Msaada kujua gharama ya kufyatua tofali 4,800

Tunauza mbao kwa bei ya jumla.Njoo ofisini kwetu TEGETA tukuhudumie kwa gharama nafuu sana:-
2*2 fut12=2500
2*2 fut12(treated) ya dawa=2800
2*2 fut18(treated) ya dawa=5000
2*4 fut12 treated(ya dawa)=5000
2*4 fut12 isiyo ya dawa=4500
1*6 fut12=4500
1*8 fut12=8000
1*8fut12 ya fisher board(treated)=9500
1*10 fut12=13000
1*10fut 18 fisher board( treated)=15500
2*4 fut18(treated)=9500
2*6 fut12=8000
1*4 fut12=2800
2*6 fut 18=19000
Tunapatikana muda wote kwa namba za simu zifuatazo:-
----0759630751
----0687371138
----0654830416

vile vile kuna huduma ya kuchana,kuranda na kusize mbao inapatikana ofisini kwetu
 
Ni vema tujifunze kufuata viwango (sisi sio wa kwanza kufyatua tofali, walishafyatuaga wenzetu huko miaka ya nyuma) ndio maana ikaonekana ni vema kuweka viwango katika kila kitu kinachofanyika...
Uko sahihi kabisa na hiyo kwa cement namba 42.5 angalau utoe tofali 35 zenye ubora wa hali ya juu kabisa ila kwa sement namba 32.5 angalau tofali 25 hapo utapata tofali zenye ubora wa hali ya juu na zisizo pukutika tena hasa kama unajenga nyumba yako binafsi usijibailie ili upate nyumba imara kabisa
 
Sure, ni kweli mfuko wa cement unatoa tofali hadi 50 na zinakuwa imara, cha msingi ni uchanganyaji mzuri na kuimwagilia vizuri hata wiki kama una maji ya kutosha!

Kupata tofali 4800 inabidi anunue mifuko 107 ya cement kwa idadi ya 45 kwa kila mfuko.

Mende moja ya 14.5 - 16m3 inachapa mifuko 21 hadi 24 ,Tukiweka Average ya mifuko 22 kwa mende hivyo itakulazimu kununua Mende 5.....Sio kila mchanga unafaa kwa tofali....Mchanga unatakiwa uwe laini kama mpana inabidi waumix na udongo kama ule wa kifusi.

Kukodisha mashine ni elfu 5 kwa siku na gharama za ufundi ni elfu 5 kwa mfuko, mafundi wakiwa watatu wanaweza kupiga mifuko 10 kwa siku, kwahiyo kwa idadi ya mifuko 107 wataimaliza kwa siku 11.

Gharama:-

1. Cement 16,000 x 107 = 1,712,000/=
2. Mchanga Mende 5 = 200,000 x 5 = 1,000,000/=
3. Gharama za mashine = 11 x 5,000/= 55,000/=
4. Gharama za ufundi = 5,000/= x 107 = 535,000/=

Kwakuwa utamwagilia mwenyewe na maji unayo uliyochimba bwawa(ya mvua) basi hatutajumlisha gharama zake.

Grand Total = 3,302,000/= Hapo utaokoa Tsh 1,500,000/= kama utanunua kwa @ Tsh 1000 kwa kila tofali hadi Site.
Mende ndio nini? Ufafanuzi
 
Mende ndio nini? Ufafanuzi
MENDE.png
 
1: Mfuko mmoja 42 ..tofali 40 (standard)
2: Mfuko mmoja fundi ni 6,000 (elfu sita)
3: Kwa siku fundi anapiga mifuko 10
4: Mchanga mende ni 220,000-240,000....mende mbili zinapiga tofali hizo na kubaki labda wasijaze vizuri
5: Tofali mchawi maji, power to you
Naombeni ujazo wa haya malori kwa anayejua tafadhali:
Mende, Mbaula, Faw, Fuso, Bajaji
 
Naombeni ujazo wa haya malori kwa anayejua tafadhali:
Mende, Mbaula, Faw, Fuso, Bajaji
Mende kuna yenye 17m3 na 20m3
FAW kuna yenye 20m3 na 15m3 ambazo ndio nyingi
Ila gari zote itategemea na ujazaji, wengine hawajazi kama ni mchanga unapungua na kama unafanya biashara ya tofali utapata shot kidogo
 
  • Thanks
Reactions: JMF
Kwa gari ya 4.7qm kila trip mifuko7, na kila mfuko unatoa tofali 40 za nchi5
Hivi mkuu tofali moja hutumia mchanga chepe ngapi na cement chepe ngapi? Au kwa kutumia vile vindoo vidogo unapima kiasi gani?
 
Hivi mkuu tofali moja hutumia mchanga chepe ngapi na cement chepe ngapi? Au kwa kutumia vile vindoo vidogo unapima kiasi gani?
Chukua 40tofali gawanya kwa 50kg utapata jibu.
Then pima chepe moja inabeba cement kilo ngapi.
Do the same kwa mchanga pia.
Maana mfuko mmoja(50kg) unatoa tofali 40 za 5'.
 
Duh hatari mfuko mmoja tofali 45...hilo tofali au mchanga
hapa hata mimi nimeshangaa na hiyo cement ya kutoa hizo tofauli 45 ni cement gani? maana hata 42.5 yenyewe ukitoa zaid ya tofali 35 tu ujue hizo tofali hata kuku akidonoa anaingia ndani.
 
Back
Top Bottom