Msaada: Mdogo wangu ana stress za maisha

Nimepitia ushauri mbalimbali kwenye Uzi huu kupitia posts za Watu hapa.
Ila kitu nilichogundua ni kwamba Watu wengi sana wame-base kwenye tatizo LA kukosa kazi au ajira baada ya kuhitimu Chuo Kikuu. Yes, yawezekana kweli chanzo cha stress za mdogo wako ni hiki.
Lakini Mimi napenda kukusisitizia kuwa, suluhisho sahihi LA tatizo LA stress za huyo ndugu yako utalipata baada ya kujua KWA uhakika tatizo halisi linalomkabili huyo mdogo wako,

Jaribu kumdodosa KWA undani zaidi ili kujua nini hasa kinamtatiza kwenye nafsi yake???
Kaa naye chini ili uzungumze naye kirafiki kabisa, MPE Uhuru WA kutosha kabisa WA yeye kuweza kueleza bayana matatizo yake, pia umhakikishie Usalama wa kutunxiwa siri zake juu ya masuala ambayo yeye hapendi yawe publicly, ili Kumpa confidence ya yeye kuweza kuwa huru kukueleza matatizo yake.
Kama bado hayupo huru kwako ktk kueleza matatizo yake yanayomkabili, Unaweza kuwatumia marafiki zake WA karibu wenye rika moja naye ili kupata taarifa zake.Yawezekana pemgine anajisikia aibu kueleza kila kitu kwako kutokana na kupishana rika, kuhofia kuwa taarifa zake za siri pengine utazifikisha KWA wazazi wenu jambo ambalo yeye hataki liwe hivyo, etc.

Endapo kama utagundua kuwa tatizo lake ni kukosa kazi au ajira, jaribu kujadiliana naye kuhusiana na kile ambacho yeye anafikiri kuwa anaweza kufanya ili kujipatia kipato huku akiendelea kutafuta ajira au kazi ya kudumu.

Usimshurutishe kufanya kazi ambayo yeye mwenyewe binafsi hajaridhika kutoka moyoni mwake kuifanya. Jadilianeni KWA kina, KWA hekima NA ustaarabu, umsikilize yeye kuwa ana maoni gani juu ya suala hili. You've to allow 'the criticisms free environments".
Katika majadiliamo yenu, jikite zaidi ktk kufahamu matatizo yake kuhusiana na mambo haya:-
1.kukosa kazi/ajira, na mapendekezo ya kazi anazoweza kuzifanya, as interim solution measures for his problems of been unemployed.
NOTE:-
Mtaji siyo lazima uwe pesa taslimu tu, hata ushauri WA mawazo mazuri NA yaliyo sahihi, au msaada WA vitendea kazi pia ni mtaji mzuri ktk maisha.

2.Mahusiano yake, uchumba, urafiki, n.k.
3.Afya yake ya Mwili/AKILI, magonjwa, n.k.
4. Matokeo mabaya ktk Mitihani yake chuoni, etc
5.Kero au shida anazopata Kutokana NA kuishi nyumbani kwako kama mwanafamilia.
Kumbuka kuwa, Wakati mwingine wake zetu tunaowaacha majumbani nwetu huwa ni chanzo cha mateso NA manyanyaso KWA ndugu zetu WA karibu, wanashindwa kutueleza waziwazi KWA sababu wanaogopa wasije wakavunja NDOA zetu NA wenza wetu, etc.
 
kweli matokeo mabaya yanaweza kusababisha stress.

usikute ana lower second, anaona ndo hamna tena kuajiriwa mpaka Yesu arudi.
 
Dogo ana upper second na matokeo yake ya mwisho amefaulu tu vizuri
 
Duh maradhi ya wazungu yameingia Tanzania. We mpe hela huyo dogo uone kama haponi.
 
Mambo ya kijinga haya

Wenzie wana mwaka wa tano mtaani na hawana stress yy mwezi wa saba juz stress za nn
We acha tu mkuu,watu wana/tuna miaka ya kutosha mtaani na ukipata hela unaishia hela ya kula tu.

Kiukweli inabidi kuziweka pembeni hizi degree zetu kabisa.
 
Habari

Kuna mdogo wangu mhitimu wa chuo kikuu mwaka huu mwezi wa 7.

Baada ya kumaliza chuo nilimfwata nyumbani kwa mzee nikamchukua nakuishinae hapa nyumbani kwangu.

Lakini baada ya kukaanae nimegundua kuwa dogo anapresha ya maisha, yani anastress kutokana nakuwaza sana maisha.

Hali hiyo humfanya kutokuwa na furaha kabisa ilhali hakuna anachokosa hapa nyumbani maana anakula vizuri na kulala vizuri.

Sasa ndugu zangu naombeni ushauri nifanye nini hili nimsaidie dogo maana naona anakosa furaha muda mwingi asijekuathirika kisaikolojia
Ni wa kike?
 
Hao ndo watakuja kua wezi..yani ana stress za maisha kukaa miezi mitatu nyumbani..anakula bure analala bure..akiingia mtaani je itakuaje..unapata kazi ya laki mbili mshaara kwa mwezi unatakiwa ule ulipe nauli,ujihudumie na imalize mwezi ujao..wengine wamekaa miaka mitano hawana ajira yoyote..sa huyo akifikisha miaka mitatu tu utasikia kajinyonga..na mwambie asije akategemea mtaji wa kupewa kutoka mfukoni kwa mtu,kwa maana izo ni bahati za wachache..atoke atafute mwenyewe..kama ni wakike akaolewe asogeze siku..
Duuuh,wakati nipo chuo nilikua siamini kama mtu anaweza ku survive kwa mshahara wa laki mbili na bado maisha yakaenda ila mtaani ni noma sana.
 
Mpe mtaji au project kidogo kidogo aanze kujitegemea
 
Aisee mimi nilisambaza CVs kama mchele ila bado nikatoka kapa,nikajaribu kujitolea miezi miwili tu nikaacha coz huku najitolea na mama mwenye nyumba nae alikua anatishia kunitolea vyombo nje,..ni wakati ambao kila ventures zangu ndogo ndogo zilipo dorola..ni wakati ambao nilijihisi kama sina msaada wowote dunia hii...yani kuna muda hata baadhi ya maboss ninaofahamiana nao nikaona kama wana nibania tu...kila nilofanya nikaona halifai,na kila alie nitizama nilihisi ana niona vile nawaza kichwani. Kuna muda nikahisi nilipoteza muda wangu kusoma chuo,hakika nilijutia sana! Nikahisi huenda nilipoteza muda...

Siku zilisonga bila mafanikio,matarajio yalimeza hata juhudi zangu za awali za utafutaji. Stress zilizonga maisha yangu,roho ya kukatia maisha tamaa ilikua ina ninyemelea but Tumaini lilikua kubwa kushinda roho hiyo. Mbaya zaidi sikua na mzazi au mlezi wa kunipa hata faraja tu kwa wakati huo.
Na nikipindi ambacho nilitamani hata nipate mtu nimweleze yake yanayo nisibu,..daaah sikumpata mtu huyo,na sidhani kama nitakuja kumpata...daah maisha ya upweke yasikie tu kwa jirani.
Ila yote yalipita,muda ulifika kila kitu kikawa mahala pake. Kazi sikupata kwa wakati huo,ila niliamua kubadili mtazamo na kusimama imara katika vijibihashara fulani vidogo vidogo,ubize ulipozidi na ile hali ikapungua kwa kiasi fulani,ingawa sonona ni sehemu ya maisha yangu.

So,huyo kijana namshauri atafutiwe kazi ya kufanya ili awe bize,pia mjenge kisaikolojia ili aondoe matumaini makubwa alojiwekea. Kula vizuri na kulala vizuri haiwezi kuwa chachu ya furaha yake, mpe uhuru kiasi. Namaanisha acha akapange na mpe kianzio cha bihashara au mtafutie pahala pa kujishikiza.
Hongera Kwa baadaye kuwa stable, maana ukitoka chuo/nilivotoka chuo nikaanza kuchora ramani ya maisha,nikijisemea hapa nikipata kazi ntafanya hivi na hivi full kujipa hopes,sasa uhalisia ni no job aisee,unahisi kuchanganyikiwa ,stress kibao

Solution ni kama hivo kujikeep busy na vibiashara, inasaidia sanaa

Pole usiruhusu sonona kuwa sehemu ya maisha bana, itoe kabisa unakwama wapi?
 
Habari

Kuna mdogo wangu mhitimu wa chuo kikuu mwaka huu mwezi wa 7.

Baada ya kumaliza chuo nilimfwata nyumbani kwa mzee nikamchukua nakuishinae hapa nyumbani kwangu.

Lakini baada ya kukaanae nimegundua kuwa dogo anapresha ya maisha, yani anastress kutokana nakuwaza sana maisha.

Hali hiyo humfanya kutokuwa na furaha kabisa ilhali hakuna anachokosa hapa nyumbani maana anakula vizuri na kulala vizuri.

Sasa ndugu zangu naombeni ushauri nifanye nini hili nimsaidie dogo maana naona anakosa furaha muda mwingi asijekuathirika kisaikolojia
KULA au kulala vizuri si factor za kupunguza stress.
1. Mdogo wako aliweka matarajio bado hayajatimia lazima awe stressed
2. Mdogo wako anaonyesha ni mpambanaji sana anaupeo wa maisha, masomo aliyopata alifaulu akiwa na dhamira ya kufanya makubwa hapo baadaye. Sasa ndoto yake inafikia.
3. Ondoa naye kakae naye sehemu outing ukiwa umejiandaa kumpa support ya maisha, mwambie unampango wa kumpa support ila ungependa kujua nini angependa kufanya kama miradi wake binafsi. Mdogo wako atafungua kile anachokitaka utafutaji na atakuwa mchangamfu kuliko siku zote.
4. Ilimchukua nyumbani na unampa kila atakacho tatizo hujakaa naye kutaka kujua angependa afanye nini maishani mwake. Kumbuka sasa hivi hakuna ajira serikalini kama zamani wewe ndiye msaada kwake. Unaporudi nyumbani na kumkuta Kala Kalala hiyo kwake yeye inamuongezea stress maana hakusikii ukimuuliza mpango wake.
5. Huwezi jua unapoondoka huku nyumbani anaishi vipi na mwenye nyumba upande wa pili yaani mkeo. Unaweza kuona stress zingine ni vijicho vya mkeo vioimtaka aondoke nyumbani.
6. Kifupi mfungulie miradi aondokane na stress, jaamini siku moja itarudi hapa JF kutuambia mengine yaliyo mazuri kumhusu huyu mdogo wako
NB: Ule msemo wa " aliyefanya kazi na asile" unamsuta mdogo wako mpe mradi auendeleze na umwambie kuwa ni mradi wake wake moja kwa moja.
ASANTE
 
Unakosea sana..! Mkodishie chumba mlipie miezi 3, kagodoro kadogo, na neti kisha timua nyumbani kwako.
 
Mkuu nimekupata sana
 
Habari

Kuna mdogo wangu mhitimu wa chuo kikuu mwaka huu mwezi wa 7.

Baada ya kumaliza chuo nilimfwata nyumbani kwa mzee nikamchukua nakuishinae hapa nyumbani kwangu.

Lakini baada ya kukaanae nimegundua kuwa dogo anapresha ya maisha, yani anastress kutokana nakuwaza sana maisha.

Hali hiyo humfanya kutokuwa na furaha kabisa ilhali hakuna anachokosa hapa nyumbani maana anakula vizuri na kulala vizuri.

Sasa ndugu zangu naombeni ushauri nifanye nini hili nimsaidie dogo maana naona anakosa furaha muda mwingi asijekuathirika kisaikolojia
Follow this link to join my WhatsApp group: https://chat.whatsapp.com/KUpcNlnUNQCBukQVMilKVj
 
Habari

Kuna mdogo wangu mhitimu wa chuo kikuu mwaka huu mwezi wa 7.

Baada ya kumaliza chuo nilimfwata nyumbani kwa mzee nikamchukua nakuishinae hapa nyumbani kwangu.

Lakini baada ya kukaanae nimegundua kuwa dogo anapresha ya maisha, yani anastress kutokana nakuwaza sana maisha.

Hali hiyo humfanya kutokuwa na furaha kabisa ilhali hakuna anachokosa hapa nyumbani maana anakula vizuri na kulala vizuri.

Sasa ndugu zangu naombeni ushauri nifanye nini hili nimsaidie dogo maana naona anakosa furaha muda mwingi asijekuathirika kisaikolojia
Mtafutie milion moja halafu nimuunganishe na jamaa wako China na Vietnam aagize mzigo auze aanze kupiga hela baadaye atakuwa ashazoea maisha
 
Back
Top Bottom