Msaada kujua gharama ya kufyatua tofali 4,800

Mama Nehemiah

JF-Expert Member
Sep 9, 2018
240
433
Habari Wakuu.

Nahitaji tofali 4,800 kwa ajili ya kuweka fence ya ukuta wa nyumba, ili kupunguza gharama kidogo nimefikiria kukodisha mtu wa kufyatua kwenye site yangu. Sasa naomba anayefahamu anijuze;

1) Zitahitajika cement mifuko mingapi ili kutoa tofali 4,800
2) Mchanga kiasi gani?
3) Gharama kwa kila tofali kwa mtu ataefyatua
Kama Kuna gharama nyingine naomba mwenye uzoefu anijuze na tuone kama tunaweza fanya kazi pamoja

NB: Maji ninayo ya kutosha site.

Asanteni
 
Yes mkuu ndicho nilifikiria.kwangu kuokoa hata laki 5 tu nitashukuru

On a roughly but serious note:

Kwa hesabu ya tofali 45, kwa tofali 4800 utahitaji simenti mifuko takribani 110. Kwa bei ya 20,000/- kwa mfuko ni 2.2M.

Mchanga kila tripu ikupe tofali 200, utahitaji tripu 24... bei ya mfano ni 50,000/- kila hivyo itakula 1.2M.

Fundi wa kupiga tuseme utamlipa 150 hadi 200 kwa tofali, tuweke 800k.

Jumla kuu ni 2.2M+1.2M+800k = 4.2M.

Hapo bado maji, hatujui kama ni ya kulipia au niaje... na ishu ya kumwagilia hizo tofali sijui itakuwa kwako au kwa mpigaji!

Weka laki hapo ziada ihusishe huduma kama hizo.

Wakati huo, tofali zilizo tayari zinauzwa 1000 hadi 1200.... jumla 4.8M hadi 5.8M sijui kuhusu usafiri.

Piga hesabu utajua kiasi cha kuokoa hapo, na muda wako na usumbufu wa kusimamia na kuhakikisha kazi inafanyika kwa ubora.

Laki tano hadi milioni unaweza kuokoa.

Kumbuka mwaka huu sio wa kupata raha sana.
 
Ni vema tujifunze kufuata viwango (sisi sio wa kwanza kufyatua tofali, walishafyatuaga wenzetu huko miaka ya nyuma) ndio maana ikaonekana ni vema kuweka viwango katika kila kitu kinachofanyika, kwa mujibu wa Viwango(tukumbuke kila kitu kina kiwango chake kinachokubalika kimataifa, kikanda au hata kwa nchi), mfuko mmoja wa simenti unatakiwa kutoa tofali 25(hiki ndo kiwango kinachotumiwa na Serikali kwa sasa).

Hivyo, ukitoa tofali 25 -35 (kwa mfuko mmoja) ZITAKUWA IMARA, lakini tofali 45 kwa mfuko SISHAURI. Ukifyatua tofali mbovu bado hatuna teknolojia ya kurudisha mkanda nyuma Ili kuitumia sementi ileile kurekebisha makosa!!!!! Inakuwa hasara, labda uyatumie matofali hayo kama kifusi!
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom