Msaada kwa ndugu yetu huyu

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,796
Last week nilipata mgeni toka nchi jirani ya Kenya. Ni mwana JF aliyekuja Tanzania kunitembelea. Siku ya Ijumaa iliyopita aliniaga kuwa ana hamu ya kufika beach, maisha yake mengi hajawahi kuwa karibu na Pwani

Hivyo aliondoka kuelekea Dar ili afike beach, mawasiliano na yeye yalikatika kwenye saa 12 jioni akiwa njiani kwenda Dar.
Siku ya Jumamosi mchana nikapata wito toka polisi Kigamboni kwamba kuna ndugu yangu yuko chini ya ulinzi hapo kituoni kwa makosa ya kutaka kujiua.. Ya kwamba jana yake usiku wa saa mbili akiwa kapanda kivuko cha Kigamboni arijirusha baharini kivuko kikiwa hakijafika upande wa pili. Aliokolewa na wazamiaji na kupelekwa kituoni na baadae hospitalini.

Jumamosi asubuhi alitolewa hospitali na kupelekwa polisi na Jumamosi jioni alihamishiwa toka kituo cha polisi Kigamboni na kuletwa kituo cha polisi kilicho karibu na Azam

Jumatatu asubuhi alikabidhiwa kwa maofisa Uhamiaji lakini changamoto ikawa hana nguo kwakuwa alizozama nazo hazikuwepo tena na alikuwa na shuka tu.

Nimeshafanya mpango wa nguo na slippers lakini kwa sasa hana document yoyote passport na simu na hela vilipotea wakati wa uokozi.

Niko mbali na Dar ambaye anaweza kutoa assistance yoyote tuwasiliane. Yuko kituo cha polisi marine na hana hata pesa ya kula.

Natanguliza shukrani
 
Mimi nasaidia wetu wa Mtaani kwanza, sina nilichobakiza kusaidia mgeni.

Kila la Heri!
 
Back
Top Bottom