Msaada jinsi ya kuandika talaka

Msaada jinsi ya kuandika talaka

Kibukuasili

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2010
Posts
1,053
Reaction score
616
Naomba mwenye kujua "format" ya kuandika talaka anifahamishe. Yaani heading yake inakuwaje, unaiadresi kwa nani, na vitu kama hivyo.

Sio kwamba mambo yameharibika, la. Napenda kujua tu
 
mzee unataka kutoa talaka?...talaka unajua ni nini kisheria?...TALAKA ni hati ya kuvunja mkataba wa NDOA kati ya wawili waliouingia...pia unatakiwa ujue kuwa kuna NDOA ZA AINA TATU hapa tanzania....Ambazo kwayo MIKATABA husainiwa
1- ndoa za kidini
2-ndoa za kiserikali
3- ndoa za kimila

NDOA ZA KIDINI- hapa ndoa hizi nazo zimegawanyika katika makundi mengi kulingana na uwepo wa imani tofauti kwa makundi tofauti
1- ndoa za kiislamu
2- ndoa za ki-kristo- hizi nazo ndio usiseme anzia romani katholic, sabato, walokole-hawa wapo kama makundi 100 huko mbeya

katika ndoa zote kuu 3 hizi za kidini huwa na complications katika kutoa talaka ila hizo mbili yani ya ki-mila na ki-serikali fasta n easy.

katika hizi za kidini ndoa za kiislamu ni rahisi kutoa talaka kuliko za ki-kristo, na katika za kikristo-ni ngumu sana kutoa talaka kwa makanisa ya kizamani(old school churches kama romani catholics) kuliko makanisa haya ya kizazi kipya...

hili la talaka mkuu unaweza kuandikia papper na ukawa Prf. wa talaka wa kutisha duniani
 
Naomba mwenye kujua "format" ya kuandika talaka anifahamishe. Yaani heading yake inakuwaje, unaiadresi kwa nani, na vitu kama hivyo.
Sio kwamba mambo yameharibika, la. Napenda kujua tu :=)

Mkuu nimeipenda sana signature yako
 
Naomba mwenye kujua "format" ya kuandika talaka anifahamishe. Yaani heading yake inakuwaje, unaiadresi kwa nani, na vitu kama hivyo.
Sio kwamba mambo yameharibika, la. Napenda kujua tu :=)

...:doh::closed_2: ...hapana bana. Binafsi si support mtu yeyote kukushauri hili. Kwanza talaka inamchukiza mwenyezi Mungu. Jamvi hili ni la kujenga, sio kubomoa.
Mpe nafasi nyingine Mkeo.
 
wanywaji utawajua tuu, yani ukimensheni pombe koo linataka!
Mhhh Lady N ungelijua hili kwamba kwa miaka 30 sijawahi kuonja balaa hili na kati ya miaka hiyo nina miaka 14 niko ndani ya Y.E.S.U.

si rahisi kwangu kuonja dude hili.

Lakini nilipata ufunuo tofauti na mawazo ya wanywaji katika signature hii.
 
Naomba mwenye kujua "format" ya kuandika talaka anifahamishe. Yaani heading yake inakuwaje, unaiadresi kwa nani, na vitu kama hivyo.
Sio kwamba mambo yameharibika, la. Napenda kujua tu :=)

Mimi mbona sielewi? "Format" ya kuandika talaka? Ndio nini hiyo?
 
Miye nilidhani unachora tu Mimi XYZ leo tarehe 24 July 2010 namuacha mke wangu ABC na hivyo kuanzia leo si mke wangu tena. Nadhani kunatakiwa kuwe pia na mashahidi wa kuthibitisha kwamba talaka ile imeandikwa na mhusika. Sikujua kama kuna format ya kuichora talaka.
 
naomba mwenye kujua "format" ya kuandika talaka anifahamishe. Yaani heading yake inakuwaje, unaiadresi kwa nani, na vitu kama hivyo.
Sio kwamba mambo yameharibika, la. Napenda kujua tu :=)

usione haya kusema hata kama ni wewe ikiwa yamekufika utaelezwa ila talaka kwa waislamu ina taratibu zake na jinsi ya kuandika nadhani ukienda bakwata utapata maelezo kamili kulingana na aina ya talaka yenyewe ila nadhani itakua unaiaddress kwa mlengwa.
 
Mzee wenzako wanatangaza ndoa kila kunapokucha, wewe unaulizia format ya talaka? Pole sana mkuu! Bila shaka yamekukuta. Raha au ugumu wa ndoa ni hadi hapo utakapoiingia. Mwamuzi wa mwisho ni wewe. Hawa wengine watakushauri, watawapatanisha lakini cha moto unakipata peke yako wao wakiwa hawapo. So pakifika mahali ambapo hapavumiliki, bora tu kuwa huru.
Kiujumla talaka haina regular format. Kuna watu wanaandika misitari miwili tu ya kwamba kuanzia leo sikutambui kama mke wangu. Mwingine anaandika kwa kurefer cheti cha ndoa, kwa hiyo anaanza kuandika kwa kuelezea kwamba mimi.... navunja ndoa iliyofungwa tar... kwa kutoa talaka tar... kwamba ... kutokana na.... nk nk. Lakini kuna wengine wanaamua kuiandika kisheria. Kwa hiyo unaweza kumtafuta mwanasheria akakuandikia kwa kufuata sheria za talaka. Lakini katika hali zote inategemea zaidi wewe ni mtu wa kariba gani.
Mwisho, kabla hujaamua kutoa talaka, mpe kwanza last warning. Kama ni tabia ya kawaida naamini atajirekebisha, labda kama ni uzinzi, huko siwezi kushauri lolote, maana machungu ya kumegewa bila shaka unayajua mwenyewe. Ila kama ni haya mengine jaribu ushauri wa biblia. Mshauri wewe peke yako, asipokusikia waite wazee wamshauri, asipowasikia lishirikishe kanisa, na kama hatalisikia hata kanisa, basi muache aende kwa amani.
 
Huku kwetu mwanamme anaweza sema ;;;you are divorced... and she will be divorced..no need paper no need witnesses ...:doh: but dont get me wrong..even after The divorce he is bound to take care of her and provide Financial support and proper accommodation mpaka aolewe na mwanaume mwengine....u aint gonna throw her outside :nono:...most of the cases men who are divorcing their wives without proper reasons, are the one who suffer the sequences...

Now Kibu I wonder why you wanna divorce your wife....
 
Wanajukwaa vitendo anavyonifanyia mke wangu nimeshachoka.

Ninachohitaji kutoka kwenu ni jinsi ya kuandika talaka tu, sihitaji ushauri wowote nimechoka na wala sitosikiliza ushauri wa yeyote yule.
 
Duh!, akaaaa mimi simo.

Halafu mnasema jukwaa la siasa ndio lina mastress? mimi nasema huku MMU ni stress kwa kwenda mbele. Wacha nirudi zangu siasani, humu sitii langu kwa leo.
 
Ww Mwambie Tu kuanzia sasa si mke wangu, tosha kabisa
 
Wanajukwaa vitendo anavyonifanyia mke wangu nimeshachoka.

Ninachohitaji kutoka kwenu ni jinsi ya kuandika talaka tu, sihitaji ushauri wowote nimechoka na wala sitosikiliza ushauri wa yeyote yule.

Acha mbwembe.
Anza hivi
Yah: Talaka
Mimi ..... Kutokana na sababu...... Nimeshindwa kukuvumilia kwa hiyo naamua kukupa talaka.
Ainisha aina ya talaka maana anaweza kubadirika ukamsamehe
Sahihi .....
Jina kamili.....
Tarehe......
Shahidi
Then kitu out
 
mimi Fulani bin Fulani nimemuacha bibi Fulani binti Fulani kwa talaka (taja kama moja mbili au zote tatu) kutokana na kadha kadha kadha. mpatie akaheme.

hairuhusiwi kutoa talaka zaidi ya moja kwa wakati mmoja! na hata akizitoa talaka zaidi ya moja kwa wakati mmoja, bado itasimamam kama talaka moja! mamaafacebook M. Mungu anajua zaidi!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom