Msaada kumpata mtu aliyepokea muamala kimakosa

Msaada kumpata mtu aliyepokea muamala kimakosa

Bigmaaan

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2023
Posts
624
Reaction score
1,367
Kuna jamaa yangu kamtumia Mtu 700,000 badala ya 70,000. Jamaa alifanya naye biashara ni chinga. Tunduma. Sasa jamaa amegundua siku 2 baadae. Akamcheck chinga akagoma, wakakubaliana waonane amuonyeshe Muamala. Akazima simu.

So, anawezaje mtrace? Maana hata namba amesajilia ya mtu mwingine.
 
Zoezi la usajili wa laini za simu kwa alama za vidole lingerudiwa tu likiwa limeboreshwa na kuziba mianya ya watu kusajiliana ama mawakala kughushi,hili lishabuma!! Hakuna maana yoyote tena.
 
Pole sana, mm nimewahi wekewa 1.5 mil kwenye simu yangu badala ya laki na 50...nikaenda home usiku wakagundua nikapigiwa simu nikasema kweli njooni mchukue hela yenu..wakaja kuichukua hawakuamini Hadi kesho🤣🤣🤣..mdada akashukuru sana aliniambia wangemkata mshahara Hadi hiyo hela iishe😀😀
 
Kuna jamaa yangu kamtumia Mtu 700,000 badala ya 70,000. Jamaa alifanya naye biashara ni chinga. Tunduma. Sasa jamaa amegundua siku 2 baadae. Akamcheck chinga akagoma, wakakubaliana waonane amuonyeshe Muamala. Akazima simu.

So, anawezaje mtrace? Maana hata namba amesajilia ya mtu mwingine.
Wewe! Mmachinga anasaga lami kila siku anatafuta jero halafu arudishe 700000 kiboyaboya tuu? Kwanza hakuna ushahidi kama hiyo laki 7 siyo mliyokubaliana. Hata ukimpata akasema ndiyo hela mlikubaliana kuna mahali mliandikiana 70000?
 
Kuna jamaa yangu kamtumia Mtu 700,000 badala ya 70,000. Jamaa alifanya naye biashara ni chinga. Tunduma. Sasa jamaa amegundua siku 2 baadae. Akamcheck chinga akagoma, wakakubaliana waonane amuonyeshe Muamala. Akazima simu.

So, anawezaje mtrace? Maana hata namba amesajilia ya mtu mwingine.
Mwambie ajiunge Jf kila siku watu wanaolizwa ni jamaa yangu
 
nenda cybercrime unit, watakusaidia. laki sita na selasini elfu ni nyingi
Cybercrime ya hapa hapa hapa Tanzania?? Kama ni ya hapa Tanzania basi huo muda wa kupoteza kuonana na hao jamaa aweke nguvu kufanya kazi kulipishia hiyo hasara.

Ila kama ataenda kwa Hawa cyber kanjanja wetu wa Tanzania ajiandae kupoteza zaidi ya alichokipoteza
 
Zoezi la usajili wa laini za simu kwa alama za vidole lingerudiwa tu likiwa limeboreshwa na kuziba mianya ya watu kusajiliana ama mawakala kughushi,hili lishabuma!! Hakuna maana yoyote tena.
Tatizo siyo alama za vidole..tatizo ni mifumo ya pesa kwenyesimu ilitakiwa kuboreshwa ...mfano pesa ikitumwa kuwe na mifumo miwili
1) mfumo wa haraka(special)
2) mfumo usio wa haraka (normal)

Mfumo wa haraka uwe na malipo.. unalipia kwa mtumaji na mpokeaji ...yaani ukitaka kutuma fedha yenye kuitajika kwa haraka kutolewa kwenye simu ndani ya masaa 24 lazima mlipie malipoya ziada...hii itapunguza asilimia 90% ya mtu kuchukua pesa uliyotuma kimakosa na itazuia wizi wa haraka ..yaani pesa kutolewa kwa haraka...

KITENDO CHA MAKAMPUNI YA SIMU KURUHUSU PESA KUTOLEWA KWA HARAKA NI SABABU KUU YA KUIBIWA NA KUPOTEZA PESA ZAO
 
Tatizo siyo alama za vidole..tatizo ni mifumo ya pesa kwenyesimu ilitakiwa kuboreshwa ..
Lengo la kusajili laini kwa alama za vidole unalijua?

Siyo kwenye kutumiana pesa tu,hata uhalifu mwingine unaohusisha simu kwa sasa wahusika hawapatikani.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Back
Top Bottom