Msaada kwa ndugu yetu huyu

Msaada kwa ndugu yetu huyu

Sio vizuri kufanya hivyo labda kwa ruhusa yake.. Ila aliye tayari kutoa msaada anaweza kufika pale Posta marine police aonane na mhanga moja kwa moja
Mshana Jr unaweza weka hapa majina kamili ya mtuhumiwa wa kutaka kujiua, kaunti aliyotokea, mtaa na picha?
Nadhani itasaidia pia upelelezi....japo pichani atakua kavaa shuka
 
Wasiliana na ubalozi wa Kenya.
mtoa hoja ni mtu mwenye staha kubwa na hawezi ku risk kuharibu wasifu wake kwa issue kama hii,umeshauri kitu kizuri sana kuwa awasiliane na ubalozi wake,but hii kwa nchi zetu za shithole ni ngumu mno,nimeshuhudia watanzania wengi ughaibuni wakipatwa na matatizo hizi balozi zetu ni useless kabisa,msaada unaotakiwa hapa na pesa za kujikimu na hati ya muda ya kusafiria lazima aripoti kwenye ubalozi wake,na nauli ya kumrudisha Kenya achangiwe nina hakika ubalozi wake utamtolea nje.
 
Sio vizuri kufanya hivyo labda kwa ruhusa yake.. Ila aliye tayari kutoa msaada anaweza kufika pale Posta marine police aonane na mhanga moja kwa moja
pls inbox me tuangalie jinsi ya kusaidiana ili mwenzetu arudi kwake,binafsi ninakuamini kuwa mkuu huwezi kabisa kufanya kitendo cha kutaka kutapeli kwa kutumia issue ndogo kama hii,mimi ninaoganise wenzangu wa hapa Lingusenguse ili to try to make a small difference.
 
NiMK254 NINI? embu punga mkono kama siyo wewe

Kha!! Haya maisha yalivyo matamu niache bidada wazuri nikajitose baharini huko Kigamboni...hehehe sio mimi.

Huyo itakua labda kweli anasumbuliwa na kifafa, tatizo miaskari ya kwenu Tanzania ina mihemko sana ikikamata Mkenya, hapo watamzingua mpaka akhera.

Mshana Jr muulize huyo Mkenya namba za mtu wao au ndugu yake yeyote Kenya nitawasiliana naye achakarike. Nitumie kwenye inbox, au hata kama hajui namba za ndugu yake yeyote aseme au ataje wapi ninaweza kwenda kumkuta mtu anayemfahamu, ofisi, duka la mtaani chochote au yeyote wanayefahamiana naye.
.
Hayo ya ubalozi yatakuchelewesha, japo wanaweza wakaingilia ila issue itakwenda kwa kasi kama ndugu zake watahusishwa. Wao watakuja huko na kuchakarka na kuhusisha ubalozi na mengine yote.
 
Unajua kuna watu (haters) wapuuzi wachache wanajaribu kupotosha.. Sasa hapo mimi nataka nitapeli nini hapa kwa mfano

Nilichoomba ni msaada kwa mtu aliye polisi na kituo nimetaja.. Kuna watu upunguani umewajaa vichwani...
Kuna namba ya askari nimeweka hapo juu pls jaribu kucheki naye
pls inbox me tuangalie jinsi ya kusaidiana ili mwenzetu arudi kwake,binafsi ninakuamini kuwa mkuu huwezi kabisa kufanya kitendo cha kutaka kutapeli kwa kutumia issue ndogo kama hii,mimi ninaoganise wenzangu wa hapa Lingusenguse ili to try to make a small difference.
+255692604026
 
Kwa connection ulizonazo sidhani kama umeshindwa kupata mtu aliyeko Dar akakusaidia.

Kitendo cha kuleta hii issue hapa tells something fishy is around the corner.

Kama kweli mtu katoka Kenya kaja kutembelea Tanzania sidhani kama alikuwa na shida sana ya kufika beach, sababu hata Kenya beach zipo pia. Gharama za kwenda beach Kenya ni ndogo kuliko kuja beach za Tanzania. Umejiridhisha vp sio shushushu au mtu mwenye nia ovu?

Pia inawezekana vipi mtu atoke nchi jirani aje kukutembelea wewe, then umuache aende peke yake mkoa mwingine? Sababu wewe upo Pwani, ulimruhusu vipi aje Dar?

Kingine, inakuwaje mgeni wa nchi kama huyo, adai anaenda beach, then aache beach zooooote ambazo hazihitaji kupanda kivuko then aende Kigamboni ambako kunahitaji kivuko?

Pia, inakuwaje hukumpa maelekezo aende beach gani for his/her safety ukamuacha aende Kigamboni mpaka yamemkuta ya kumkuta kama haya?

Lastly, kama kweli alikuwa mgeni wako, how comes unashindwa kujitoa kumsaidia? Kwa nini usiahirishe shughuli zako za siku 1 au 2 uje kumtoa selo rafiki yako?

Akili kumkichwa.


Cc Unforgetable
 
Asante kwa wale waliojitoa kwa hali na mali... Kuna wanaojipanga kufika kituoni... Wanaweza kuleta mrejesho
 
Back
Top Bottom