Msaada kuhusu ulipaji kodi TRA

Msaada kuhusu ulipaji kodi TRA

Yelawolf49

Member
Joined
Sep 20, 2017
Posts
73
Reaction score
65
Wasalaam ndugu zangu.
Hali iliyonikuta ni kuwa nlikua na biashara ndogo nliachiwa uendeshwaji wake kwangu na shule ikawa changamoto ikafa nikahangaika na vitu vingine sasa nataka kufungua biashara mpya napata taarifa kwa watu kuwa itabidi nilipie kodi miaka 4 nlokua nimefunga ile biashara. Je ni kweli? Na hizo penalty zikoje maana nimeshindwa kwenda hata TRA.
Asanteni
 
Ukipata suluhisho uniambie ndugu. Mwaka jana sijalipa hata senti tano.
 
Ukipata suluhisho uniambie ndugu. Mwaka jana sijalipa hata senti tano.
Uko kwny category gani?mlipa Kodi mdogo(ambae anakadiriwa tu na hahitaji kupeleka returns Wala kuandaa mahesabu) au uko kwny category ya mlipa kodi mkubwa/Kati anayepeleka returns na kuandaa mahesabu)?
 
Mlipaji kodi mdogo. Makadirio ya mauzo yalikua chini ya 14M per year. Nilifunga biashara.
 
Wewe nenda TRA. Kalie njaa ili wakukadirie hata miezi 3 tu ya kulipa kama fidia, badala ya hiyo miaka 4 uliyofunga biashara.
 
Na Mara ya mwisho ulikua unalipia Kodi ya sh. Ngapi kwa mwaka/kila quarter ulikua unalipia sh.ngapi?
Kama 65,000/quarter. Biashara ilifunguliwa Jan 2021 ila kuna mambo yalitokea nikashindwa kuendelea nikawafuta kuwa nataka kufunga wakasema hadi Dec niandike barua na kulipa kodi yao.
 
Back
Top Bottom