Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,973
- 30,154
Wadau,
Kuna Jamaa mmoja tunafanya kazi ofisi za karibu hapa Town hivyo sometimes tunakutana Lunch hour kwenye menu jirani na tunapofanyia kazi, na bahati nzuri zaidi Mke wa huyu jamaa alikua class mate wangu wa primary ila hatukua na mazoea kivile kipindi hicho. Jamaa hatujazoeana kihivyo ila tunajuana tu kwa sura na ofisi tunazofanyia kazi.
Kama miezi miwili nyuma ofisini kwa huyu jamaa kulikua na family day ambapo ndugu wa staff wa ofisi yao walikua wanakutana ofisini kisha wanaenda wenyewe kuspend wanakokujua ndio nikabahatika kumuona mkewe huyu jamaa tukasalimiana na mkewe, na tukatambulishana na jamaa pia mambo yakawa poa.
Issue ilikuja kua baada ya siku chache after ile shughuli yao, yule jamaa akawa ananitafuta, kuonana akanipa namba ya mkewe kwamba ananitafuta. Mi kumpigia mkewe akadai kua alikua ananizimikia toka primary na anashukuru sana ameniona. Anataka japo tuwe wapenzi a.k.a michepuko tu. Kusema ukweli sikutaka kumsikiliza nikakata ile simu na nikawa sipokei tena simu yake. Next day yule jamaa (mumewe) akanifuata ofisini kuniambia Mkewe analalamika kwanini nilimkatia simu jana yake.
Baada ya kama wiki hivi yuleyule mumewe akanipa na bahasha imepigwa stapler, kuifungua ni ujumbe kutoka kwa mkewe kua ananipenda sana na anataka tuwe wapenzi. Kaweka na $70.00 pamoja na siku + direction ya kukutana mahali nikifika nilipie chumba tufanye yetu. Yaani ujumbe huu umepitia kwa mumewe!!!!!!!!!!!!!!. Nilishangaa sana nikasema huu mtego ama vipi. Jioni yake nikapata msg kutoka kwa mkewe kuulizia kama nilipata ujumbe kupitia kwa mumewe, nikamjibu kua niliupata ila nitampa jibu.
Kesho yake wakati niko lunch nakula, mume wa yula ex-mate akaja kuniuliza kua why simjibu mkewe mpaka ye anasumbuliwa kila mara kunitafuta. Nilitaka nimuulize kama anajua kitu kinachozungumziwa ama lah ila nikasita. Nilimjibu tu kua nafuatilia nitamjibu mkewe nilipofikia. Nikamuuliza mkewe kwanin anawasiliana na mimi issue za kuchepuka kupitia mumewe? anamchukulia vipi mumewe? Ni ----- ama vipi.
Sasa jana nimepewa appointment kua wikiend hii tukutane hoteli fulani hivi, ujumbe umekuja kupitia kwa yuleyule mumewe lakini kupitia bahasha, na safari hii ameweka $100.00 na Tshs 50,000/= ya hoteli na Taxi. Tena Mumewe kasisitiza niharakishe hii issue (anaijua???) iishe mapema maana yeye amechoka kusumbuliwa. Nimeshindwa kuwaelewa hawa Mtu na Mkewe, sielewi huyu jamaa ni ----- kihivyo au kuna mipango inaendelea nyuma ya pazia. Wadau naombeni ushauri wenu, niko njia panda!!