Msaada: Kutoka kwa wanasaikolojia wa mapenzi

Msaada: Kutoka kwa wanasaikolojia wa mapenzi

Msigazi Mkulu

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2013
Posts
4,186
Reaction score
3,421
Natanguliza shukrani.

Mimi ni kijana wa miaka ya 27 nina shahada ya ualimu na ndo kazi yangu, niliyoipata mwaka huu. Tatizo langu wana MMU ni kwamba nimebahatika kuwa na wapenzi 2 kwa vipindi 2 tofauti ambao wanatoka kwenye familia bora ikifika kipindi cha kipindi cha uchumba huwa najiona sina hadhi ya kumuoa huyo binti na hivyo kuanza kumukwepa na hatimae kuachana. Hii inatokana na kuanza kujirudi mwenyewe kwa kuangalia background yangu.

Nimetoka familia fukara sana ambapo nimekulia ujombani, nimesoma kwa misaada ya watu mbalimbali, nimeishi kwa kutothaminiwa na mtu yoyote. Yapo mambo mengi ya kusimulia.

Na sasa nimempata mwngine ambaye tulisoma wote lakini wazazi wake ni wasomi na heshima zao pamoja na uchumi wa kati. Binti yupo tayari tuanze uchumba lakini yale mawazo yashaanza kunijia kwa kujiona sifai.

Je, nifanyeje au nisioe kabisa.

Nahitaji msaada wenu wana MMU

Asanteni
 
Mwalimu unatuangusha wenzio bana. Sisi ndio watu muhimu sana hapa nchini. Go ou'there and knock 'em dead.
 
Umesoma chuo gani.?? Maana haiwezekani ikawa UDSM..
 
Ondoa wasiwasi km mkristu muombe toho mt akupe ujasiri na ujitahidi kisaikolojia pia. Km ni mkweli atakupenda vile ulivyo sio kwa bkground yako. Hilo sio muhimu. Akianza mambo ya bkground ni mlafi hakufai hana mapenzi ya kweli. Ni ujasiri wako. Ondoa fikra potofu kwenye hiloboga. Hii mentalitu mbaya sana. Mindset za wengi zipohivyo. Inabidi kubadilika. Komaa ondoa woga thats all u neef
 
Sasa ukiwakwepa utasaidikaje!? Kuna wanawake hawajali background yako ya kifukara isipokuwa mtaendeleeaje na maisha yenu na kufanikiwa.

Piga moyo konde na sahau yaliyopita, wako wengi sana waliosoma kwa dhiki au kwa kuungaunga ila sasa ni watu wenye familia zao na wanafurahia maisha.

Ila pole pia hiyo ni sehemu ya maisha kulingana na ubora/uduni wa familia zetu. Jitahidi wanao wasijekupitia yake maisha ya dhiki uliyoyapitia.
 
Nashukuru sana mwana MMU, hayo mawazo huwa yananipeleka mbali na kusema hyu wife atakosa hata mashemeji na mawifi wa kujivunia. Na ndo naanza maisha yaani hata nyumbani hakuna.
 
Muhimu kwenye life ni future
na sio past

na hata hao unao waona wako juu...we hujui walianzia wapi

Tanzania watu wachache sana wanatoka familia bora toka enzi na enzi
wengi wako kama wewe tu....wewe unajistukia tu
 
Nikiwa kama katibu wa walimu hapa JF nasema umetuangusha sana
 
Sasa ukiwakwepa utasaidikaje!? Kuna wanawake hawajali background yako ya kifukara isipokuwa mtaendeleeaje na maisha yenu na kufanikiwa.

Piga moyo konde na sahau yaliyopita, wako wengi sana waliosoma kwa dhiki au kwa kuungaunga ila sasa ni watu wenye familia zao na wanafurahia maisha.

Ila pole pia hiyo ni sehemu ya maisha kulingana na ubora/uduni wa familia zetu. Jitahidi wanao wasijekupitia yake maisha ya dhiki uliyoyapitia.

Asante madam kwa ushauri mzuri ndo maana nimeamua niliweke wazi hili jambo kuliko kunikaa rohoni tu japo wengine wananibeza.
 
We piga ngozi hiyo muambie maisha mnaanza wote from 0 ,vya baba au mama huko huko kwao
 
Muhimu kwenye life ni future
na sio past

na hata hao unao waona wako juu...we hujui walianzia wapi

Tanzania watu wachache sana wanatoka familia bora toka enzi na enzi
wengi wako kama wewe tu....wewe unajistukia tu

Nashukuru sana mkuu The Boss, nilihitahi motuvation kama hiii.
 
Back
Top Bottom