Msaada: Mdogo wangu ana stress za maisha

Msaada: Mdogo wangu ana stress za maisha

Huyo kamaliza juzi tu bado mbichi.....
mwambie atulie.....
kuna njemba ziligraduate miaka 11 iliyopita zipo street tu.....
zikajiongeza baadhi zinafanya vizuri kwenye kilimo na biashara.....
sio mpaka uajiriwe....
mimi nawakubali sana watu wanaosaka mitaji..... wenye plan....
 
Hii hali ilintokea kipindi hicho nimemaliza chuo,, broo alingundua mapema akanichana live, akasema dogo acha mawazo mambo yatajipa tu,,

Ila nlipata pa kuingiza buku 3 kwa siku + misosi juu,, ile hali ikatoweka kabisa ya kuwaza ,,

Ilikuwa 2009,
 
Stress zitamuua,askae sana ndani kunaboa sana...cha msing afanye issue yyte kitaa hata sport inasaidia kuondoa stress
 
Kuna watu wenye stress wewe sio huyu acha utani yeye ni fresh from collage, bado ajasota mtaani miaka 5, anakula aumwi, muulize vizur labda kagombana na mpenzi wake, ,
 
Aisee, kumbe haya mambo yapo for real, kwa ku-share namna hii kuna mtu unamponya mahali... [emoji119]
Hicho kipindi aisee ni kibaya sana,tena kwa mtoto wa kike nadhani ni kipindi kibaya zaidi tho' binadamu ni binadamu,.niliwahi kukieksipiriensi few years ago...lol[emoji23][emoji23][emoji23]nyumbani unakula vizuri tena wakati mwingine wewe ndio unapanga mle nini japo huna hata100 mbovu,unalala vizuri and you can hang out with friends sometimes lakini nilijihisi kabisa siko sawa i need something extra,nahitaji KUJITEGEMEA hata kama niko home nahitaji kuwa na "cha kwangu" yaani unakuwa na stress halafu sijui inakuwaje kipindi hiki nacho mahusiano hayanogi yaani hupati mtu yule unamuhitaji daaah[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]but all in all ni kipindi kifupi lakini kina mapito ambayo ukivuka salama hakika taji inakuhusu nilikuwa napenda kujiongelesha kwa sauti "Abba Father where are You" "are you listening" "why this" "please help me".....

Ndugu wa karibu pia mna mchango mkubwa wa kumpunguza hayo mawazo,kumpa moyo kwa mifano iliyo hai na kumuhusisha na mambo ya IMANI kama niwaamini..
 
Mwambie akatafute kazi kama ngumu kupata atafute hata sehemu ya kujitolea kulingana na fani yake. Ili aweze kujuana na watu wengi na kujenga connection
 
mpaka unaenda kwa specialist kuongea nae maana yake njia zote za mazungumzo zimeshindikana,
mpaka unaenda kwa specialist manake kwenye ukoo hakuna mtu mwenye uwezo wa kumuweka sawa kijana wao,
mpaka unaenda kwa specialist manake umekosa marafiki kabisa wa kuzungumza nao.

mimi nashauri amtafute mtu mzima aongee nae, ikishindikana basi kakaake arudi hapa JF aombe mtu ajitolee kumshauri mdogo wake.

mimi naamini humu kuna washauri wazuri, watu wenye uwezo wa kuongea na mtu mpaka akili ikakaa sawa..
na anaweza akapata mtu mwenye roho ya usamalia mwema akasaidiwa bila gharama zozote.

Hujaelezea izo streess zake ni zakupata kazi maalum au toyote ilimradi apate kazi.

Yupo kimya au anaropokwa ili apate kazi? Anawalazimisha hata nyinyi mumpatie kazi?

Ana muda gani amemaliza chuo ana majukumu gani mengine yanayomlazimu ateseke kama hana kazi?
 
Hujaelezea izo streess zake ni zakupata kazi maalum au toyote ilimradi apate kazi.

Yupo kimya au anaropokwa ili apate kazi? Anawalazimisha hata nyinyi mumpatie kazi?

Ana muda gani amemaliza chuo ana majukumu gani mengine yanayomlazimu ateseke kama hana kazi?
mimi mchangiaji tu chief hayo siyajui.
 
Unamshangaa, endelea kumpa ugali after two yrs ndo utamshangaa vizuri kama co kumtimua kwako TAKE MEASURES
 
Back
Top Bottom