Msaada kwenye tuta - sijielewi nilipofika

Msaada kwenye tuta - sijielewi nilipofika

kingwipa1

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2008
Posts
334
Reaction score
51
Kuna dada mmoja nimetokea kumpenda na kwa dalili alizonionyesha ni kwamba hata yeye ananipenda. Tumekuwa kwenye mahusiano karibia miezi sita sasa. Juzi kati aliugua na kulazwa na kwa mshangao wangu alinitaarifu juu ya hali yake nami nikaenda kumjulia hali.

Hapo nilipata nafasi ya kukutana na ndugu zake ambapo wengi wao wameonyesha kunikubali kwani tunaongea vizuri. Baada ya kupona alinitaarifu kuwa atakuwa na safari ambapo hakutaka kuniweka wazi ni safari ya namna gani na inahusu nini. Kuna muda nilikuwa nahisi kama itakuwa safari yakikazi na mara nyingine nikawa nafikiri mambo ya harusi kwani pia aliwahi kunidokezea juu ya kuhudhuria harusi mahali fulani.

Kitu kinachonitatiza ni kuhusu hii safari yake ya sasa, kwa kweli sikuwahi kuipinga na wala sikuwa na mpango wa kuipinga kwani najua yeye ni mtu huru na anahitaji kuzitafuta fursa mbalimbali za maisha. Tatizo langu ni kwamba safari yake imekuwa ya siri mno ingawa aliniaga ila hataki nijue yuko wapi na anafanya nini. Kuna kipindi aliniambia kuwa hatakuwa hewani, mimi nilidhani atasafiri nje ya nchi.

Tuliendelea kuagana mpaka alipotoweka hewani (nadhani alikuwa ndani ya ndege) kwa hiyo moja kwa moja nikajua ameenda ughaibuni kwa kuwa hakutaka kunijulisha anakoelekea na mimi nimeamua ku-compromise.

Kinachonifanya kuomba ushauri kwa wataalamu wa masuala ya mahusiano ni hiki nilichokiona leo. Nilikuwa kwenye shughuli zangu za kila siku na nikiwa kwenye kikao cha uongozi wa juu wa kazini kwetu meseji ikaingia kuifungua nikakuta meseji kutoka kwa kipenzi cha moyo wangu ikiwa ikinilaumu kwa kumtenga kwani sijawasiliana nae tangu alipoondoka.

Nilijitahidi sana kumsihi kuwa sijamtenga na nilidhani yuko nje ya nchi akadai hawezi kwenda mbali na mimi kiasi hicho. Baadae mawasiliano yalikatika ghafla na alipokuja kupatikana jioni alidai alikuwa kwenye kikao. Tuliendelea kujadili mambo yetu na baadae nikamuomba tuongee kwenye simu, kimsingi sikutaka kumlazimisha bali nilimuuliza muda gani yuko free ili nimpigie tuongee akaniuliza ninataka tuongee nini?

Sikufurahishwa na majibu yake kwa hiyo niliamua kupishia mbali na mara ya mwisho nilipo-m-text sikupata majibu mpaka nikapitiwa usingizi. Kwa sasa nimeamka na wala sina usingizi nimekuwa na mawazo kibao kichwani mpaka nikaamua kuamka na kuwasha laptop ili nijiliwaze kwa muziki laini. Hakuna faraja niliyopata zaidi ya stress juu ya stress na mara inakuja kichwani kitu kinachoniumiza roho yangu mpaka sijielewi.

Sijui kama nimekuwa pessimist katika kumuwazia mpenzi wangu ama ni taarifa za universe juu ya huyo mpenzi wangu. Kwa nini hajataka tuongee kwenye simu na ni kwa nini hataki nijue alipo kwa sasa?

Why, why, why!!!!!!
 
labda kazi yake usalama wa taifa hajakuamini kukuambia bado

Kazini kwake napajua na pia baadhi ya wafanyakazi wenzake wananijua. Shida ni kwa nini hataki nijue alipo na anafanya nini????
 
Kazini kwake napajua na pia baadhi ya wafanyakazi wenzake wananijua. Shida ni kwa nini hataki nijue alipo na anafanya nini????

labda ni kibuzi labda ni business ya siri....labda matibabu ya siri labda anything....why wewe hang on utajua tu
 
do not make decisions out of fear....endelea kuwa nae...ukweli utaujua tu...kama ana mtu au hana..utajua tu good things come to those who wait.....umeshakaribia kufika keep going....

Ushauri mzuri sana, but in this fragile world where a mistake can cost life, how comes akiwa ana mishe mishe zake. She said the ticket is not with her and she don't know where she was going. Is it true that you can arrange for a long safari without knowing where you are going. Confidence of a doubt!!!

Ninatamani mpenzi wangu awe muwazi kwani nimekuwa wazi kwake. Nilikuwa na safari ya kwenda nje ya nchi lakini nikaahirisha kwa ajili yake ili tupate muda wa kuwa pamoja kwani kwangu mimi kusafiri si shida. Kwa nini afanye safari ya siri??? Anyone out there for help/ideas
 
labda ni kibuzi labda ni business ya siri....labda matibabu ya siri labda anything....why wewe hang on utajua tu

Yote ni sawa kwani ili kupata ukweli inabidi uamini kila unachoambiwa na mwisho wa siku uchange akili. I have a sense of detectives ila kwa hili niko gizani. Niko huru kwake na mimi nimemuomba awe huru kwangu kwani pamoja tunaweza kulindana.
 
with time utajua ukweli..so subiri tu
 
Read between the lines mwenye macho haambiwi ona
 
Kuna msemo unasema ''Mwongo mwongozeni''. Mwongoze pasipo kupandwa na hasira hadi pale utakapokuwa na uhakika wa ukweli wa safari yake.
 
Mmmh, binafsi napenda mwanaume mkali na possessive. Unamuitaje mpenzio kama anasafiri na hujui ameenda wapi, anafanya nini na anarudi lini, na hauna free access ya simu? Huo ni ubushoke bwana.

Mimi ni mwanamke, take it from me. Uko kwenye point ya kutengeneza ama kuvunja mahusiano. Chora mstari. Mwanaume ambaye ananifaa mimi angesema hivi: kama mimi ni mpenzio, nataka kujua uko wapi, unafanya nini na hata kama hamna tarehe kamili ya kurudi i demand kuwa updated. Sio kwa sababu ya wivu tu lakini ni kwa sababu nakupenda na nakujali. Otherwise im your casual friend, nikiwa na nafasi nitakupigia na wewe ukiwa na nafasi nipigie. Staki malalamiko. Period!

Hapo utazijua mbivu na mbichi na zilizooza mapema! Hivi unakuwaje na mpenzi anasafiri na usimpeleke airport ama ubungo? Mapenzi yenu ya kisikuhizi uvivu umewajaa sijui hata kunjunji kama hamtumii playstore applications hakyamama!
 
Kuna dada mmoja nimetokea kumpenda na kwa dalili alizonionyesha ni kwamba hata yeye ananipenda. Tumekuwa kwenye mahusiano karibia miezi sita sasa. Juzi kati aliugua na kulazwa na kwa mshangao wangu alinitaarifu juu ya hali yake nami nikaenda kumjulia hali. Hapo nilipata nafasi ya kukutana na ndugu zake ambapo wengi wao wameonyesha kunikubali kwani tunaongea vizuri. Baada ya kupona alinitaarifu kuwa atakuwa na safari ambapo hakutaka kuniweka wazi ni safari ya namna gani na inahusu nini. Kuna muda nilikuwa nahisi kama itakuwa safari yakikazi na mara nyingine nikawa nafikiri mambo ya harusi kwani pia aliwahi kunidokezea juu ya kuhudhuria harusi mahali fulani.

Kitu kinachonitatiza ni kuhusu hii safari yake ya sasa, kwa kweli sikuwahi kuipinga na wala sikuwa na mpango wa kuipinga kwani najua yeye ni mtu huru na anahitaji kuzitafuta fursa mbalimbali za maisha. Tatizo langu ni kwamba safari yake imekuwa ya siri mno ingawa aliniaga ila hataki nijue yuko wapi na anafanya nini. Kuna kipindi aliniambia kuwa hatakuwa hewani, mimi nilidhani atasafiri nje ya nchi. Tuliendelea kuagana mpaka alipotoweka hewani (nadhani alikuwa ndani ya ndege) kwa hiyo moja kwa moja nikajua ameenda ughaibuni kwa kuwa hakutaka kunijulisha anakoelekea na mimi nimeamua ku-compromise.

Kinachonifanya kuomba ushauri kwa wataalamu wa masuala ya mahusiano ni hiki nilichokiona leo. Nilikuwa kwenye shughuli zangu za kila siku na nikiwa kwenye kikao cha uongozi wa juu wa kazini kwetu meseji ikaingia kuifungua nikakuta meseji kutoka kwa kipenzi cha moyo wangu ikiwa ikinilaumu kwa kumtenga kwani sijawasiliana nae tangu alipoondoka. Nilijitahidi sana kumsihi kuwa sijamtenga na nilidhani yuko nje ya nchi akadai hawezi kwenda mbali na mimi kiasi hicho. Baadae mawasiliano yalikatika ghafla na alipokuja kupatikana jioni alidai alikuwa kwenye kikao. Tuliendelea kujadili mambo yetu na baadae nikamuomba tuongee kwenye simu, kimsingi sikutaka kumlazimisha bali nilimuuliza muda gani yuko free ili nimpigie tuongee akaniuliza ninataka tuongee nini??

Sikufurahishwa na majibu yake kwa hiyo niliamua kupishia mbali na mara ya mwisho nilipo-m-text sikupata majibu mpaka nikapitiwa usingizi. Kwa sasa nimeamka na wala sina usingizi nimekuwa na mawazo kibao kichwani mpaka nikaamua kuamka na kuwasha laptop ili nijiliwaze kwa muziki laini. Hakuna faraja niliyopata zaidi ya stress juu ya stress na mara inakuja kichwani kitu kinachoniumiza roho yangu mpaka sijielewi. Sijui kama nimekuwa pessimist katika kumuwazia mpenzi wangu ama ni taarifa za universe juu ya huyo mpenzi wangu. Kwa nini hajataka tuongee kwenye simu na ni kwa nini hataki nijue alipo kwa sasa????

Why, why, why!!!!!!

She is cheating you. Chunguza taratibu utajua.
 
Ushauri mzuri sana, but in this fragile world where a mistake can cost life, how comes akiwa ana mishe mishe zake. She said the ticket is not with her and she don't know where she was going. Is it true that you can arrange for a long safari without knowing where you are going. Confidence of a doubt!!!

Ninatamani mpenzi wangu awe muwazi kwani nimekuwa wazi kwake. Nilikuwa na safari ya kwenda nje ya nchi lakini nikaahirisha kwa ajili yake ili tupate muda wa kuwa pamoja kwani kwangu mimi kusafiri si shida. Kwa nini afanye safari ya siri??? Anyone out there for help/ideas
Kuna mdau kakuambia huenda ni mtu wa usalama wa taifa. Ninavyoona ni kweli coz nilikuwa na mtu kama huyo, madepression na mastress niliyapata sana. Na hata alivyokuja kuniambia nature ya kazi yake; l tried but it didn't work.
Kitendo cha kutokuonesha ticket, kutokuambia aliko ni typical style yao.
As The Boss said, tulia relax ukiweza na mwisho wa siku mambo yatakuwa sawa tu.
Ila watu wale wana maisha magumu hadi unawahurumia.
 
Last edited by a moderator:
Kazini kwake napajua na pia baadhi ya wafanyakazi wenzake wananijua. Shida ni kwa nini hataki nijue alipo na anafanya nini????

Wanakuwa na cover job, hivyo kupajua kazini kwake sio issue.
I have been there so l know. Give her a benefit of doubt. Usifikirie worse siku zote. Kuna black, white na greys zenye mkolezo tofauti.
 
Una ekti u zoba. Mark your territory mapemaaa. Utashangaa wengine wanang'oa mzigo mbele yako.

Miezi 6 mapenzi ya kaka na dada? Huko aliko kuna jamaa anakamua mzigo kwa kwenda mbele, lakini mdada anaonekana hajafika kivile, bado anasaka.

Sasa kazi ni kwako.
 
Nimekupenda bure.

Miezi 6 hawaambiani hata destination za safari zao? Huyu kaka kainamishwa, na akiendelea hivi hata walioana yeye ndio atakuwa mama wa nyumbani.

Back
Top Bottom