KWANZA NAKUOMBA MUNGU NIEPUSHE NA MWANAMKE WA HIVI HATA KWENYE KIZAZI CHANGU

.
Kuna mtu hapo juu kakuambia ukweli ukasema amejibu kwa hisia sio ushauli tho hata wewe unambeba uyo kakako kwa hisia sio uhalisia.
Najaribu kuwaza kama mnawatoto humo ndani sijui mnatengeneza kizaz cha haina gani hasa kwa watoto wa kiume!.
Dada hakuna maamuzi utaweza fanya daima kwa kutotaka kuonekana mbaya, otherwize unaenda kua kwenye kundi la WANAFIKI.
Pia nachokiona upotayari kuambiwa vile ambavyo ushajishauri tiyari ila hauko tayari kushauriwa.
Kwa maana iyo leo na kesho mumeo asipokuwepo(mungu aepushe) means ukitaka kumtoa kaka yako akalialia kua ndo malipo unayomlipa hayo then utakubali kubeba iyo character yake maana usidanganye watu CHARACTER ndo imebeba wasifu wote wa mtu.
Kama kaka anakupa ugumu ivo ni vipi kesho watoto wako uliowazaa/utaowazaa wakikua na baba akawa hayupo wakanza tabia kama za mjomba wao utaweza kiwamanage? Utawakatazaje na leo hii wanaona haya, je wakija mdugu wa mume wakaiga utaweza kuwamanage? Je utalaumu?
Mi naona bado mentally unautoto haujawa matured enough kua mama na kiongozi msaidizi wa familia, wamekupa JOHO kabla hujagraduate, hata uyo kaka yako bado kijana tuu ila unampa heshima na ukubwa asio kua nao. Daima huwezi kumlea mtu mzima, huwezi kulipa fadhira kwa kukumbatia ujinga, maana hata yeye hawez kukulipa unavyombeba leo kwenye nyumba yake. Hatulipani mema kwa kutukuza maovu, tunalipana mema kwa wema, Kwanini unashidwa kuusema KWELI juu batiri kisa huonekane mzuri! huo ni UNAFIKI daraja la kwanza. Kila kitu kinamipaka na mtu akishavuka mipata lazima apokee matokeo.
Ok mi ushauri wangu ni kua kwanza msimfukuze tho najua hamuwezi/mtashidwa. Inabidi kwanza huende kwa viongozi sahihi wa dini yako wakumentol, ukiwakosa nambie nitakudirect, wakufundishe kujielewa position yako ya kua mke wa mtu na namna ya kulinda heshima ya mumewako nyumba yako na familia yako in general kama mke/mwanamke.
Sababu tatzo haliko kwa kaka yako, tatizo lipo kwako. We ukishajitambua vizuri bas utaweza kuishi na watu vizuri na zaidi ukimtanguliza mungu.
JARIBU KUA MTU BORA NA SIO KUA MTU MZURI.
(AN-NISAAI-5)
Wala msiwape wasio na akili mali yenu ambayo Mwenyezi Mungu ameyajaalia yawe ni kiamu yenu.
YOHANA 2:12-
“..kawakuta mle hekaluni watu wakiuza ng'ombe, kondoo na njiwa, na wavunja fedha walikuwa wamekaa kwenye meza zao. Akatengeneza mjeledi wa kamba, akawafukuza wote nje ya hekalu pamoja na kondoo na ng'ombe wao, akazitawanya sarafu za wenye kuvunja fedha na kupindua meza zao. Akawaambia wale waliokuwa wanauza njiwa, “Ondoeni vitu hivi hapa. Msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa soko!”.