Msaada kuhusu mfumo mpya wa Insurance ya Gari

xox

JF-Expert Member
Sep 23, 2018
1,398
6,507
Habari waungwana,

Kuuliza sio ujinga, nilikuwa naomba kujua kuhusu huu mfumo mpya wa Insurance za magari wa kutokuwa na sticker za kubandika kwenye kioo.
Je, inapaswa utembee na cover note kama ithibati kuwa Insurance yako ni hai. Hofu yangu ni hawa ma traffic wetu wanaweza kukamata na akakwambia kuwa hana mashine ama smart phone ya kuhakiki uhai wa bima yako.

Natanguliza shukran zangu za dhati na kama unahisi ulikuwa unajua kabla na huna nia ya kutoa jibu basi jaribu pia kuto toa maneno ya dhihaka maana si kila mtu anajua.
 
Hauna haja ya kutembea na covernote,japo kwa kuwa huu mfumo ni wa kidijitali basi unakuwa na uthibitisho katika simu yako na unakuwa salama.

Lakini pia kama gari hiyo mnatumia mtu zaidi ya mmoja nenda print certificate ile ya kielektroniki uiweke kwenye droo ya gari kama unavotembea na kadi ya gari tu.

Trafiki atakayeleta nongwa hapo bila kuwa na mashine kuhakiki hilo siyo kosa lako ni lake.
 
shukran sana
 
hapana, traffic akichukua namba za gari tu na kuweka kwenye mashine inaonesha kama umelipa au la

ila jitahidi kukumbuka umenunua lini?, coz sasa hivi ni ngumu kukumbuka umenunua lini , hamna kikumbushio cha stika mbele ya kioo
 
Online tunaangalizia kwa address ipi? Wekeni link ya kuangalizia online
 
hapana, traffic akichukua namba za gari tu na kuweka kwenye mashine inaonesha kama umelipa au la

ila jitahidi kukumbuka umenunua lini?, coz sasa hivi ni ngumu kukumbuka umenunua lini , hamna kikumbushio cha stika mbele ya kioo
Kuna utaratibu wa kupigiwa simu ya ukumbusho na kampuni ya bima tarehe ya mwisho inapokaribia, japo sina uhakika kama makampuni yote yanafanya hivyo.
 
Nina gari mbili, moja nimeikatia crdb nyingine BUMACO, zote mbili hazioneshi. Nimepigwa au ni hii system mbovu?
Kampuni ya bima uliyokata ndiyo inaweza kuwa changamoto,labda bado hawajaziweka kwenye database..

Bima Pap ya Milembe iko poa zaidi..
 
Nina gari mbili, moja nimeikatia crdb nyingine BUMACO, zote mbili hazioneshi. Nimepigwa au ni hii system mbovu?
Haujapigwa, kampuni huwa wanamchezo wa kutopeleka taarifa za insurance ya gari zako kwa wakati sahihi kwenye mfumo wa TIRA.
 
Ili mradi umeweza kuingia JF, naamini unayo simu inayoweza kutunza picha ya covernote, mi nilimuonyesha mmoja kwa simu, akacheki akaniruhusu niende.
 
Hauna haja ya kutembea na covernote,japo kwa kuwa huu mfumo ni wa kidijitali basi unakuwa na uthibitisho katika simu yako na unakuwa salama.

Lakini pia kama gari hiyo mnatumia mtu zaidi ya mmoja nenda print certificate ile ya kielektroniki uiweke kwenye droo ya gari kama unavotembea na kadi ya gari tu.

Trafiki atakayeleta nongwa hapo bila kuwa na mashine kuhakiki hilo siyo kosa lako ni lake.
Hakika...
 
Back
Top Bottom