Msaada kujua gharama ya kufyatua tofali 4,800

Asante sana mkuu, nataka hiyo ya mikono kwahiyo niagize mikoani?

Hata huku zinapatikana ila inatakiwa uwaambie thickness ya chuma kinachotengenezea inatakiwa chuma kinene na sio "CHUMA MPESE MPESE"! Nyingi zile ambazo tayari zimetengenezwa ni famba haziwezi kuhimili mikiki ila chuma kinene bei yake pia imechangamka kwa DAR!! Kwa Mkoa ni 300k ila huku unaweza kuambiwa 450k.

Ila kama unataka kwa biashara ni nzuri ila kama ni kufyatua tofali onetime ni bora ukodishe tu.
 
Hata huku zinapatikana ila inatakiwa uwaambie thickness ya chuma kinachotengenezea inatakiwa chuma kinene na sio "CHUMA MPESE MPESE"! Nyingi zile ambazo tayari zimetengenezwa ni famba haziwezi kuhimili mikiki,ila chuma kinene bei yake pia imechangamka kwa DAR!! Kwa Mkoa ni 300k ila huku unaweza kuambiwa 450k.

Ila kama unataka kwa biashara ni nzuri ila kama ni kufyatua tofali onetime ni bora ukodishe tu.
Ninaitaka one-time for now

But nitaitumia kujenga nyumba nyingine mbele huko
 
Watu mnabwabwaja tu ili muonekane wazee wa viwango, ni aidha mnaishi kwa shemeji hamjui kitu au lengo lenu ni kukatisha tamaa wenzenu!

Mfuko tofali 19!!
Yaani bora umewajibu hao vijana ambao hawajawai haya kufanya ujenzi wa kibanda cha sungura.

Mimi nimefyatua kwa ratio ya 45 na tofali ni nzuri tu.

Wanaotumia mashine wanapiga hadi tofali 55- 60 kwa mfuko ila zinapigwa maji mengi tu.

Yaani tofali 19 au 25 kwa mfuko nani angefanya biashara kichaa ya tofali.
 
Wengi humu ni watu mnaongea bila experience mnaongea kutokana na madesa tu ila ufuko mmoja ni tofali 25-60 strength inategemea na mambo mengi kama aina ya cement maana kuna 42.5R ,32.5R n.k ,umwagiliaji, compaction n.k.

Ukisoma kwenye mfuko wa cement wameweka ratio ya cement to sand mfano 1:3 for bricks (matofali) lakini uswahilini mafundi wanapiga 1:6 mpaka 1:8 hapo unapata mpaka tofali 60 na bado maisha yanaenda unaangalia na uchumi wako .
 
Mkuu tofali 45 kwa Mfuko wa Cement hapo ni Biskuti unatengeneza,
Angalau hata Tofali 35 kwa mfuko sio mbaya
Achana na ujenzi wa pdf na project za serikalini. Njoo mtaani uone uhalisia wa mambo.

Tofali zinatoka mpaka 50 sembese 45 na zinadumu miaka nenda rudi hakuna cha ufa wala nini
 
On a roughly but serious note:

Kwa hesabu ya tofali 45, kwa tofali 4800 utahitaji simenti mifuko takribani 110. Kwa bei ya 20,000/- kwa mfuko ni 2.2M.

Mchanga kila tripu ikupe tofali 200, utahitaji tripu 24... bei ya mfano ni 50,000/- kila hivyo itakula 1.2M.

Fundi wa kupiga tuseme utamlipa 150 hadi 200 kwa tofali, tuweke 800k.

Jumla kuu ni 2.2M+1.2M+800k = 4.2M.

Hapo bado maji, hatujui kama ni ya kulipia au niaje... na ishu ya kumwagilia hizo tofali sijui itakuwa kwako au kwa mpigaji!

Weka laki hapo ziada ihusishe huduma kama hizo.

Wakati huo, tofali zilizo tayari zinauzwa 1000 hadi 1200.... jumla 4.8M hadi 5.8M sijui kuhusu usafiri.

Piga hesabu utajua kiasi cha kuokoa hapo, na muda wako na usumbufu wa kusimamia na kuhakikisha kazi inafanyika kwa ubora.

Laki tano hadi milioni unaweza kuokoa.

Kumbuka mwaka huu sio wa kupata raha sana.
Nimependa makisio haya.
 
Back
Top Bottom