Msaada katika hili

Msaada katika hili

donlucchese

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2011
Posts
17,258
Reaction score
22,139
Wakuu,

Naomba msaada kufanya verification of address kwenye Skrill account.

Mimi ni mtumiaji wa Skrill, na awali nilikua nafanya miamala vizuri tu bila shida yoyote.

Imefikia stage ya kufanya verification of iD nikafanya bila shida, balaa limekuja kwenye proof of address.

Yaani kila document ninayoupload inakua rejected. Nimeenda mpaka bank wakaniprintia bank statement nikaiupload lakini wapi, mkuu mmoja akanishauri nitengeneze affidavit ya proof of address, nikatengeneza nika-upload still tatizo. Mpaka sasa sijafanikiwa chochote na kuna visenti vyangu humo nina shida ya kuvitoa. Naomba msaada kwa ambaye amewahi kuexperience changamoto kama hii nakuipatia ufumbuzi. Natanguliza shukrani zangu za dhati [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
IMG_20220428_123922.jpg
 
Kwani hao Skrill hawana mahali pa maswali na majibu..?

Waulize na uwatolee shida yako ujue wanataka nini na hawataki nini au unawaogopa..😂
 
Mkuu ungewasiliana nao labda wanaweza kukuambia Tatizo lipo wapi.

Ila haya mambo ya Adress yanatakiwa ya match, mfano unakuta Credit card yako inaonesha mwananyamala na wewe unajaribu Kuverify kutumia Adress ya Sinza ujue italeta Confilct.

Mfano hapo point ya mwisho kwenye adress wameandika kabisa proof of identity ya adress uliotumia kufungulia Skrill account, unakumbuka uliweka Adress gani?
 
Naomba mfano mkuu
Ni matumaini yangu lengo lako sio kuitumia Upwork kama mbadala wa Payoneer iliyoathiriwa na balaa la WireCard manake sidhani kama Skrill imesharudishwa Upwork baada ya biashara kati yao kufa 3+ years ago. Lakini kama kwa shughuli nyingine, ofcoz Skrill wasumbufu sana ku-approve docs manake nakumbuka kwangu hadi ku-approve ilikuwa mbinde kweli kweli. Kama bado hujafanikiwa, nenda benki ukawasimamie wa-edit anwani yako ili include location.

Kwa mfano, kama address yako ni: Nafaka bin Kunde
P.O. Box 4587,
Dar es salaam
Unachotakiwa kufanya, ingia hapa ili upate postcode ya eneo lako. Sasa assume unaishi Magomeni, Mtaa wa Suna ambao postcode yako ni 14101, na nyumba unayoishi ni #12, waambie benki wa-edit anuani ili iwe kama ifuatavyo:-
Nafaka bin Kunde
Magomeni Suna Street, #12
P.O. Box 4587
DSM1401

Dar es salaam.

Kwa upande mwingine, utakavyojaza address kwenye Skrill Form,
Address #1 weka hiyo Magomeni Suna Street, #12
Address #2 Andika Box #

Ukiangalia hii screenshot ya Fomu ya CRDB(assuming banker wako ni CRDB), utaona format yake ipo tofauti lakini itabidi waandike hivyo kwenye sytem, at least kwa muda ili hatimae uweze kupata bank statement yenye hiyo address format hapo juu. Kwavile hiyo staili yao, na inawezekana hawafahamu address formats za wenzetu zipo vipi, itakuwa vizuri sana ukifika tawini cha kwanza chukua fomu ya kufungulia akaunti kisha ijaze hayo menzo niliyojaza hapa chini kisha address waliyoandika wao kwenye system, wai-edit na ifanane kama utakavyokuwa umeandika.

View attachment 1492920
Hizo sehemu nyingine unaweza kujaza lakini kama format ya statement za CRDB hazijabadilika, hizo sehemu hata ukijaza hazitatokea kwenye statement kwahiyo hazitaathiri format wanayoitaka Skrill. Seehemu nyingine unayoweza ku-edit address ni kwenye utility bills, lakini huko mziki wake unaweza kuwa mkubwa ukilinganisha na benki.
fuata huo mwongozo nime quote kwenye uzi flani, pia ubadilishe adress kwenye account ya skrill
 
Wakuu,

Naomba msaada kufanya verification of address kwenye Skrill account.

Mimi ni mtumiaji wa Skrill, na awali nilikua nafanya miamala vizuri tu bila shida yoyote.

Imefikia stage ya kufanya verification of iD nikafanya bila shida, balaa limekuja kwenye proof of address.

Yaani kila document ninayoupload inakua rejected. Nimeenda mpaka bank wakaniprintia bank statement nikaiupload lakini wapi, mkuu mmoja akanishauri nitengeneze affidavit ya proof of address, nikatengeneza nika-upload still tatizo. Mpaka sasa sijafanikiwa chochote na kuna visenti vyangu humo nina shida ya kuvitoa. Naomba msaada kwa ambaye amewahi kuexperience changamoto kama hii nakuipatia ufumbuzi. Natanguliza shukrani zangu za dhati [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]View attachment 2203634
Weka address yenye mpaka street name na nambari, na house number. Wanataka physical address. So chuku hata bank statement edit weka
 
Back
Top Bottom