Msaada: Kutoka kwa wanasaikolojia wa mapenzi

Msaada: Kutoka kwa wanasaikolojia wa mapenzi

Natanguliza shukrani.

Mimi ni kijana wa miaka ya 27 nina shahada ya ualimu na ndo kazi yangu, niliyoipata mwaka huu. Tatizo langu wana MMU ni kwamba nimebahatika kuwa na wapenzi 2 kwa vipindi 2 tofauti ambao wanatoka kwenye familia bora ikifika kipindi cha kipindi cha uchumba huwa najiona sina hadhi ya kumuoa huyo binti na hivyo kuanza kumukwepa na hatimae kuachana. Hii inatokana na kuanza kujirudi mwenyewe kwa kuangalia background yangu.

Nimetoka familia fukara sana ambapo nimekulia ujombani, nimesoma kwa misaada ya watu mbalimbali, nimeishi kwa kutothaminiwa na mtu yoyote. Yapo mambo mengi ya kusimulia.

Na sasa nimempata mwngine ambaye tulisoma wote lakini wazazi wake ni wasomi na heshima zao pamoja na uchumi wa kati. Binti yupo tayari tuanze uchumba lakini yale mawazo yashaanza kunijia kwa kujiona sifai.

Je, nifanyeje au nisioe kabisa.

Nahitaji msaada wenu wana MMU

Asanteni

Pole sana ndugu;

Napenda kukupa ushauri ufuatao

1:Yakupasa kutambua kesho yako ni bora kuliko Jana yako na leo yako;Maisha uliyoyapitia ilikua ni darasa la kuyafurahisha maisha ya sasa

2:Mapenzi huwa hayana mahusiano yoyote na status za watu unaokua nao...

3:Tambua kua unaoa mke,hauoi familia kwa hiyo usitishwe na hali za wakwe na maisha ya ndoa ni ya kwako na mkeo na si ya ndugu zako

4:Tafuta upendo wa dhati

Ikiwa wewe na mwenzio mnapendana kwa dhati ni rahisi kuishi pamoja na yeye anaweza kukufanya usahau machungu ya nyuma..

Yangu ni hayo tu
 
Natanguliza shukrani.

Mimi ni kijana wa miaka ya 27 nina shahada ya ualimu na ndo kazi yangu, niliyoipata mwaka huu. Tatizo langu wana MMU ni kwamba nimebahatika kuwa na wapenzi 2 kwa vipindi 2 tofauti ambao wanatoka kwenye familia bora ikifika kipindi cha kipindi cha uchumba huwa najiona sina hadhi ya kumuoa huyo binti na hivyo kuanza kumukwepa na hatimae kuachana. Hii inatokana na kuanza kujirudi mwenyewe kwa kuangalia background yangu.

Nimetoka familia fukara sana ambapo nimekulia ujombani, nimesoma kwa misaada ya watu mbalimbali, nimeishi kwa kutothaminiwa na mtu yoyote. Yapo mambo mengi ya kusimulia.

Na sasa nimempata mwngine ambaye tulisoma wote lakini wazazi wake ni wasomi na heshima zao pamoja na uchumi wa kati. Binti yupo tayari tuanze uchumba lakini yale mawazo yashaanza kunijia kwa kujiona sifai.

Je, nifanyeje au nisioe kabisa.

Nahitaji msaada wenu wana MMU

Asanteni

Inferiority Complex. daima utakuwa kile fikra zako kinawaza. Kama umetimia kiakili, kiufahamu na kiviungo sidhani kama utakuwa na ufukara kiasi gani kupita dhana ya kibinadamu. Si kila alokuwa na wewe anataka kujua ulichonacho sometimes love is all that it takes.
 
Utakuwa na tatizo jingine mkuu,swala sio back ground yako. Hebu acha hizo bhana. Komaa nae mpaka mwisho.
 
That is inferiority complex ma men.... just try to kick it out...Damn!!

Itakukosesha mademu hiyooo shauriyako we iendekeze tu.
 
Back
Top Bottom