Msaada juu ya kaka yangu, nifanyeje?

Nahirat

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
597
984
Mi nimeolewa miaka miwili iliopita lakini kutokana kutafta maisha mme wangu anaishi nchi za nje kutafta maisha nakweli mungu mwena tunaendelea vyema pamoja kwamba hayuko hapa.

Alimchukuaga kakaangu kamtaftia kazi huko kakaangu kutokana natabia yake nakujingiza katika kazi flani akawa deported

Kutokana kwamba nimtu wastarehe sana hela aliokua nayo ilivyoisha tukakubalina pamoja na mme wangu aje tuishi pamoja hapa Arusha maana hakuna watu wengi sana nyumbani.
Sasa kilichonifanya niandike hii post kakaangu anabadilisha wasichana mpaka naogopa kila siku lazima alete mwanamke napia alishawahi kumleta sister hadi.

Kwaupande wangu naumia jinsi anavyo chezea watoto wawatu wengine wanakua namatumaini kwamba atawaoa kumbe hana huu mpango. Ambao tumezoweana kwa haraka wananipigia cm wakilia juu yake wala hata yy hana habari
Namweshim sana maana he is over 35 kwahyo amenizidi ka miaka 10. Natafta jinsi yakuongea nae nashindwa
Naomba mnisaidie nifanyeje aweze kuwa na msichana moja tu basi hata wawili sio kukutana kwenye corridor na sura mpya kila cku.

Lakini pia tangu j. Mosi iliopita alileta mwanamke moja nimkubwa kama mamayetu kama 45-50 alafu cjawahi kuona akika na mwanamke mda mrefu hivo amejichubua vibaya sema mstarabu alafu anjituma sana jikoni. Pili huyu mama msafi sana pamoja kwamba ni mnene ila anajitahidi kazi hapa napale Sasa naona kakaangu kafika kwamara yakwanza naona akitoka kazini kuwahi nyumbani kumchukua bibie nakwenda Mjini kupooza koo. Sina shida nahuyu mama sema mamaangu mwezi wa10 anakuja nyumbani nahuyu mama naona ndo kafika hadi naona anazungmzia kuweka banda lakuku.

Ebu naomba mnishauri jinsi yakumwambia either aondokena huyu mamaake mlezi maana yetu nae sio habba atokubali kwa jinsi navyo mjua mama pia ana pressure, au huyu mama aondoke mwenyewe maana kaka hata hajigusi wala kumhofia maza. Nifanyeje wakuu
 
Si ulikuwa unaombea kaka yako aache kubadili wasichana abaki na mmoja sasa si kapata huyo jamani kaamua kutulia sasa tena hutaki!

Huyo mama wewe mwenyewe unamsifu msafi anafanya kazi za ndani pengine ndio sifa kaka yako alikuwa nataka hizo sasa tena hamumtaki!

Achana na mambo ya umri, muhimu wenyewe wanapendana na maisha yanaenda. Please achana na visichana vidogo havijajitambua bado.
 
pole..hilo janga la familia........bado najiuliza kweli kaka yako an over 35yrs unamlea kama mwanao.....kwanza hana adabu....unawezaje kumkazia dem nyumbani kwa shemeji yako....kwenye familia yenu malezi yenu yalikuwaje?? yaani dadako anakazwa chumba kile....na wewe unakaza chumba hiki.....hayo maradhi umeyalea mwenyewe....vumilia tuu si ni kaka yako.....
 
Familia yenu ina walakini kidogo, kaka yako kuishi kwako yan kwa shemejie, Hii kiafrica ni aibu sana, Bado analeta wake zake anawagongea hapo hapo, sasa katekwa na jimama kamleta hapo na anataka kufuga kuku heheheheee kasheshe, mama yako nae anakuja hapo huyo mume atakukimbia best, aisee Hii Kali pole sana, timua kaka yako huyo
 
Aisee mwanaume ana miaka 35 bado unaishi naye!!!!
tapatalk_1471242596986.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom