mbio kwenye computer games. Lakini naamini watoto wanabadilika tabia; sio kama watu wazima.
Huyo anayesema wazungu hawaangalii katuni, hajui asemalo. Kama ni rate ya kuangalia tv, sisi watitu ni asilimia 10 tu; wakati wazungu ni zaidi ya 85%. Nenda ughaibuni ukashuhudie mambo.
Salama wakuu!
Mimi nina mtoto wa miaka 5 mtoto huyu anapenda sana katuni anaweza kuangalia katuni asubuhi mpaka jioni bila kuchoka
Na ikitokea ukizima Tv ni kilio mtindo mmoja mpaka uwashe
Kuhusu shule anasoma chekechea na huwa nikimpaga home work natumia nguvu za ziada sababu ya katuni
Je kuangalia katuni kwa masaa mengi kunaweza kumwadhiri?
Au katuni zinaweza kumjengea uwezo zaidi?
Naombeni kueleweshwa wanajamvi natarajia majibu mazuri kutoka kwenu
Pamoja na kwamba hujaeleza ni katuni series ipi mtoto anatezama(kuna Tom and Jerry, The Flints etc)huo umri ni umri unaoitwa kitaalamu 'formative' yaani ni umri wa kujenga mustakabali wake wa maisha ya baadaye.
Hicho kitu ambacho wewe unaita 'addiction' ni kitu kilichoko kwenye nafsi ya mtoto kilichokubaliana na kuvutiwa na katuni. Kuna uwezekano mkubwa katuni hizo zimeamsha kipaji fulani alicho nacho mtoto. Kuna uwezekano mtoto ana vipaji vifuatavyo:
1.Kuigiza na ubunifu wa mizaha ya kuchekesha
2.Uchoraji na kupamba
Vipaji hivi vitajitokeza na kudhihirika atakapofikia umri wa miaka 7+.Dalili zake ni mtoto kuwa mtundu sana kwa kufanya 'vitu visivyoeleweka'
Kwa sasa mchanganyie katuni aina tofauti zenye mafundisho.
"too much television watching got me chasing dreams"
coolio: ganster's paradise
Samahani dada FaizaFoxy mimi nina binti wa miaka 3na miezi 4..Yani yeye muda wote ni kukaa kwenye kioo,kujifunga khanga na vitenge vya mama yake cku nzima...lotion yenyewe,poda na mafuta ya nywele nk ukiacha kwenye dressing table inakua shida sana.Nimejaribu sana kumbadilisha labda kukawekea cartoons na muvies za kitoto lakini wapi,ilifika wakati nikampeleka kwa bibi yake wiki mbili labda atabadilika lakini wapi..kwa kesi hii nini solution yake??Natumai ulimaanisha kumuathiri.
Jibu ni ndio, anaweza kuathirika kisaikolojia na hata kimwili kwani anaweza kuiga mambo yanayofanywa na vikatuni akajiumiza au kuumiza wenzake.
Kila kitu kina limit zake. Anza kumbadilishia utaratibu, awe na wakati maalum wa kutazama katuni, nzuri zaidi ni zile zenye kufundisha. Awe na muda wa kusoma, hii unaanza kumzowesha kwa wewe kumsomea vitabu vyenye hadithi za kitoto zenye mafunzo, kumbuka, siyo kumhadithia, kumsomea. Awe na wakati wa kucheza, awe na wakati wa kupumzika.
Nakushauri google "child rearing" utapata kujifunza mengi, kuna kila aina ya mafunzo kuhusu kulea mtoto vyema.
Kama ana bibi, shangazi au ahli zake wako shamba (kijijini) mpeleke akakae nao kwa muda wa miezi miwili au mitatu atabadilika.
Samahani dada FaizaFoxy mimi nina binti wa miaka 3na miezi 4..Yani yeye muda wote ni kukaa kwenye kioo,kujifunga khanga na vitenge vya mama yake cku nzima...lotion yenyewe,poda na mafuta ya nywele nk ukiacha kwenye dressing table inakua shida sana.Nimejaribu sana kumbadilisha labda kukawekea cartoons na muvies za kitoto lakini wapi,ilifika wakati nikampeleka kwa bibi yake wiki mbili labda atabadilika lakini wapi..kwa kesi hii nini solution yake??
Ukweli ni kwamba katuni zinatumika sana kupumbaza watoto, pia mitandao ya kijamii inawalevya sana vijana hata sisi watu wazima! Kama aliyoyasema huyo sheikh ni uongo basi leta utafiti wako kuwa haziathiri kwa vithibitisho. Naamini zinaathari tena kubwa kwa watoto wetu kwani hatuna taratibu za kuweka ratiba juu vitu hivyo tofauti na watoto wa kizungu
ba be bi bo bu
eye ear Noise arm foot leg
wagagagigikoko
fullmassinonder FULL-MASS-IN-ORDER
miaka 5 hapewi Homework kwani anasoma kwa vitendo zaidi
mwache aangalie Katuni, kucheza na Computer au simu nk
kwani sisi hatuna uwezo wa kuwanunulia vigari, biskeli treni nk
Hao wanaesma kwamba Cartoons nchi za Wazungu hazitumiki na kwamba zimeletwa kuharibu maadili.
Huu ni uzushi ilimradi mtu ajulikane na yeye kasema tu.
Demonstrations nyingi mpaka chuo kikuu zinatumia Cartoons.
Na Japan ndio wanaongoza kwa kuwa na Cartoons nyingi na ndio Maana watoto wao tangu wadogo ni vichwa.
Na baada ya kuwa advanced ndio wakaona sasa walete remoted Cartoons ambazo ndio Video Games and Video Learning Tools.
Na Bada ya hapo sasa ndio wameingia Ulimwengu wa Affordable Robots.
Asikudanganyeni mtu Cartoons kwa mtoto ni muhim sana na zinafunza mtoto.Sasa wewe utakuta mtu anamzuia mtoto asione Cartoons au kumabda wakati ikifka muda wa maigizo ya kiswahili anamuachia aone jinsi Wanvyopigana denda.Hapo ndio watu wanaona sawa.
Hii inategema na mtoto yupoje.
Mfano kwa wangu:
Nina watoto wawili wa 9 yrs(Std 3) wakiume na 6 yrs wakike(Top class)
Hawa wanajua katuni zote mpaka wajukuu wa katuni.
Ila wao ratiba yao wanaiweza.
Wanaosoma English Medium School:
Time Table:
06h30:Kuamka kunywa chai
07h00:Kwenda Shule(Wanatembea Maana tupo Karibu na Shule)
15h00:Wanatoka shule(Wanakuwa wameishakula shule)
15h15:Wanaenda Madrasa(Chuo)
18h45:Baada ya kuwa mameswali Salat Isha,wanatoka chuo wanakuja Home
19h00 - 20h00:Home Work,kisha chakula
20h00 - 09h00:Katuni kwenda mbele mpaka usingizi unakuwakuta hapo hapo
Weekends:
08h00 - 10:00 Madrasa(Chuoni)
10h00 - 12:00 Weekend Home works
12h00 - 14:00 hatuni na kula
14h00 - 15:00 Kulala,hapa wengine wanapoteneza baadhi ya siku
15h00 - 18h45:Madrasa (Chuo)
Nimechogundua kwenye Catoons ni kwamba wame Gain alot.
Asikuadangaye mtu,mtoto ambae anatizama katuni ana uelewa mkubwa sana kuliko mtoto asietizama katuni.
1)Kwangu nime experience uwezo wao wa Lugha ya Kiingereza umekuwa kwa kazi ya ajabu sana.
Na hii ilikuwa kwamba wanafuatilia vitendo na maamrisho,na mara nyingi neno kama likiwapita basi wanauliza,na ukiwaambia hawasahau tena,maana mmoja akisahau mwingine anamkumbusha,is really good.
2)Uwezo wa kufanya maamuzi pia ni tofauti sana,mtoto mwenye kutizamana Catoons wengi wanamaamuzi ambayo ni sahihi sana,na uwezo mkubwa wa kujieleza na kukwepa maswali ya mitego na uwezo mkubwa wa kuchambua mambo.
Unaweza kukuta kwamba mtu mzima kichwa kinakuzunguka hata hujui ufanye maamuzi yapi,basi wakati huo utashangaa anakuambia Baba au Mama siufanye hivi itakuwa hivi(Jaribuni hilikufanya majaribio mtagundua)
3)Kujiamini:watoto wengi wenye kutizama catoons wanajiamini sana,hata mwalim akimuita basi jua anakwenda with confidence na yupo tayari kwa lolote.Na hata mzazi ukimuhoji basi anajiamini sana na kutoa maelezo sahihi.
Kama mtoto anapenda Catoons mwachie tu,atakapokuwa basi ratiba ya Shule ndio itakayobadilisha maisha yake.La Sivyo ukimdhibiti hapo basi atatoka nje atakutana na watoto waliopinda kama ni wakike basi wataanza kuchezeana uchi Sasa kipi bora.
Mie wangu niliwaachi,mpaka umri huo wameofikia ndio ratiba ya shule na Madrasa ika waset outomatically,na wala walikuwa hawana michezo ya ajabu nje,unajua lazima tukubali sasa hivi unavyomlea mwanao sio mwenzio anavyomlea mwanae,kuna watoto wadogo sana wanamambo ya kikubwa,na hii inaanzia katika makuzi yao na familia zao.Kwahiyo fanya kitu kitakachofanya mtoto awe busy.
Yangu ni Hayo
Swadakta Zanzibar spices kwa maelezo hayo. Watoto wanaoangalia katuni wana upeo mkubwa. Mimi watoto wangu wanaangalia zaidi channel ya Cee Beebies. Ni nzuri sana kwa elimu ya watoto.
Si bora katuni hizo kuliko kuruhusu watoto kushiriki ngoma ya vigodoro na baikoko? Watajifunza kukata viuno tu.
Bora aangalie katunii kuliko bongo movie
Samahani dada FaizaFoxy mimi nina binti wa miaka 3na miezi 4..Yani yeye muda wote ni kukaa kwenye kioo,kujifunga khanga na vitenge vya mama yake cku nzima...lotion yenyewe,poda na mafuta ya nywele nk ukiacha kwenye dressing table inakua shida sana.Nimejaribu sana kumbadilisha labda kukawekea cartoons na muvies za kitoto lakini wapi,ilifika wakati nikampeleka kwa bibi yake wiki mbili labda atabadilika lakini wapi..kwa kesi hii nini solution yake??
Thats a real lady, hayo ndiyo anayaona nyumbani. Akikuwa atabadilika, bado ni mdogo sana, so just enjoy it while it lasts.
itakuwa ngumu
Ugumu wa nini nawe, mwanamke khanga!