Kipi Bora kati ya kununua Tofali na kufyatua mwenyewe

Mkulima na Mfugaji

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,013
1,634
Habari Wana ujenzi, nilikua naomba ufafanuzi kati ya kununua Tofali za block kutoka kiwandani na kupeleka site na kununua Material na kupeleka site na kufyatua pale pale site.

Mfano kama nina million 2 hapo nikinunua Tofali kiwandani napata Tofali 2000 mpaka site je nikifyatua mwenyewe naweza kupata Tofali ngapi,?
 
Kufyatua ni best option maana utapata matofali ya ubora unaotaka na kwa uhakika 100%

Mtaji wa hili ni MUDA tu.

Kununua n labda kwa kazi ndogo ndogo,ila kazi kubwa kama kupandisha nyumba,Fensi,nk (Fyatua mkuu).
 
Uko sahihi, kufyatua mwenyewe ni bora sababu unaweza kufyatua tofali imara tofauti na kununua ambao tofali haziwi imara.
 
Muda ninao tena wa kutosha tu wa kuweza kusimamia
Nunua. Ili kufyatua tofali 2500 unahitaji mifuko 100 ya cementi. Kama mfuko wa cementi ni 16-18,000/= *100 = 1,800,000/ lori za mchanga 14 @80000/= maji ya kufyatulia na kunyeshea lita 20,000, fundi wa kufyatua tofali@200/= kwa tofali. Piga hesabu uone wapi parefu. Bado fundi hajakuibia cementi
 
Sasa wale wa kuuza wanapataje faida ikiwa cement mifuko yote hiyo plus gharama zingine?
 
Wananunua cementi nyingi kwa bei ya jumla, na wanaletwa hadi site bure.

Wanapata Cementi ya mchongo,

wanafyatua tofali zaidi ya 25 kwa mfuko na kwa kua zinashindiliwa kwa mashine ni ngumu sana.

Akifyatua kwa mkono tofali 30 kwa mfuko zitakuwa za kiwango cha chini sana.
 
Habari Wana ujenzi, nilikua naomba ufafanuzi kati ya kununua Tofali za block kutoka kiwandani na kupeleka site na kununua Material na kupeleka site na kufyatua pale pale site
Mfano kama nina million 2 hapo nikinunua Tofali kiwandani napata Tofali 2000 mpaka site je nikifyatua mwenyewe naweza kupata Tofali ngapi,?
Hata mimi niko kwa hiyo dilemma nahitaji tofali nyingi sana ..nipo na miezi miwili tu kujenga nyumba ya ghorofa moja . Likizo yangu ni miezi miwili
 
Nunua. Ili kufyatua tofali 2500 unahitaji mifuko 100 ya cementi. Kama mfuko wa cementi ni 16-18,000/= *100 = 1,800,000/ lori za mchanga 14 @80000/= maji ya kufyatulia na kunyeshea lita 20,000, fundi wa kufyatua tofali@200/= kwa tofali. Piga hesabu uone wapi parefu. Bado fundi hajakuibia cementi
Mfuko mmoja tofali 25???? Hizo ni tofali za kisima au foundation ya ghorofa?
 
Back
Top Bottom