Je, mfumo mpya wa TRA Efiling unaweza kuongeza wigo wa kodi?

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,497
5,533
Habari za wakti huu,

Kwanza nianze kwa kuwapongeza TRA Tanzania kwa mfumo wao mpya wa usimamizi wa masuala ya kodi.

Ni hatua nzuri hasa kutoka kwenye mfumo wa ukusanyaji wa kodi wa "Manual" na kisha kuhamia katika ule mfumo wao wa online uliokuwa very user unfriendly mpaka kwenye huu mfumo wao mpya ambao naona sasa umekuwa live mtandaoni.

Kama mwananchi mpenda mabadiliko nimeona nitoe maoni na nifanye uchambuzi kidogo kuhusu mfumo huu mpya wa TRA Tanzania na pia nichokoze mjadala wa kuujadili mfumo huu hapa nikiamini kwamba kwa kuujadili wengi watapata hamasa ya kuufahamu na kuutumia kwa ajili ya kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa.

1675747389943.png


Kabla ya kuanza mjadala nieleze wazi kabisa mimi ni average user kwa hivyo basi maoni na mtazamo wangu yachukuliwe hivyo.Tuendelee.

Kwanza nianze kwa kusema kwamba huu mfumo una maboresho makubwa ukilinganisha na mfumo wa awali uliokuwa unatumika miaka miwili ya nyuma hasa katika eneo la muonekana,huduma zinazopatikana,kasi,urahisi wa kutumia na upekee lakini niweke wazi mapema kwamba bado haujafikia katika kile kiwango kinachotakiwa cha kuwezesha kila mtu kulipa kodi halali na ya uhakika.

Kabla sijaendelea napenda nieleze kwa nini nasema kwamba mfumo haujafikia kiwango cha kuwezesha kila mtu kulipa kodi kwa kiwango kinachotakiwa na ni kwa nini bado huu mfumo hauleti hamasa ya kutaka kulipa kodi.

Tunafahamu kwamba kodi zipo za aina nyingi hapa nchini na zinatozwa kwa njia mbalimbali kama vile,VAT,PAYE,SDL,Mapato,TOZO,Majengo etc.

Sasa huu mfumo bado haujawezesha namna ya Mlipa kodi wa kutambua kwa uhakika kabisa analipa kodi kiasi gani katika kuchangia maendeleo ya nchi yake.

TRA Tanzania Mnapaswa kuwa na mfumo ambao unawezesha mlipa kodi kufahamu TOZO amelipa kiasi gani, VAT amelipa kiasi gani, PAYE amelipa kiasi gani,Mapato amelipa kiasi gani, na kodi na tozo zote ambazo zipo zionekana kwa namba ya mlipa kodi.

Hili linawezekana na lina faida kwani kwa kufanya hivyo mnaweza kuleta MFUMO wa TAX credits na TAX refunds kwa ajili ya kuongeza incentive ya watu kulipa kodi, kutoa risiti, kudai risiti na kutumia mifumo ya kielectronic kufanya malipo ambapo kwa pamoja itarahisisha gharama za kufanya biashara na kukusanya kodi na hata kuongeza makusanyo na uwjibikaji.

Haya ni maoni yangu kwa ujumla na nafikiri mnaweza kuyaweka katika development scope ya mfumo wenu ili kuborsha na kuhamasisha ulipaji wa kodi.

1675747263402.png


Sasa nianz kutoa maoni yangu kuhusu mfumo wenu mpya na maeneo ambayo nafikiri mnaweza kuboresha:
  1. Kwanza kabisa nianze na issue ya database connections,Nilicho observer ni kwamba bado mfumo wenu unatatizo la database connection time out hasa wakati wa kupakua taarifa mbalimbali.Hii ilikuwepo kwenye mfumowa zamani ila tofauti na sasa mfumo haukutoi nje(Automatic log out )bali unakwamakwama kwa muda. Nimepima lagging nimeona inafikia sekunde 3 had 7 na kwa mfumo ambao bado haujawa busy 3secs ni very significant.Mlitazame muangalie namna ya kulishughulikia.
  2. Eneo la Pili ni issue ya OTP naelewa umuhimu wake kiusalama ila nashauri OTP itumike tu wakatiwa kujisajili na wakati wa kureset password hakuna haja ya kutumia OTP kila mara mtu anapo login kwenye System
  3. Eneo la Tatu ni kwenye usajili wa TIN nimeona option iliyopo ni ya kutumia NIDA napendekeza Mruhusu Hata asiyekuwa na NIDA aweze kujisajili kwa sababu tunajua kwamba Utoaji na Upatikanaji wa NIDA bado ni TATIZO hapa nchini
  4. Eneo la nne ni kwa Upande wa hii menu yenu inayokuwa na maneno manage returns.Mimi nimeigundua kwa bahati tu maana ile video yenu ya mafunzo ni ndefu sidhani mtu aliyeko busy anaweza iangalia.
    1675746463230.png
    Nawashauri hii menu ama muiweke sehemu nyingine au muifanye ionekana kama Menu ambayo ni clickable.
  5. Eneo la tano ni eneo la main dashboar ambapo kuna taarifa muhimu za mlipa kodi kama unfiled returns,filed payment etc.Nashauri katika eneo hilo basi zile figures ziwe clickable na zimpeleke mlipa kodi kwenye list husika ili aifanyie kazi.Hakuna haja ya mtu kuanza kuzurura kwenye mfumokutafuta kitu ambacho unaweza kukiwekea tu shortcut
  6. Eneo la sita lugha.Kwani mkiweka na swahili Option kuna Ubaya gani?Au walipo kodi lazima wawe na PHD ya kiingereza?
  7. Eneo la saba ni kuhusu sheria za kodi.Kwa sababu huu ni mfumo mpya na mnataka uwe adopted as fast as possible basi mnaweza kufanya marekebisho yafuatayo:
    1. Kwanza angalieni namna ya kutoa digital tax amnesty kwa walipa kodi ambao ni dormant ili waingie mtandaoni kuupdate taarifa zao.Na pia angalieni namna ya kufutilia mbalimbali madeni ya kodi ambyo yana umri zaidi ya miaka kadhaa mfano 5-10 etc au hata 2 ili kuwapa watu nafasi ya kuanza na clean sheet
    2. Pili angalieni viwango au namna ya ukokotoaji wa zile penalty zenu ambazo nyingi watu huzipata kwa sababu ya changamoto za mifumo yenu au udhaifu wenu katika utoaji wa elimuya kodi
  8. Kuna maeneo mengi ambayo tunaweza fanyia maboresha na ninaamini kwamba wadau wengine kama wahasibu na wafanya biashara ambao wameutazama mfumo huu wanaweza kutoa maoni ya maboresho
Karibuni tuendelee na mjadala huu ambao naamini utakuwa na TIJA na maslahi kwetu sote.
 
Vile vile ili kurahisissha uwekaji wa taarifa za wafanyakazi napaendekeza kuwa na uwezdkano wa kufanya BULK updates ya Taarifa za wafanyakazi kwa ajili ya kukokotoa PAYE.

Vile kuwe na uwezekano wa mtu kufanya DATA EXPORT katika baadhi ya maeneo na ikiwezekana pia kwenye mfumo wa EFD kuwa na uwezekano wa mtu kutoa statements za efd
 
Sisi tunashindwa ku log in kwenye mfumo kwa sababu password inaonakana ni wrong lakini ili kupata password mpya inatakiwa otp itumwe kwenye namba iliyotumika wakati wa kusajili account kwenye mfumo wa zamani, tatizo ni kwamba namba iliyotumika kwa sasa haipo valid.Tafadhali naomba ufafanuzi
 
Sisi tunashindwa ku log in kwenye mfumo kwa sababu password inaonakana ni wrong lakini ili kupata password mpya inatakiwa otp itumwe kwenye namba iliyotumika wakati wa kusajili account kwenye mfumo wa zamani, tatizo ni kwamba namba iliyotumika kwa sasa haipo valid.Tafadhali naomba ufafanuzi
update namba ya simu unayotumia sasa hivi,utaulizwa maswali kuverify nida namba kisha utatumiwa details. TRA Tanzania wanaweza eleza zaidi.
 
Back
Top Bottom