Msaada mchanganuo wa kufunika nyumba hii

fundi msati

JF-Expert Member
Aug 22, 2013
203
67
Wadau habari,

Hapa nilitaka iwe vyumba 3 sebule na jiko. Nikapandisha ikafika sehemu ikakwama fedha ilikata ila najipanga niamie ili mengine yanikute hapohapo sasa naomba msaada wa makadilio ya kufunika hapo kuanzia kenchi na bati hapo palipopigwa lita kila chumba kina upana wa ft 10 vipo viwili na jikon ft 8 urefu ft 13.

Huku ambako sijapandisha kuna chumba na sebule ambacho upana wake jumla ni ft 28 urefu ft 24 naomba kujua bati ngapi? Pia naomba kujua bando moja huwa ina bati ngapi?? SAMAHANI kama kuna sehemu sijaeleweka.

IMG_20221022_090726.jpg
 
mimi sio fundi haya ni makadirio ya uzoefu

kenchi hapo ni 100-120
bati bando 2 (futi 10 moja na futi 8 moja) zinaweza sizitoshe ukaongeza bati (kama utatumia bati nyeupe)

kama watumia za rangi hapo bi bando 3

bati zinatofautina kwenye wingi hizi nyeupe zinakuwa 24 (futi 8) 20(futi 10)

kwa bati za rangi zinakuwa 16 kwa bando moja
 
Kam ni nyumba ya tofali za kuchoma basi paua kama wanavyopaua huko vijinin usije jaribu kupaua ukaweka mzigo mkubwa juu utaangusha nyumba
Unamaanisha kuezeka kwa kurefusha paa. Hata huku kwetu wanafanya hivyo na zinakubali tu tofali hizi za kuchoma ni imara kweli na kujengea tope au cement sio ttzo nymba nyingi ukija huku ukikuta zimesha kamilika huwezi amini kama ilianzia hivyo ok. Ila mimi upauwaji wakurefusha sana paa sivutiwi nao nataka kuwa na paa lakawaida tu
 
mimi sio fundi haya ni makadirio ya uzoefu

kenchi hapo ni 100-120
bati bando 2 (futi 10 moja na futi 8 moja) zinaweza sizitoshe ukaongeza bati (kama utatumia bati nyeupe)

kama watumia za rangi hapo bi bando 3

bati zinatofautina kwenye wingi hizi nyeupe zinakuwa 24 (futi 8) 20(futi 10)

kwa bati za rangi zinakuwa 16 kwa bando moja
Ahaa aiseeh nakushukuru sana sana comment yako imenipa mwanga kwa kweli Asante. Nilikuwa sijui idadi ya bando ya bati nita fatuta izo za rangi na nimesha ona uzi zakutosha zikizungumzia ubora wa bati kulingana na viwanda husika
 
Unamaanisha kuezeka kwa kurefusha paa. Hata huku kwetu wanafanya hivyo na zinakubali tu tofali hizi za kuchoma ni imara kweli na kujengea tope au cement sio ttzo nymba nyingi ukija huku ukikuta zimesha kamilika huwezi amini kama ilianzia hivyo ok. Ila mimi upauwaji wakurefusha sana paa sivutiwi nao nataka kuwa na paa lakawaida tu
Sio kwamba nasema sio imara mie mwenyewe Nina mpango wa kujrnga nyumba nzuri ya tofali za kuchoma. .

Nyumba yangu nilisimamishapaa kubwa Mita nane. Limekula bati na mbao balaa. Mwisho wa siku unaiwekea nyumba uzito mkubwa. .

Siku yakipita yake magari ya kushindilia Barabara nyumba inapasuka. .
 
Mkuu hizo tofali ni imara sana, na ukisema ujengee smenti utapata hasara,

mfano tofali 1500 utatumia mifuko 8,na nyumba kama hiyo tofali 1500 ni laini 3 tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom