Bill
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 8,290
- 8,512
Pamoja ni michango bora ya wahusika naongeza haya.Habari Wakuu.
Nahitaji tofali 4,800 kwa ajili ya kuweka fence ya ukuta wa nyumba,ili kupunguza gharama kidogo nimefikiria kukodisha mtu wa kufyatua kwenye site yangu.sasa naomba anayefahamu anijuze;
1)Zitahitajika cement mifuko mingapi ili kutoa tofali 4,800
2)Mchanga kiasi gani?
3)Gharama kwa kila tofali kwa mtu atayefwatua
Kama Kuna gharama nyingine naomba mwenye uzoefu anijuze na tuone kama tunaweza fanya kazi pamoja
NB:Maji ninayo ya kutosha site
Asanteni
Utapata tofali bora na imara ukilinganisha na za kununua. Wafanyabiashara wanatoa hadi tofali 60 kwa mfuko na wewe utatoa 45.
Angalia sana usimamizi wakati wa kufyatua mafundi wataiba cement hadi utachanganyikiwa na kukosa ubora na unafuu uliokusudia.
Hakikisha umwagiliaji mzuri ili kuzifanya imara zaidi.
Ni hayo tu.