Msaada: Hili ni tatizo gani?

Kayoka

JF-Expert Member
Jun 21, 2011
2,239
1,884
Habari Madaktari na wanadau wengine huku ndani.

Kama wahenge wasemavyo "Mficha maradhi Kifo Humuumbua" nipo njiani narudi tena hospital kuonana na daktari kufanya uchunguzi na kupata matibabu lakini ningependa kuwashirikisha na naomba msaada wenu juu ya tatizo langu.

Siku ya Jumapili nilianza kuoana dalili ambazo si za kawaida kwenye dhakari (uume) wangu kama vile maumivu makali wakati wa kukojoa, kukojoa mara kwa mara, kuwasha kwenye kichwa na kujitotokeza vipele vidogo vidogo mithili ya kama vile mba mweusi pia mwili mzima ukiwa na joto, na kuumwa kichwa.

Nikaenda hospital na kupima (mkojo na choo nikaambiwa hakuna shida), BS nikaambiwa malari wadudu wanne nikapewa dawa (Malafin & Diclofenac) na kuanza kuzitumia, nashukuru Mungu nimepata afueni na naendelea vizuri.

Lakini sasa ile hali ya kwenye dhakari kuwa na vipele na baka jeusi bado imezidi kusambaa huku nikipata maamivu, sasa naomba msaada wenu wataalamu niweze kujua taizo hili na namna ya kupata matibabu yake na nini naweza kumueleza daktari kwa uchubguzi zaidi.

Status yangu "NAISHI NA MKE"
 
Pole mkuu!

Umechepuka hivi karibuni?

Anyway, hizo ni dalili za gonorrhea(inaonekana bado ni hatua za awali) ingawa yaweza kuwa syphilis pia.

mchukue wife mwende pamoja hospital , wambie wawapime gono na VDRL ,, ni rahisi kutibika ktk hatua hizi za awali.
ugua pole.
 
πŸ™„πŸ™„πŸ™„πŸ˜²πŸ˜²πŸ˜²πŸ™ˆπŸ™ˆπŸ™ˆ hata kama bwana hebu futa hio picha,kuwa na aibu kidogo.Ungeenda hosp kubwa umweleze doctor vizur.
Yuko hapa kutaka kupata ushaurinwa daktari..Hili si jukwaa la afya?πŸ˜€

Ila ushauri aende hospital na akumbuke kuvaa condom next time kuepusha magonjwa ya zinaa.

Syphilis is really vijana kuweni makini. Kuna magonjwa mengine ya ngono hatari yasiyo na tiba.
1. Hepatitis B
2 HIV
 
Habari Madaktari na wanadau wengine huku ndani.

Kama wahenge wasemavyo "Mficha maradhi Kifo Humuumbua" nipo njiani narudi tena hospital kuonana na daktari kufanya uchunguzi na kupata matibabu...
πŸ™„
Pole sana!
 
  • Kwa tatizo la ndani, wacheki UTI na mengineyo uanze dozi mara moja, wewe na mkeo
  • Kuhusu muonekano wa nje, unaweza kutumia BBE kwa kupaka na hali kurejea kuwa kawaida.
 
Yuko hapa kutaka kupata ushaurinwa daktari..Hili si jukwaa la afya?πŸ˜€

Ila ushauri aende hospital na akumbuke kuvaa condom next time kuepusha magonjwa ya zinaa.

Syphilis is really vijana kuweni makini. Kuna magonjwa mengine ya ngono hatari yasiyo na tiba.
1. Hepatitis B
2 HIV
Sawaaa sijakataa anataka ushaur,ila angejitahid kueleza kadir awezavyo humu hakuna mtoto tungeelewa tu jaman,siyo kuona mipin asubuh asubuh nimeshtuka 🀭🀭🀭πŸ€ͺπŸ€ͺ,afu nipo karibu na wababa wa watu hapa πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†naangalia hii picha nawaangalia na wao naona kama hawajavaa tu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
kumbe unapenda vizeeπŸ˜€πŸ˜ƒ

Kuna siku katika purukushan za game penis Ikalia taaa maumivu yake sio ya nchi hii
Nikaend modem manzese hospital πŸ₯ nikakuta mzee mmoja daktari sasa nikamuelezea mwisho nataka nivue ninwonyesh yule Mzee daktari aligoma kata kata hakutaka kabisa akawa ananichorea nimpe mifano🀣🀣 mwisho akasema yeye ni dokta wa kawaida sio specialists wa haya mambo ni schedule jumamosi kuna ma specialists.

Akanambia nikakandanxenna maji chumvi moto na ninywe panada kesho nije kumuona daktar
Baadae nikaona maumivu yameisha nikapotezeaπŸ˜€ inawezekana ndio maana mpaka leo imepinda🀣
 
Pole mkuu!

Umechepuka hivi karibuni?

Anyway, hizo ni dalili za gonorrhea(inaonekana bado ni hatua za awali) ingawa yaweza kuwa syphilis pia.

mchukue wife mwende pamoja hospital , wambie wawapime gono na VDRL ,, ni rahisi kutibika ktk hatua hizi za awali.
ugua pole.
Mkuu,
Asante kwa ushauri wako, nitawajuzeni baada ya kuonana na daktari na kupata matibabu.
 
Sawaaa sijakataa anataka ushaur,ila angejitahid kueleza kadir awezavyo humu hakuna mtoto tungeelewa tu jaman,siyo kuona mipin asubuh asubuh nimeshtuka 🀭🀭🀭πŸ€ͺπŸ€ͺ,afu nipo karibu na wababa wa watu hapa πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†naangalia hii picha nawaangalia na wao naona kama hawajavaa tu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Nisamehe sana,

Ni kwa ajili ya matibabu tu sina maana nyingine.
 
Pole sana.

Ijapokuwa hujaeleza wazi ni vipimo gani daktari alikuandikia. Hujatuelezea pia historia yako ya hivi karibuni ya ushiriki wako wa tendo la ndoa.

Kwa dalili hizo, yafuatayo ni baadhi ya maradhi ambayo huenda umeambukizwa. Kupata uhakika, ninakusihi upate vipimo sahihi.
1. Genital Herpes
2. Gonorrhea
3. UTI

Dawa utaandikiwa kulingana na majibu ya vipimo. Kama hukushiriki tendo na mtu mwingine isipokuwa mkeo, basi mchukue muende wote katika kituo cha afya kwa uchunguzi zaidi.

Nakutakia uponyaji mwema.
 
Pole sana.

Ijapokuwa hujaeleza wazi ni vipimo gani daktari alikuandikia. Hujatuelezea pia historia yako ya hivi karibuni ya ushiriki wako wa tendo la ndoa...
Natamani sana kueleza yote ila nimejaribu kusema kwa ufupi;

Mara ya kwanza nikipita Stool, Urine na BS.

Mimi na mwenzangu tulishiriki tendo la ndoa mara ya mwisho siku ya ijumaa last week.

Nashukuru sana Dr kwa ushauri wako.
 
Ulimuonesha daktari dhakari yako na kumuelezea unavyojisikia? Sikuona sababu ya kupima stool. Urine okay.

Nakusihi leo uende tena kwa uchunguzi zaidi. Usimsahau mwenza wako kama una uhakika hukufanya na mwingine yeyote. Inawezekana yeye ndiye mwenye shida. Kujitibu huku ukimuacha yeye, ni kupunguza tu tatizo. Siyo kulimaliza kabisa.
 
kumbe unapenda vizeeπŸ˜€πŸ˜ƒ

Kuna siku katika purukushan za game penis Ikalia taaa maumivu yake sio ya nchi hii
Nikaend modem manzese hospital πŸ₯ nikakuta mzee mmoja daktari sasa nikamuelezea mwisho nataka nivue ninwonyesh...
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€£πŸ€£πŸ€£ nyie Kuna watu mna mambo,ila nimecheka
 
Back
Top Bottom