Aisee mimi nilisambaza CVs kama mchele ila bado nikatoka kapa,nikajaribu kujitolea miezi miwili tu nikaacha coz huku najitolea na mama mwenye nyumba nae alikua anatishia kunitolea vyombo nje,..ni wakati ambao kila ventures zangu ndogo ndogo zilipo dorola..ni wakati ambao nilijihisi kama sina msaada wowote dunia hii...yani kuna muda hata baadhi ya maboss ninaofahamiana nao nikaona kama wana nibania tu...kila nilofanya nikaona halifai,na kila alie nitizama nilihisi ana niona vile nawaza kichwani. Kuna muda nikahisi nilipoteza muda wangu kusoma chuo,hakika nilijutia sana! Nikahisi huenda nilipoteza muda...
Siku zilisonga bila mafanikio,matarajio yalimeza hata juhudi zangu za awali za utafutaji. Stress zilizonga maisha yangu,roho ya kukatia maisha tamaa ilikua ina ninyemelea but Tumaini lilikua kubwa kushinda roho hiyo. Mbaya zaidi sikua na mzazi au mlezi wa kunipa hata faraja tu kwa wakati huo.
Na nikipindi ambacho nilitamani hata nipate mtu nimweleze yake yanayo nisibu,..daaah sikumpata mtu huyo,na sidhani kama nitakuja kumpata...daah maisha ya upweke yasikie tu kwa jirani.
Ila yote yalipita,muda ulifika kila kitu kikawa mahala pake. Kazi sikupata kwa wakati huo,ila niliamua kubadili mtazamo na kusimama imara katika vijibihashara fulani vidogo vidogo,ubize ulipozidi na ile hali ikapungua kwa kiasi fulani,ingawa sonona ni sehemu ya maisha yangu.
So,huyo kijana namshauri atafutiwe kazi ya kufanya ili awe bize,pia mjenge kisaikolojia ili aondoe matumaini makubwa alojiwekea. Kula vizuri na kulala vizuri haiwezi kuwa chachu ya furaha yake, mpe uhuru kiasi. Namaanisha acha akapange na mpe kianzio cha bihashara au mtafutie pahala pa kujishikiza.
Aisee kipindi after chuo,kinatesa sana maana expectations vs reality ni tofauti, mi sikuhisi kama ningesota sana kitaa bila kazi,nilikua na stress mno nawaza hadi vocha niombe home[emoji30] acha tu, sambaza CVs kama mchele but no any call aisee.
Mshauri tu asijistress sana,ipo siku mambo yatakua poa, ajitahidi kusambaza CVs asichoke, pia kama unaweza mpa kimtaji ajishughulishe na vibiashara asikae idle,itamsaidia