Msaada jamani tumetekwa kasulu

Kama pia wameondoka na simu za habiria,ipo techology ya kuwapata,but cjui police wetu kama wana vifaa(japo ni so easy to do it) poleni sana wahanga wote wa tukio hili

Teknolojia unayosema wala siyo ya kununua au ya kutafuta. Teknolojia hiyo ipo kwenye kampuni za simu. Haitumiki mpaka Mtoto wa JK au kibosile fulani aibiwe ndo wanatumia. Kampuni za simu hazitimii labda sababu TCRA wamesinzia na wenyewe wapo after profit even at cutomers expense.

Equipment identity register (EIR): The EIR is a database for all IMEIs, i.e.,
it stores all device identifications registered for this network( eg Tigo, ZAIN Vodacom etc). As MSs are
mobile, they can be easily stolen. With a valid SIM, anyone could use the
stolen MS. The EIR has a blacklist of stolen (or locked) devices. In theory an
MS/ Mobile phone is useless as soon as the owner has reported a theft. Unfortunately, the
blacklists of different providers are not usually synchronized and the illegal
use of a device in another operator's network is possible (the reader may
speculate as to why this is the case)
. The EIR also contains a list of valid
IMEIs (white list), and a list of malfunctioning devices (gray list)......


source Book tiitled Mobile Comunication by JOCHEN SCHILLER

Kwa hiyo mtu akikuibia simu kama ilikuwa registered Tigo aliyeiba akiweka line ya Tigo Tigo wanafacility za kutambua. Pia Mobile company zingekuwa zinashare IMEI number ya simu zilizoibiwa basi walau simu iliyoibiwa isingeweza kutumika Tanzania.
 
Mmoja wa waliofariki kwa kupigwa risasi na hao majambazi ni Katibu wa vijana wa Ccm Musoma mjini Ndg Buga.RIP
...Ni kweli na inasemekana hata polisi wawili waliokuwa wakisindikiza hilo basi walitupa silaha zao na ku-craw na kuingia porini. Nadhani jeshi la polisi kuna haja ya kuangalia mbinu nyingine za medani kupambana na hawa jamaa kwani hii ya kuweka tu askari wenye silaha kwenye basi haitoshi. Majambazi wamekuwa wajanja na wana silaha nzito mno.Matukio yote ya ujamabazi kwenye njia ya kigoma/Kibondo/Nyakanazi polisi wanaosindikiza mabasi huingia mitini sasa sijui nini maana ya wao ku-escort basi.
 
Preta jana nilikuwa na muadi na mtu akaniyeyusha sasa nilivoona hii avarta yako nikawa natamani kama mapaja yanaweza kufunguka . Yaani ningekuwa jogoo ningezunguka mtaa mzima kutafuta. Anyway poleni mliovamiwa

Duh! hii kali, ndy maana hata kanisani watu wanapigana voko! Watu wameuwawa kwenye hiihii thread! na wengine wanatamaniana kwenye hii hii thread! R.I.H...., Oh! sorry R.I.P
 
Preta jana nilikuwa na muadi na mtu akaniyeyusha sasa nilivoona hii avarta yako nikawa natamani kama mapaja yanaweza kufunguka . Yaani ningekuwa jogoo ningezunguka mtaa mzima kutafuta. Anyway poleni mliovamiwa

pole sana kwa kuachwa mbuzi......labda alitaka kukuchuna akaona huna manyoya ya kutosha
 
...Ni kweli na inasemekana hata polisi wawili waliokuwa wakisindikiza hilo basi walitupa silaha zao na ku-craw na kuingia porini. Nadhani jeshi la polisi kuna haja ya kuangalia mbinu nyingine za medani kupambana na hawa jamaa kwani hii ya kuweka tu askari wenye silaha kwenye basi haitoshi. Majambazi wamekuwa wajanja na wana silaha nzito mno.Matukio yote ya ujamabazi kwenye njia ya kigoma/Kibondo/Nyakanazi polisi wanaosindikiza mabasi huingia mitini sasa sijui nini maana ya wao ku-escort basi.

Ile njia ni balaa! 2008 nilipanda basi ktokA MZA-KG, kwa lengo la kupunguza gharama! Escort tuliopewa ni fresh kutoka "depo", wawili wameshika SMG na magazine mbilimbili!!! mmoja nikakaa naye siti moja-nikawa namdodosa! Ndg yangu wanatimiza wajibu tu, tena wanaogopa kuliko hata sisi raia! wale wakimbizi wakt mwingne wanakuwa na LPG na magrenade! Njia nzima ni kujambajamba tu-mkivuka salama mnashusha pumzi! Ilinibd niache ubahili nitoe lak2.5 kupanda ndge to Dar!
 
jana nilikuwa njiani kutoka kasulu kuja mwanza ila safari ilikuwa iwe ya leo baada ya juzi kukosa basi la golden inter city nilitaka nihairishe safari nije leo na hilo basi, namshukuru mungu kwa hili pia nawapa pole hao ndugu zangu yani hiyo njia sijui serikali iko wapi mi sielewi
 
Kigoma kusafiri kwa basi ni kama kucheza bahati nasibu kama utavamiwa au la, mimi nikienda kigoma huwa natumia treni hata kama itakaa siku 3 bora usalama, nasikia hata barabara ya mwanza kwenda shy sehemu wanaita magambo napo hatari sana!
 
Habari wanaJF naomba msaada wa haraka kutoa taarifa kwa wahusika wa jeshi la polisi kwani kuna basi limetekwa mbele yetu zaidi ya nusu saa na hakuna polisi wala nini tuko kijiji cha makere wilaya ya kasulu tunasafiri kwenda Dar.

sali kabla ujasaliwa!!kwa hapa sijui kama msaada utawahi na ukifika nadhani kuna kamaumivu kameshawapitia si haba wahusika msaada ila we unaonekaana ujatekwa omba mungu wasilifikie gari lenu hao jamaa akuna tofauti na CCM roho zao mbaya zilivyo awachelewi kuwavua nguo wote bila kujali uko na mkweo..walishawahi kuwavua timu nzima ya wanandoa wakielekea MOSHI mpaka na bibi mzaa chema wacha mama mzaa chema baba waoto wajomba ni hatari mbaya nadhan walizaliwa porini
 
pole sana kwa kuachwa mbuzi......labda alitaka kukuchuna akaona huna manyoya ya kutosha

Preta bana watu tunaomboleza humu alafu wewe unaendeleza mijadala yako!
Si mwende kule kwenye jukwaa la Maria roza bana!
 
Habari wanaJF naomba msaada wa haraka kutoa taarifa kwa wahusika wa jeshi la polisi kwani kuna basi limetekwa mbele yetu zaidi ya nusu saa na hakuna polisi wala nini tuko kijiji cha makere wilaya ya kasulu tunasafiri kwenda Dar.

Pole sana Mu-sir, hiyo njia ina matatizo ya ujambazi zaidi ya miaka 10. Walikuwa wanasingizia wakimbizi lakini kwa asilimia kubwa wakimbizi wamerudi kwao na makambi yote Kibondo yamefungwa.

Inasemekana Jambazi mkuu alikuwa anagombea ubunge akapigwa chini, isijekuwa ameamua kulianzisha kwa hasira?
 
Hilo tukio ni la kweli, limeripotiwa sasa hivi na Radio one, Basi lililotekwa na la Wachina, na lilikuwa likitoka KGM kwenda MWZ. Ndani ya Basi hilo kulikuwa na Askari wawili wa Escort na bunduki mbili, ambazo zote zimechukuliwa na Majambazi pamoja na mali mbalimbali walizokuwa nazo abiria. Katika tukio hilo Abiria mmoja amepoteza maisha kwa kupigwa risasi na majambazi. Mhhh hali mbaya kweli kweli!!!!
 
Ile njia ni balaa! 2008 nilipanda basi ktokA MZA-KG, kwa lengo la kupunguza gharama! Escort tuliopewa Ndg yangu wanatimiza wajibu tu, tena wanaogopa kuliko hata sisi raia! wale wakimbizi wakt mwingne wanakuwa na LPG na magrenade!

Ni RPG mkuu.
Kimsingi wale askari huwa wanaangalia kwanza siraha walizokuwa nazo adui.
Kama adui ana siraha kali zaidi ni lazma askari asalimu amri na hilo wala tusiwalaumu.
Kikubwa askari wawe wa kutosha na ikiwezekana mmoja wao abebe ile siraha ya 'msaada' yenye mkanda.
 
Hiyo silaha yenye mkanda hawawezi pewa polisi kwani itahatarisha na usalama wa mafisadi...mapolisi wengi wanawachukia mafisadi ila basi tu wafanye nini na mafisadi pia wanalijua hilo...kamuuulize Masha Mwanza kwani naye wamemfanyizia kiaina ktk uchaguzi alitegemea sana kuwatumia kama walivyofanya Karagwe
 
Eti nchi ya amani wakati kumbe mabasi ya kigoma yanalindwa na askari wawili kila siku!hapo kuna amani?tumekua philipines!majambazi ya leo ni balaa hao saizi yao jwtz.
 
Kuna thread nyingine kule inasema kuwa kuna kiongozi mmoja wa CCM Mara ameuawa na majambazi akiwa safarini kutoka Kigoma kwenda Mwanza. Isije ikawa hii...?
 
uuuh...poleni sana najua mlipata mitikisiko ya moyo....hiyo hali huwa inatisha sana......huyo jamaa aliyekufa ni abiria wa hilo basi lililotekwa au ni kati ya hao polisi?

aliyekufa ni abiria polisi wote wamekimbia.
 
Polisi aliyekuwa akisindikiza basi amepona au basi halikuwa na askari wa kusindikiza mwenye silaha??

polisi aliyesindikiza gari ndio hao escort wawili waliotupa silaha na kukimbia kusikojulikana so bunduki za askari waliondoka nazo watekaji.
 
aliyekufa ni abiria polisi wote wamekimbia.

nasikia redion pia wametangaza......ni jambo la hatari sana......na kama polisi wanakimbia sijui hii serikali yetu inawaza nini kuhusu hilo coz inaonyesha jeshi halina silaha za kujitosheleza au hailichukulii hili swala kwa uzito, wao ilimradi wakubwa wanapaa na ndege nyie mliosalia mtajijua....poleni sana atakayewalinda ni Mungu
 
Pole sana, ndo naona wajumbe wanatuma taarifa sasa ivi kuwa mtu huyo mmoja aliyeuwawa ni katibu wa CCM kigoma Wily Muga.
 
Back
Top Bottom