DeepPond
JF-Expert Member
- Nov 18, 2017
- 40,454
- 99,086
Wakuu,
Kila kitu kilikua sawa mpk pale Mwezi 9 TRA walipopita kukagua mashine zao za efilling zinavofanya kazi na wakaelezwa khs usumbufu wa mashine zao za efilling kutoa mahesabu kwa wakati.
Ilipofika mwisho wa mwezi ripoti ya mwezi ikachelewa kutoka kwa Zaid ya siku kadhaa mbele,Ila Ilipotoka TU Kodi yao ikalipwa kwa wakati. Malalamiko ya ucheleweshaji huu wa ripoti walifikishiwa TRA na wao wakasema Haina shida endelea na KAZI watakuja kukagua shida nn. Ila hawakuja mpk mwezi ukaisha.
Ilipofika Mwezi wa 10 ripoti ya mwezi pia ikachelewa kutoka, ikabidi kuwafata wakasema itakua mfumo unasumbua, tuvute subira. Ripoti ilipotoka TU mda huo huo ikiwa mchakato wa kuilipa uko mbioni,Simu ikapigwa na TRA kufahamisha kua mfumo ushakaa sawa Kodi Yao ikalipwe.
Nimekwenda kulipia naambiwa kwenye mfumo kuna Deni la penalty ya ucheleweshaji kwa mwezi uliopita. Baada ya kuwafafanulia sana wakasema wameelewa niachane na hiyo penalty, nilipie TU kodi ya mwezi huu. Kodi yao ikalipwa vizuri tu.
Ilipofika Mwezi wa 11, kwa zaidi ya wiki 2 mashine ikawa inasumbua sana kutoa risiti. TRA walipotaarifiwa wakaja na kugusa gusa Kisha wakasema watarudi endelea kwanza kutoa huduma bila mashine tunalishughulikia, hawakurudi wakapotea mazima. Biashara ikaendelea bila mashine kutoa risiti.
Wamekuja kurudi wiki moja kabla mwezi haujaisha wakarekebisha na mashine ikaendelea kuchapa kazi mpk mwisho wa mwezi.
Mwisho wa mwezi umefika mashine ikawa haitoi mahesabu ya kodi. Baada ya kuwafata,wakasema nivute subira mfumo unalifanyia kazi, siku kadhaa mbele ripoti ikatoka na kodi Yao ikalipwa bila tatizo.
Mwezi wa 12 umefika mashine ikaanza kusumbua tena, TRA wameitwa wamegusa gusa Kisha wakasema watarudi,hawakurudi. Biashara ikawa inafanyika bila kutoa risiti. Ghafla unashangaa wanakuja kukukamata unauza mafuta bila kutoa risiti.
Unawaambia Mbona taarifa mnayo, wanasema barua iko wapi. unawaambia kua walikuja wenyewe wakaangalia wakasema watarudi,hawakutokea na barua hawakuacha. Wanakwambia ulifanya jitihada gani kuifatilia barua yako, Unabaki mdomo wazi maana walipokuacha hawakukawia taarifa kua inatakiwa barua.
Hujakaa sawa unaitwa na kukabidhiwa barua ya faini, unalalamika sana ila hakuna anaekusikiliza. Wanakwambia faini ni lazima kwanza ilipwe ndo mazungumzo mengine yataendelea tena ndani ya deadline ya siku chache sana walizo amua wao ukailipe kwa kutumia control namba uliyopewa, utajua mwenyewe pesa utapata wapi.
Unaamua kufatilia suala lako ngazi za juu uone watakusaidiaje maana faini Ni kubwa mno inakata mtaji, gafla unaskia na account zako zimezuiliwa, na sio account ya biashara ya mafuta TU, Bali Hadi account za binafs na za biashara nyngn zisizohusu mafuta nazo zimezuiliwa
Unawafata kuwauliza imekuaje Tena, wanakwambia umekaidi kulipa penaty uliyoandikiwa, pia una mlolongo wa kukaidi kulipa penalty kwa miezi ya nyuma. Wanaanza kukusomea Hadi zile penalty za ucheleweshaji wa mahesabu ya VAT ya mwisho wa mwezi Kwa miezi iliyopita waliyokuruhusu wao wenyewe uendelee na kazi.
Miezi ambayo wao wenyewe wanajua mashine zao ndo zilikua na shida ya mfumo na ulifuatilia Sana na walikupa majibu mepesi kua "Tunalifanyia kazi", na hata zile penalty baadhi ulisamehewa kwa mdomo, ila kumbe kwenye mfumo hawazikuondoa na Sasa wanazidai kwa Nguvu zote.
Yaan imefikia hatua pesa yao ya Kodi unayo ila namna ya kuwalipa inashindikana kwasababu ya mfumo wao mbovu wa efilling hautoi mahesabu kwa wakati.
Hivi hii nchi namna hii inaelekea wapi? Inafikia hatua mpk unaingiwa na mawazo mabaya kwamba Huenda mfumo wa efilling unahujumiwa kusudi ili mradi Watu wapigwe penalty za lazima pesa ipatikane.
Najua mawaziri, wabunge na Viongozi mbalimbali wa serikali wamo humu jf, plz Naombeni mlishughulikie hili bila kuangalia ni Nani kalalamika.
Sio vizur kushughulikia matatizo ya watu maarufu TU kisa wamepeleka malalamiko Yao kwenye media, ndo wanaitwa in person kwenye meza ya majadiliano.
Wajasiliamali wengi TU uku kwenye mafuta tunateseka sana hasa mwezi huu decemba na malalamiko yetu mengi tumeyafikisha Sana TRA ila hayasikilizwi Wala hatuitwi meza ya majadiliano. Tunaambiwa TU straght tulipe faini Ndo majadiliano yataendelea.
Serikali mnachotaka Nini, au mnataka mskie Watu wamejinyonga na kufa kisa wamefilisika. Maana kushikilia account za mtu Hadi zisizohusu mafuta Ni kutengeneza frustration Hadi kwenye biashara nyingine na kwenye mabenki tuna madeni lukuki, mikopo inasubiri marejesho.
Naombeni serikali mtambue kuwa kwenye mafuta Hakuna anayekwepa kulipa Kodi yenu , tatizo mazingira mliyoweka ya ulipaji Kodi yanatukwamisha Sana wajasiliamali.
NAWASILISHA tafadhali.