Msaada kuhusu cheque kutoka nje ya nchi na kuidepost hapa nchini

konda msafi

JF-Expert Member
Sep 5, 2018
1,666
8,588
Habari zenu wakuu.

Kwa wale wenye uelewa wa hili naomba mnifahamishe kama inawezekana.

Kuna hela kutoka Canada natakiwa nitumiwe. Mtumaji amejaribu kunitumia kupitia bank account yangu hapa nchini.

Hela kaituma toka tarehe 10, siku ya Jumanne lakini hela haikuweza kufika kwenye account yangu mpaka imerudi tena kwakwe.

Ameniambia "inaonekana kwa sasa Tanzania kuna matatizo sana kumtumia hela mtu". Jana na juzi nilienda bank kuwauliza shida ni nini, mbona hela imetumwa lakini hainifikii?

Majibu yao wanasema hakuna shida yoyote, Ila mimi nadhani kuna shida sehemu, huenda labda serikali imeweka masharti flani flani kuhusu kutumiwa hela kutoka overseas.

Mtumaji amesema option aliyonayo ni kuniandikia cheque na kuituma kwa njia ya air mail. Swali langu ni hili "Je inawezekana ku-deposit cheque kutoka nje ya nchi hapa nchini?"

Natanguliza shukrani zangu.
 
Sina hakika sana na hili,ila nimewahi kusikia kuwa kwasasa kuna changamoto mno katika utumaji wa fedha kulingana na kiwango cha pesa kutoka nchi za nje kuja Tanzania(haswa katika benki na njia za kieletroniki i.e Paypal).

Ila nafikiri ni vyema ukafuatilia ujue kwa kina ni nini haswa kinaleta shida au utumie njia zisizo na changamoto (ukiachana na benki unayotumia i.e nenda BOA(WESTERN UNION) uone ni namna gani wanaweza kukusaidia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu wakuu.

Kwa wale wenye uelewa wa hili naomba mnifahamishe kama inawezekana.

Kuna hela kutoka Canada natakiwa nitumiwe. Mtumaji amejaribu kunitumia kupitia bank account yangu hapa nchini.

Hela kaituma toka tarehe 10, siku ya Jumanne lakini hela haikuweza kufika kwenye account yangu mpaka imerudi tena kwakwe.

Ameniambia "inaonekana kwa sasa Tanzania kuna matatizo sana kumtumia hela mtu". Jana na juzi nilienda bank kuwauliza shida ni nini, mbona hela imetumwa lakini hainifikii?

Majibu yao wanasema hakuna shida yoyote, Ila mimi nadhani kuna shida sehemu, huenda labda serikali imeweka masharti flani flani kuhusu kutumiwa hela kutoka overseas.

Mtumaji amesema option aliyonayo ni kuniandikia cheque na kuituma kwa njia ya air mail. Swali langu ni hili "Je inawezekana ku-deposit cheque kutoka nje ya nchi hapa nchini?"

Natanguliza shukrani zangu.
Ni fedha nyingi kiasi gani mpaka zilete shida namna hiyo? Mbona utumaji wa fedha kwenda Tanzania ni rahisi sana? Mwambie atumie WorldRemit na unaweza kuchagua hata fedha ziingie kwenye Mpesa au TigoPesa kwenye simu yako.

Kwa taarifa yako kutuma fedha Tanzania hakuna shida yoyote na watu wanatuma kila siku. Niambie ni fedha nyingi sana labda. Na fedha zilirudi huenda alikosea namna ya kutuma.
 
Watz tumezidi ujuaji. Katika waliomjibu hakuna hata mmoja aliyejibu kama mleta mada alivyouliza. Hajataka options, ila kasema utaratibu wa kutumiwa cheque toka nje na kuchukua cash kwa local bank kama upo uwezekano. Ndio maana tunafail mitihani kwa kujibu mbadala wa jibu halisi.
 
Babu tatizo letu kila mtu ni mjuaji.
 
Kabisa mkuu. Watu hawajibu swali bali wanajibu kile wanachodhani napenda kukisikia.
 
Nnachokijua mimi ukilipwa cheque unaipeleka kwenye bank yako kwa ajili ya kudeposite. Ukisha deposite bank yako itaipeleka ile cheque kwenye bank ya anayekulipa ili wakaangalie kama anayekulipa ana salio na wanaisign na then kuirudisha kwenye bank yako then bank yako ndo inakudumbukizia mpunga kwenye account yako.
Sasa kama hiyo bank ya mlipaji iko abdroad naona kama kuna kaugumu hapo. Labda kama atakuandikia bankers cheque
 
Babu tatizo letu kila mtu ni mjuaji.
Noma mzee wangu. Hivi kama hujui kitu si unapiga kimya kwani kuna haja gani ya kujaza thread zisizo na majibu kwa swali husika. Kila mtu anataka kujifanya anajua huwa anatumiwa pesa kutoka abroad. Swali la mleta mada la msingi sana nami nikajua nitajifunza kitu. Lakini majibu yote ni blah blah tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom