Msaada: Mdogo wangu ana stress za maisha

Msaada: Mdogo wangu ana stress za maisha

Mbotech

Member
Joined
Aug 23, 2019
Posts
81
Reaction score
79
Habari

Kuna mdogo wangu mhitimu wa chuo kikuu mwaka huu mwezi wa 7.

Baada ya kumaliza chuo nilimfwata nyumbani kwa mzee nikamchukua nakuishinae hapa nyumbani kwangu.

Lakini baada ya kukaanae nimegundua kuwa dogo anapresha ya maisha, yani anastress kutokana nakuwaza sana maisha.

Hali hiyo humfanya kutokuwa na furaha kabisa ilhali hakuna anachokosa hapa nyumbani maana anakula vizuri na kulala vizuri.

Sasa ndugu zangu naombeni ushauri nifanye nini hili nimsaidie dogo maana naona anakosa furaha muda mwingi asijekuathirika kisaikolojia
 
Talk to him and listen what he wants. If possible, take him to a psychotherapy session. Maana ni vitu vidogo kama hivyo vinaweza vikaleta madhara makubwa wakati ambao hata hutegemei.

Imagine people cut their lives short and it's something that could be mitigated... Depression is real na watu hawakubali. Sad!
 
Take him to a psychotherapy session. Maana ni vitu vidogo kama hivyo vinaweza vikaleta madhara makubwa wakati ambao hata hutegemei.

Imagine people cut their lives short and it's something that could be mitigated... Depression is real na watu hawakubali. Sad!
hivi tunaelekea wapi aisee? kwanini tuna uzungu sana siku hizi?

kijana ana stress za maisha na wewe ushauri wako wa kwanza ni zitumike gharama za kumlipa specialist ili amsikilize na kumpa ushauri? kabisa yani?

kweli social life is dead. inasikitisha.
 
Sio uzungu, kaka. All humans are the same no matter the race!

Wa Tanzania wengi hatuamini hiki kitu lakini kipo - Sonona ipo tena kwa asilimia zaidi ya mia! Kuna vijana wanaamua kujitoa duniani kwa sababu hizo na ni suala ambalo lingezuilika kwa maongezi tu - Yaani kubadilisha mtazamo wa muathirika kwa maongezi tu.

Kama ulinielewa nilianza na "talk to him" na uelewe anataka nini.. Ila kwa wewe haitakuwa accurate sana ukilinganisha na therapist ambae ataelewa moja kwa moja shida na namna ya kuisolve!!

But again! Is money more important than rescuing a human??
 
mpaka unaenda kwa specialist kuongea nae maana yake njia zote za mazungumzo zimeshindikana,
mpaka unaenda kwa specialist manake kwenye ukoo hakuna mtu mwenye uwezo wa kumuweka sawa kijana wao,
mpaka unaenda kwa specialist manake umekosa marafiki kabisa wa kuzungumza nao.

mimi nashauri amtafute mtu mzima aongee nae, ikishindikana basi kakaake arudi hapa JF aombe mtu ajitolee kumshauri mdogo wake.

mimi naamini humu kuna washauri wazuri, watu wenye uwezo wa kuongea na mtu mpaka akili ikakaa sawa..
na anaweza akapata mtu mwenye roho ya usamalia mwema akasaidiwa bila gharama zozote.
 
Unakula una lala bure ufanyi kazi mwanangu mtafutie kazi ata ya kuchanganya zege pili mtafutie demu apige show sometime nyenge nazo zinaleta mfadhaiko wa moyo

Mkuu nimekuelewa vizuri sana
 
mpaka unaenda kwa specialist kuongea nae maana yake njia zote za mazungumzo zimeshindikana,
mpaka unaenda kwa specialist manake kwenye ukoo hakuna mtu mwenye uwezo wa kumuweka sawa kijana wao,
mpaka unaenda kwa specialist manake umekosa marafiki kabisa wa kuzungumza nao.
mimi nashauri amtafute mtu mzima aongee nae, ikishindikana basi kakaake arudi hapa JF aombe mtu ajitolee kumshauri mdogo wake.
mimi naamini humu kuna washauri wazuri, watu wenye uwezo wa kuongea na mtu mpaka akili ikakaa sawa..
na anaweza akapata mtu mwenye roho ya usamalia mwema akasaidiwa bila gharama zozote.
Naelewa tunakwepa gharama ndiyo. Kuna freelancing therapist mbona!! I'll check and let you know where you can get one if you accept.!

Hio ishu iko serious na inaweza ikaleta matokeo ya ajabu kuliko hasara ambazo ungezipata endapo ungelipia kupata msaada wa kitaalamu. Hata hivyo, hio kitu huwezi kuelewa inavyotesa mpaka ikutokee. Kama nakumbuka vyema, sikuwa nalala kwa amani usiku. Nasikia masauti yanaongea na mimi na sielewi yanasema nini!! Hio ni kwa upande wangu na kila mtu inampata kivyake, na kwa staili yake. Lakini asikuambie mtu: Kama hupati mtu wa kuongea nae itakutesa sana na kuwaza kifo ndiyo impulse ya kwanza!!

Hata hivyo I have no say in this. Nilikuwa natoa tu ushauri... You do whatever floats your boat.
 
Kijana ana ambition katika maisha. I am like him. Maisha ni zaidi ya kula na kulala. Siwezi kulala mpaka kieleweke. Anafikiria beyond leo. Anafikiria maisha yake na familia yake ya baadae. Kama una mtaji, mfungulie biashara ajaribu.
 
Back
Top Bottom