Msaada kuhusu kubadilisha jina

Msaada kuhusu kubadilisha jina

Mr Beach Boy

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2021
Posts
1,702
Reaction score
5,115
Wakuu habari nipo kwenye harakati za kubadilisha jina wa Sababu binafsi.

Nilienda kwa advocate akasema anaandaa deed pool kwa 50k then after nipeleke wizarani nitalipia 32500/=

Sasa Kuna mtu amenishauri niende mahakamani niwe nimejaza Ile deed pool gharama haitazidi 15k

Naombeni ushauri wenu ni kweli nikienda mahakamani gharama zitapungua tofauti na kwa advocate?

"Ignorance of the law is not a defence"
 
Inachukua muda gani kuweza kuruhusiwa kuanza kulitumia jina jipya mara baada ya kujaza deed pol?
Ukishajaza hiyo deed poll 3copies na ubandike picha yako, weka viambatanisho vya majina peleka kwa msajili wa nyaraka/ ofisi ya usajili wa ardhi iliyokaribu yako ikasajiliwe bila usajili hiyo deed poll haijakamilika.Gharama za usajili 32500
 
Naomba nikusumbue kidogo kama hutojali!
1. Inasemekana kuna kipengele cha tangazo kwenye gazeti la Serikali, hilo linafanyika wakati gani? Baada ya kujaza deed poll au baada ya kufanya usajili kwenye ofisi ya usajili wa ardhi?

2. Gharama ya kutoa tangazo kwenye gazeti la Serikali inabebwa na nani? La inalilpiwa, ni shilingi ngapi?
 
Kwenye tangazo ni baada ya usajili na gharama ni zako.
 
Kwenye tangazo ni baada ya usajili na gharama ni zako.
Usinikasirikie tafadhali!
1.Tangazo linawekwa gazetini baada ya muda gani?
2. Gharama yake ni kama shilingi ngapi?
3. Wakati ukisubiria tangazo kutolewa gazetini utakuwa ukilitumia jina lipi, jipya au la zamani?
 
Tangazo month
20,000-30,000 gazeti la serikali na mwanachi pia. If told
Jina la zamani utalitumia mpaka hukumu itoke.
 
Tangazo month
20,000-30,000 gazeti la serikali na mwanachi pia. If told
Jina la zamani utalitumia mpaka hukumu itoke.
Umeniacha kidogo mkuu hapo kwenye hukumu!

Hukumu inatolewa wapi? Nani mtoa hukumu?
 
Unaruhusiwa kuanza kulitumia anytime baada ya kukamilisha mchakato .
Bado sijaelewa Dr! Mchakato katika hatua ipi?
1. Kujaza deed poll?
2. Tangazo kutoka gazetini?
3. Usajili katika ofisi ya ardhi?
4. Hatua zote kuanzia 1 hadi 3?
 
Ukishajaza hiyo deed poll 3copies na ubandike picha yako, weka viambatanisho vya majina peleka kwa msajili wa nyaraka/ ofisi ya usajili wa ardhi iliyokaribu yako ikasajiliwe bila usajili hiyo deed poll haijakamilika.Gharama za usajili 32500
Samahani kidogo naomba kujuzwa zaidi, je kama ni muajiriwa serikalini ukibadilisha majina haitaweka matatani ajira yangu baada ya kuanza kutumia jina jipya?
Pili inawezekana kubadilisha majina yote matatu na isilete shida?
 
Labda nichangie kidogo,mimi nilikuwa nashida ya kubadilisha taarifa zangu mwaka wa kuzaliwa unatofautiana na uliopo kwenye kitambulisho cha NIDA.

Nilipewa muda mfupi na muajili wangu kurekebisha taarifa zangu za NIDA ili zifanane na za kiutumishi kwani ndoo zilikuwa taarifa sahihi. Nilianzia kwa advocate akala 30,000 then nikaenda kusajili kwa msajili wa viapo akala 32500.

Baada ya hapo nikaenda kwenye ofisi za gazeti la serikali nikalipa 15,000 then nikaambiwa niende posta nikaituma Dodoma kwa sh 15000. Kisha nikapewa no ya kuwa siliana na mtu wa huko baada ya siku3 kutuma,kisha huyo mtu akasema tangazo lako litakuwemo tarehe 1/8 wakati huo ilikuwa katikati mwa mwezi wa 5.

Baada ya hapo mwezi wa nane ukafika walikuja kuingiza tangazo la tarehe 1 baada ya wiki 2 ndoo nakuja kujiona kwenye gazeti hilo la serikali..Hapa kilichobaki kwangu ni kupata barua ya katibu mkuu utumishi ili NIDA waipate niweze kubadilisha taarifa zangu.Nadhani umeona huo mlolongo ulivyo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom