Msaada kuhusu kuanzisha biashara ya matunda na mboga mboga! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada kuhusu kuanzisha biashara ya matunda na mboga mboga!

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by CHAI CHUNGU, Apr 11, 2012.

 1. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,165
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Habari wana jf.
  Poleni kwa majukumu ya kila siku.
  Najitokeza kwenu ninyi kuomba mchanganua wa mawazo.
  Ndugu yenu nina plani kuanzisha biashara ya mbogamboga na matunda,lengo langu ni kufungua duka hapa hapa Dar.
  Ila uzalishaji wa bidhaa nimeplani kuweka Arusha.
  Tayari nina mtaji wa kutosha ingawa juu ya biashara hii nimepanga kuweka mtaji wa kati ya tsh30,000,000-tsh50,000,000.
  Naomba nieleweke,hapa nahitaji mawazo kujua kama biashara hii italipa,na wapi niweke hilo duka,ikiwezekana hata nijue bei ya fungu 1 la mboga naweza uzaje kutegemea na ubora wa mboga zangu(very high quality)
  ,ninauhakika wa kuzalisha mboga yenye ubora wa 90-100% na isiyotumia kemikali ya aina yoyote.
  Kuhusu matunda ntakua nayakusanya kwa wakulima vijijini na kuyapanga katika gredi stahiki.

  Kwa hayo machache nategemea ushauri wenye tija.

  Naomba kuwakilisha wakuu:
   
 2. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,165
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Pia ningependa kufahamu na gharama za pango la duka kutegemea na saizi au ukubwa wa duka na eneo lilipo.
  Pia gharama za leseni na vibali,wafanyakazi.
   
 3. Chasha Poultry Farm

  Chasha Poultry Farm Verified User

  #3
  Apr 11, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 5,274
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  MKUU KUHUSU BIASHARA YA MBOGA NI NZURI SANA BUTI LAZIMA UWE UMEJIPANGA VYA KUTOSHA,

  1. Kama utazalishia arusha na kuuza Dar ni lazima uwe na magari ya freezer au usafirishe kwa ndege make kwa sem trela mboga ziatozea njiani

  2. Kuhusu Duka Yapu unaweza kuwa na Duka lako mithili ya Supermarket ila ni lazima liwe kubwa na liwe location nzuri na ni lazima uwalenge watu fulani au kundi fulani

  3. Kuhusu bei mimi si dhani kuna haja tena ya kupanga mafungu mkuu hapa unatakiwa kuzi park kwenye mifuko maalumu kabisa  4. Kuhusu kununua matunda kwa wakulima na kuya grade hapo itakuwa ngumu mkuu, kama umedhailia kuzalisha bila kutumia chemical hayo matunda ya kutoka kwa watu wengine si yatakua yamezalishwa na chemical?

  5. Na nakushauri kwa kuanza usauply kwenye supermarket then ukipata mtaji wa kutosha fungua supermarket yako itakayo kuwa inauza mboga na matunda labuda na vyakula vingine tu

  MKUU HAYO YA LESENI NAKUSHAURI UWAONE WAHUSIKA MAKE ZINATOLEWA BILA MALIPO
   
 4. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #4
  Apr 11, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,165
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Nimekuelewa mkuu.
  Ofcourse duka linatakiwa kua kumbwa mithili ya supermarket,kuhusu bei nadhani ntafanya kama ulivyonishauri regarding to use good parking kwenye mifuko,hapa nadhani itanibidi nipeleke special order kiwandani kwa ajiri ya kuprint mifuko yenye nembo yangu.About capital kama nilivyosema ninampango wa ku-invest about 30mil-50mil.
  Pale maeneo ya sinza vipi mkuu?
  Panafaa kwa biashara hii?
   
 5. Chasha Poultry Farm

  Chasha Poultry Farm Verified User

  #5
  Apr 11, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 5,274
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  niko ARUSHA MKUU, UNATAKIWA KUWA NA VITU KAMA HIVI
  [​IMG]

  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]
   
 6. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #6
  Apr 11, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,165
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Ahsante sana mkuu,M/mungu akubaliki kwa wema wako.
  Sasa parking hii inabidi ntafute japo mtaalamu 1 wa mambo ya parking,jee tanzania tunao watu wenye sifa za parking ya namna hii?na hii kamuni ipo hapa tz au nje ya tz?
   
 7. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #7
  Apr 11, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,165
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Mkuu malila naomba unisaidie juu ya hili kaka!!!!!
   
 8. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #8
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,165
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  hii hapa mkuu malila!
   
 9. M

  Malila JF-Expert Member

  #9
  Apr 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,262
  Likes Received: 452
  Trophy Points: 180
  Kwa sababu unalenga soko la Dar, bora upate kipande cha shamba huku huku Dar. Nitakuibia siri kidogo ya hiyo biashara ya mboga na matunda. Nenda pale St.Joseph siku ya jumamosi asubuhi na mapema, kaa pale uone nini kinatokea. Kuna Masister fulani wanalima mboga Mkuranga na wanalima organically, hiyo mboga huuzwa mara mbili kwa week, inagombaniwa sana.

  Kwa nini nimesema uwe na shamba karibu na soko lako, kwa sababu mteja mwingine atataka kutembelea shambani ili aone kwa macho kuhakikisha ubora wa mboga/matunda yako. Pili wewe mwenyewe itakuwa rahisi kudhibiti uchakachuaji.

  Nenda Kisutu, ukaone aina za mboga wanazopenda Wahindi, kisha piga kwata mahotelin ili ujue mboga zao wanapata wapi, washawishi kwamba unaweza kuwapa mboga mfululizo.

  Moja ya vitu ninavyoweza kukusaidia ni shamba la kuanzia kama utataka kulimia mboga/Matunda kwa hapa Mkuranga. Lina maji ya kutosha, kuna nyumba,linafikika na gari. Manpower juu yako. Matikiti, pilipili na mboga zingine zinamea vizuri. Pampu ya maji ni muhimu ili uweze kulima eneo kubwa.

  Nakubaliana na mtoa mchango mmoja hapo juu aliyesema, inabidi uwe na kundi maalumu la kuuza mboga zako kwa kuanzia ili baadae uweze kupanuka.

  Sinza/Mwenge/tegeta/Morocco/Kinondoni/Msasani ni maeneo mwafaka kwa biashara yako. Suala la gharama za frem sio rahisi kujua.Usisahau kulima paprica, zina soko nje ya nchi.
   
 10. SYENDEKE

  SYENDEKE Senior Member

  #10
  Apr 12, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kaka nipe abc ya hii parking where we can get i like it niko seriuos for real
   
 11. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #11
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,165
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Ahsante sana mkuu.
  Ngoja nifanye mchakato.
  So hapo mkuranga ntapata eneo la kutosha?kuhusu matunda ntaanza kwa kukusanya kwa wakulima,but mboga mboga ntalima mwenyewe!
   
 12. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #12
  Apr 12, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  nchi za wenzetu kuna options mbili za packaging 1. kama hiyo ya komandoo (kwa watakaopenda) 2. mteja anachagua anachokitaka anaweka kwenye mfuko halafu anakwenda kupima uzito then anabandikiwa price label (hii ni nzuri c'se mteja anachagua nyanya, kitunguu etc quantity anayoitaka kama gengeni) unatakiwa uweke mifuko mingi tu. Na wewe unatakiwa kuwa na options hizo mbili, hauhitaji complications za kuwa na packaging experts.
  Kumbuka kuweka mizani ili uuze bidhaa kwa uzito na uende kisasa.. weka bei ya gram moja kwa kila bidhaa eg gram 1 ya nyanya tsh 10, 1 gm ya mchicha tsh 20 etc. Price labels zionekane kabla mteja hajanunua
   
 13. M

  Malila JF-Expert Member

  #13
  Apr 13, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,262
  Likes Received: 452
  Trophy Points: 180
  Utapata, unataka eka ngapi mkuu? Na kama unataka la kununua sema, ili ununue kando ya kijito.
   
 14. queenkami

  queenkami JF-Expert Member

  #14
  Apr 13, 2012
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  mkuu nakukubali sana kwenye kilimo,unasaidia sana kwa maelezo yako.
   
 15. fmlyimo

  fmlyimo Senior Member

  #15
  Jun 1, 2013
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 197
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu project inaendeleaje?
   
 16. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #16
  Jun 1, 2013
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,320
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Weka feedback mkuu
   
 17. MASAMILA

  MASAMILA JF-Expert Member

  #17
  Mar 18, 2016
  Joined: Jun 22, 2014
  Messages: 468
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 60
  MTOA MADA TUNAOMBA UWEKE FEEDBACK.
   
 18. Macky

  Macky Member

  #18
  Mar 22, 2016
  Joined: Mar 8, 2016
  Messages: 48
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 25
 19. S

  Shamim abas Member

  #19
  Nov 5, 2016
  Joined: Aug 13, 2016
  Messages: 11
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Mi nipo Dodoma natak kufanya biashara hii nifanyeje?
   
Loading...