Natanguliza shukrani. Mimi ni kijana wa miaka ya 27 nina shahada ya ualimu na ndo kazi yangu, niliyoipata mwaka huu. Tatizo langu wana MMU ni kwamba nimebahatika kuwa na wapenzi 2 kwa vipindi 2 tofauti ambao wanatoka kwenye familia bora ikifika kipindi cha kipindi cha uchumba huwa najiona sina hadhi ya kumuoa huyo binti na hivyo kuanza kumukwepa na hatimae kuachana. Hii inatokana na kuanza kujirudi mwenyewe kwa kuangalia background yangu. Nimetoka familia fukara sana ambapo nimekulia ujombani, nimesoma kwa misaada ya watu mbalimbali, nimeishi kwa kutothaminiwa na mtu yoyote. Yapo mambo mengi ya kusimulia. Na sasa nimempata mwngine ambaye tulisoma wote lakini wazazi wake ni wasomi na heshima zao pamoja na uchumi wa kati. Binti yupo tayar tuanze uchumba lakini yale mawazo yashaanza kunijia kwa kujiona sifai. Je nifanyeje au nisioe kabisa. Nahitaji msaada wenu wana MMU, asanteni