Msaada: Hawa mtu na mkewe siwaelewi kabisa

Msaada: Hawa mtu na mkewe siwaelewi kabisa

Nataka nimchukue ndugu au rafiki yangu mmoja nimhadithie hii issue, pili nichunguze wanakaa wapi hawa watu sna nimuonyeshe huyo ndugu yangu, Kisha ndio nifikirie kama naweza kukutana na huyu mdada huku jamaa yangu akiwa anafuatilia kimya kimya.

Ndugu yangu Shark huko kote kwanini kuzunguka hivyo na kujipa makazi mengi yasiyo na maana, wewe ni kidume baba mface mwanaume mwenzio muulize mweke mtu Kati akupe yake kisha temana nao na mizigo yao wape waambie wewe si wa kihivyo wakuchukulie poa tu, na mpe warning hizo biashara na wewe waziache kabisa la sivyo.....malizia mwenyewe.

Pili uje umshirikishe ndugu au Rafiki yako wakati wewe kama wewe ushachukua hatua, na huko mahali anakokupea vitu vyake kama ni sehemu ya Kula unaweza badilisha kama mbadala upo ukawa unaenda sehemu nyingine hapa ni kiusalama zaidi.

Hata kama hitaji ni mtoto Ina maana miaka yote hiyo huyo mwanamke alikuwa anakungoja wewe tu? Kashindwa vipi kuchepuka huko kwingine kote azingoje sperm zako tu na kazijuaje zako ndizo zenye mtoto,na anamshirikisha mumewe, Wacha kabisa upumbavu huu peleka huko.

Siku hizi baba hela inatafutwa kwa udi na uvumba, poteza hela pata hela, kama si ushirikina basi ni dili la pesa mzee, na kama ndo unakijiuwezo chako na wanajua hapo job uko sekta nzuri ya mpunga na wana uhakika na salary yako nenda huko kakutane na huyo mwanamke ushushiwe jumba bovu la fumanizi, utafilisiwa hadi boxa uliyovaa,heshima yako yote kushney , hiyo case ya fumanizi ndo itakuwa fimbo ya kukuchapia kila wanachohitaji kutoka kwako wapate ili wewe ulinde tu heshima yako.

Haya ni baadhi tu yapo mambo mengi yanayoweza kuwa suspected. Stuka baba stukaaaa!!! Hii ni dunia, mjini shule......
 
Last edited by a moderator:
Wajua kujirusha na mke/mme wa mtu sio mbaya, but why mawasiliano yapitie kwa mumewe? Nina uhakika mumewe hua hafunguagi bahasha za mkewe?
Kuna mtu kaniambia sheria inasema mtu akifumaniwa inabidi alipe hela kiasi fulani, haiwezi kua napangiwa kufumaniwa ili nilipe fidia??
Mkuu..., hao hawana haja na hela zako!! Wao wana haraka na pupa za kutimiza ahadi za Mganga/mchawi wao !!!

(halafu nani kasema adulterysiyo mbaya ? Ni dhambi na crime)
Usisogelee....
 
story kama nilishazisikia na wote walikuwa wanafanya hivi ili wapate mtoto na huyo mumewe anapokuharakisha ni kuwa kipindi hiki huyo mkewe yupo katika kipindi kizuri chakushika ujauzito...yawezekana story ikawa zinajirudia kwako
 
The point kuwa una-contemplate kukutana na huyo mwanamke inanihuzunisha mno.
Shark i thought u r smarter than that. Sijitii ujuaji sana ila katika ujana wangu wote sikuwahi (na nilijiapiza) kutoka na mke wa mtu. Ya nini yote hayo. Kama ni tamaa za mwili mbona wapo mabinti wazuri tu wengi unaweza kutafuta mmoja....ni lazima mke wa mtu kweli!??

No brother..don't stoop that low please....please! Achana na mpango wowote uliokuwa nao..the fact kuwa ni mke wa mtu iwe sababu tosha kwako kusema NO! Don't be that weak...

Remember; curiosity killed the cat!!!
 
Last edited by a moderator:
Hicho ndo cha muhimu. Me nahisi huyo mumewe anajua kinachoendelea. Mume gani ambaye atapewa ujumbe na mkewe uende kwa mwanaume mwingine kila siku na hata asiufungue? Kuna kitu wamekipanga juu yake


Binadamu sio wema tena dunia imekuwa uwanja wafujo

Afanye uchunguzi taratibuuuuu asijekuwa na papara ya free p ikamcost maishani kwake
 
Shark wallahi nimecheka sana...sijui ni hadithi njoo urongo njoo au kweli..lakini yote kwa yote imenichekesha...no comment!!!
Wadau,

Kuna Jamaa mmoja tunafanya kazi ofisi za karibu hapa Town hivyo sometimes tunakutana Lunch hour kwenye menu jirani na tunapofanyia kazi, na bahati nzuri zaidi Mke wa huyu jamaa alikua class mate wangu wa primary ila hatukua na mazoea kivile kipindi hicho. Jamaa hatujazoeana kihivyo ila tunajuana tu kwa sura na ofisi tunazofanyia kazi.

Kama miezi miwili nyuma ofisini kwa huyu jamaa kulikua na family day ambapo ndugu wa staff wa ofisi yao walikua wanakutana ofisini kisha wanaenda wenyewe kuspend wanakokujua ndio nikabahatika kumuona mkewe huyu jamaa tukasalimiana na mkewe, na tukatambulishana na jamaa pia mambo yakawa poa.

Issue ilikuja kua baada ya siku chache after ile shughuli yao, yule jamaa akawa ananitafuta, kuonana akanipa namba ya mkewe kwamba ananitafuta. Mi kumpigia mkewe akadai kua alikua ananizimikia toka primary na anashukuru sana ameniona. Anataka japo tuwe wapenzi a.k.a michepuko tu. Kusema ukweli sikutaka kumsikiliza nikakata ile simu na nikawa sipokei tena simu yake. Next day yule jamaa (mumewe) akanifuata ofisini kuniambia Mkewe analalamika kwanini nilimkatia simu jana yake.

Baada ya kama wiki hivi yuleyule mumewe akanipa na bahasha imepigwa stapler, kuifungua ni ujumbe kutoka kwa mkewe kua ananipenda sana na anataka tuwe wapenzi. Kaweka na $70.00 pamoja na siku + direction ya kukutana mahali nikifika nilipie chumba tufanye yetu. Yaani ujumbe huu umepitia kwa mumewe!!!!!!!!!!!!!!. Nilishangaa sana nikasema huu mtego ama vipi. Jioni yake nikapata msg kutoka kwa mkewe kuulizia kama nilipata ujumbe kupitia kwa mumewe, nikamjibu kua niliupata ila nitampa jibu.

Kesho yake wakati niko lunch nakula, mume wa yula ex-mate akaja kuniuliza kua why simjibu mkewe mpaka ye anasumbuliwa kila mara kunitafuta. Nilitaka nimuulize kama anajua kitu kinachozungumziwa ama lah ila nikasita. Nilimjibu tu kua nafuatilia nitamjibu mkewe nilipofikia. Nikamuuliza mkewe kwanin anawasiliana na mimi issue za kuchepuka kupitia mumewe? anamchukulia vipi mumewe? Ni ----- ama vipi.

Sasa jana nimepewa appointment kua wikiend hii tukutane hoteli fulani hivi, ujumbe umekuja kupitia kwa yuleyule mumewe lakini kupitia bahasha, na safari hii ameweka $100.00 na Tshs 50,000/= ya hoteli na Taxi. Tena Mumewe kasisitiza niharakishe hii issue (anaijua???) iishe mapema maana yeye amechoka kusumbuliwa. Nimeshindwa kuwaelewa hawa Mtu na Mkewe, sielewi huyu jamaa ni ----- kihivyo au kuna mipango inaendelea nyuma ya pazia. Wadau naombeni ushauri wenu, niko njia panda!!
 
Kwel amuulize huyo mumewe kama anajua yy na mke nini kinachoendelea au kutaka kutokea

Sidhan kama mumewa atakubali hata kama anajua kinacho endelea.
Tafuta bahasha kubwa weka ishu zao mpe mumewe ampelekee. Na fuata maisha yako achana nao. Haijalishi nia yao ni ipi ila sio nia mzur
 
Hata kama mumewe hajua unafkili akija jua atachukuliaje. Kupigiwa kitu kingine et. Na hata kama ni msaada wa kuwapatia watoto sio kwa dizaini hiyo et.sikushauri utongoze matatizo
 
Kuna mawili hapo:-
-labda wanataka mtoto na wanafikiri hiyo ndio njia sahihi
-Au wamepewa masharti na mganga kuwa wamtumie mtu mwenye sifa kama zako.

ILA Habari njema ni kwamba ukiwa upande wa MUNGU kikwelikweli:-

-Kwanza: hautazini na huyo Mwanamke.

-Pili, Huo ushirikina hautakupata.
 
Hizi hadithi za abunuasi nilizani zilishatoweka kitambo kumbe bado zipo, haya bana ushaur umepata endelea kutujuza mapya zaidi.
 
Wajua kujirusha na mke/mme wa mtu sio mbaya, but why mawasiliano yapitie kwa mumewe? Nina uhakika mumewe hua hafunguagi bahasha za mkewe?
Kuna mtu kaniambia sheria inasema mtu akifumaniwa inabidi alipe hela kiasi fulani, haiwezi kua napangiwa kufumaniwa ili nilipe fidia??

Kujilusha na mke wa mtu ni jambo baya sana tena hatarii.just imagine upigiwe mkeo utajickiaje afu istoshe mtu mwnyewe upo nae kwa kazi.
Zinaa ni deni ukizini ww anakulipia mtu wako wa karibu.
Ningelikuwa mimi ningewapotezea mazima
 
Sio kwamba mumewe ni Mume-bweg.e au anamuamini sana mkewe? Au nae ananiona mimi ndio bweg.e karibia naingia mkenge? Nimefikiria nimuulize huyu jamaa kama anaaelewa tunachozungushana na mkewe muda wote lakini roho inasita.

mwulize mmewe kwa upole na unyonge. anza kwa kusema mambo yamebana kishenzi lkn unajitahidi utatimiza. hafu mchomekee, kuwa unaamini anaweza kukusaidia kufikia conclusion. na je unajua alichonituma kufanya? atakalo sema, itikia kama ndo lenyewe
 
katika hali ya kawaida, mwanaume huwez tumwa tumwa kwa mwanaume mwenzako tena kupeleka bahasha unless unajua kinachoendelea (au hata hisia)!
Kwa kifupi nina wasiwasi na huyo jamaa, possibly ni bwabwa
Au hadindi na anahitaji mtoto. Nimefikiria pia au wanaheshimiana Privacy issues za kila mmoja wao.
 
Wanataka watimize masharti ya mganga wao ili watusue kimaisha. Ww nenda tu hotelini,then njoo utupe feedback.
 
Sasa Kiongoz Wew Unataka Ushauriwe Nin Coz Kila Kitu Kipo Waz Na Nakushauri Urudishe Pesa Zote Ulizopewa Kabla Hujawa Mteja Wa .......
 
Sidhan kama mumewa atakubali hata kama anajua kinacho endelea.
Tafuta bahasha kubwa weka ishu zao mpe mumewe ampelekee. Na fuata maisha yako achana nao. Haijalishi nia yao ni ipi ila sio nia mzur

Hizo issue zao kama ni hela nimeshazila, hata $100 za Jana nishazibadili zote naa nimelipa mahali. Kwakua sikuwaomba zile hela na wala hawakunipa kwa dispatch basi nimedhani ni halali yangu.
 
Back
Top Bottom