Kutumia miguu miwili AUTO? labda udereva wa vichochoroni, Auto Mguu mmoja wa kulia unatosha, sababu kubwa ukitumia mguu wa kushoto kwenye Break hautakuwa umekaa vizuri au kama miguu yako inamatege is okey.Kumbe sikutaja aina ya transmission, ni auto mkuu. Wengi wanaotumia auto hutumia miguu yote, wakushoto breki na kulia mafuta. Wengi wanaotumia mguu mmoja wakati wakuendesha auto hujikuta kosa moja goli, wengi wanafanya hivyio ili kuepuka kupata ajali ya kugonga gari la mbele yako hasa kwenye foleni. Unaweza kufikiri unakanyaga breki kumbe mguu hujaamisha vizuri kutoka kwenye mafuta.
Itakuwa forester subaRu kwakweli wenye hizi gari wapeni heshima tena kwa dar na foleni inameza lita kwa 3km.wakienda sheli mafuta yao akiweka ya bei ndogo ni laki unappoagiza gari uwe unauliza fundi haswaa kwny upatikanaji wa spea na ulaji mafuta.
Yaani nadhani kati ya km nne au tano kwa lita moja. Wafundi wanasema nibadilishe nozzle niweke za tundu mbili maana zilizopo ni nne. Je itasaidia?
hata hizi auto mara nyingi kule upande wa kushoto kuna kadubwana fulani wamekaweka kanakuwa kanasupport mguu kama vile gari za manual ila hiyo ya mguu wa kushoto kukanyaga brake na kulia kukanyaga mafuta ndo nausikia leo.. yawezekana mkuu hukupitia veta nini...
KUna nyingine nimeiona huko nyuma jamaa kaandika Overwhole akiimaanisha OverHAUL!sio cratch ni clutch
sio break ni brake
Mkuu kuna dada mmoja hapa ofisini kwetu alimuona mwenzake amechukua Toyota Klugger naye akajitosa akaagiza Subaru Forester, ameitumia toka kwake Kimara mpaka Posta hata mwaka haujaisha ameipaki hapa ofisini amekopa akachukua Vitz sasa hizi anakula kiyoyozi wakati ule wa Subaru alikuwa anaogopa hata kuwasha kiyoyozi.Arusha hizi SUBARU FORESTER ziko nyingi sana, nadhani hawa jamaa watakua ni watu wa ''mawe'' (Merelani) au ni kule kuigana halafu baada ya hapo mtu anakufa na tai shingoni. Eti utasikia zinakimbia sana, sijui mtu utasafiri mara ngapi hizo safari ndefu za kuhitaji ukimbie?
Mkuu kuna dada mmoja hapa ofisini kwetu alimuona mwenzake amechukua Toyota Klugger naye akajitosa akaagiza Subaru Forester, ameitumia toka kwake Kimara mpaka Posta hata mwaka haujaisha ameipaki hapa ofisini amekopa akachukua Vitz sasa hizi anakula kiyoyozi wakati ule wa Subaru alikuwa anaogopa hata kuwasha kiyoyozi.
Nimesikia nyepesi nyepesi anatafuta mteja wa Subaru.
Ngoja nifuatilie halafu nitakufahamisha mkuu, ina namba series ya T...CA.anauza shing ngapi mkuu?
anauza shing ngapi mkuu?
Cheki plug kwa petrol na pump/nozzle kwa diesel, piaweka air cleaner mpya genuine....otherwise gari chakula chake kikuu mafuta....lazima ile ili itembee ... au fuata ushauri wa bujibuji...isilimishe....
Mkuu, toa information kamili ili upate msaada. Wataalam wapo.
1. Gari gani
2. Ya mwaka gani
3. Size ya Engine
4. Diesel, Petrol au Mafuta ya Korosho
5. Automatic of Manual Transimmission
Ukianzia hapo msaada utapatikana mkuu.
Mi bado ntakukatalia kuhusu hoja zako hasa unaposema mguu wake wa kushoto una nguvu. ...mimi mwenyewe natumia kila kitu kushoto toka utoto wangu lkn linapokuja suala La kudrive wala huitaji nguvu nyiiiingi kukanyaga pedal. ...gari yenyewe hata ukiwa kwenye foleni hata usipokanyaga mafuta bado utakuwa inasogea sasa kuna haja gani ya kutumia miguu miwili?
Wewe unaendeshaje hiyo Auto? Jaribu kumshauri mke wako aache kutumia mguu wa kushoto kukanyaga brake, hii imetokana na kuanzia kuendesha gari ya Auto, you never know kuna siku atakuja kwenye manual transmission hapo ndo kitakua kimbembe. Angeanza na gari ya manual hicho kitu usingekiona. Lakini mzee na wewe huoni huo ukakasi ukiwa naye anapokanyaga brake kwa mguu wa kushoto??? Usichukulie kwamba amekua ktk hali hiyo kwa 10 years bila shida, rekebisha hilo ni TATIZO.