Msaada juu ya hii ndoto inayonitesa

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Oct 23, 2016
1,091
2,000
Hapo vip!!

Jamani kwa huzuni kubwa sana..naomba niwaeleze ndoto inayonitesa mara kwa mara...ila naamini Mungu(Jehova)ananipigania kila siku.

Nimekuwa nikiota ndoto ya kushangaza na imekuwa ikijirudia mara kwa mara ni takriba miaka mitano au zaidi.

Ipo hivi najikuta kama natoa uzi kwenye meno au kama ambayo naangaika kutoa..naivuta inakuwa ndevu haikatiki lakini baadaye inaanza kujiviringisha katika mkona wangu ina fika sehemu ikikatika inaanza kama kupita katika mkono wangu nakurudi katika mwili wangu.

Sometime naota kama natoa kitu kama bablishi katika meno yangu ila inakuwa ndefu sana kiasi kwamba inaanza kujiviringisha kwenye mkono wangu, na baadaye kung'angania kunirudia.

Jana nimeota navuta kamba iliuojivoringisha kwenye ulimi wangukama ila wakati naangaika kuvuta ikawa ndevu ikaviringisha katika mkona wangu na kuanza kunirudi kwa kutoboa kwenye mikono yangu.

Jamani naomba niishie hapo kwasababu nahisi kuumizwa sana na ndoto hii..nina amini humu kuna wataalam mbali na wenye uwezo wa kunisaidia kutafsiri na ushauri.

Naombe ushauri wenu.
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
170,195
2,000
Hii ina mahusiano ya moja kwa moja na maisha yako hasa kwenye changamoto za kipato ajira na umiliki.

Tafsiri ya jumla kuna vitu vya ndoto vyako unatakiwa kumiliki lakini kila ukijaribu kuvihodhi vinakutoka.
 

stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
12,294
2,000
Ndoto ikishakuwa inajirudia mara kwa mara ni ishara kuwa kuna kitu kizuri au kibaya kinakuja kutokea,mark my words. Ni vizuri ukafanya maombi ya kudhamiria ili upate ufafanuzi wa hiyo ndoto,na kama ni jambo baya basi uombe mwenyezi Mungu akuepushe nalo, you have to be serious on this.
 

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Oct 23, 2016
1,091
2,000
Ndoto ikishakuwa inajirudia mara kwa mara ni ishara kuwa kuna kitu kizuri au kibaya kinakuja kutokea mark my words.Ni vizuri ukafanya maombi ya kudhamiria ili upate ufafanuzi wa hiyo ndoto na kama ni jambo baya basi uombe mwenyezi Mungu akuepushe nalo,you have to be serious on this...
Noted Stephot
 

Banjuka

JF-Expert Member
May 7, 2021
442
1,000
Kabla ya kutafuta suluhu yeyote katika maisha yakupasa uwe na imani kwanza. Kama huna Imani hata wangeshuka Malaika ni kazi bure. Amini kwamba unayo haki ya kuwa na utulivu, Unayo haki ya kuota ndoto nzuri. Hutakiwi kuteseka tena kwa sababu Yesu wa Nazareti alilipia yote ili uwe huru, hivyo kama hujanwalika Yesu katika maisha yako. Mwite hata sasa anapatikana.
 

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Oct 23, 2016
1,091
2,000
Kabla ya kutafuta suluhu yeyote katika maisha yakupasa uwe na imani kwanza. Kama huna Imani hata wangeshuka Malaika ni kazi bure. Amini kwamba unayo haki ya kuwa na utulivu, Unayo haki ya kuota ndoto nzuri,Hutakiwi kuteseka tena kwa sababu Yesu wa Nazareti alilipia yote ili uwe huru, hivyo kama hujanwalika Yesu katika maisha yako, Mwite hata sasa anapatikana.
Amina
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom